Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

MY CRAZY HOUSE GIRL* *______________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

25th Aug, 2025 Views 39



Asubuhi ilipofika Damian alikuwa macho siku hiyo hakulala usingizi mzuri Alikuwa akifikiria makbo anayofanya Vanessa na licha ya kuwa anamkosea lakini hawezi kumfukuza .
" Huyu msichana sijui kampa nini mama inaonekana mama anampenda sana hasikii chochote kutoka kwangu . Ila akiendelea kuniletea ujinga wake nitakifukuza nyumbani kwangu bila kujali chochote hawezi kunipangia jinsi ya kuishi wakati mimi ndio boss hapa.

Alinyanyuka pale kitandani na kwenda bafuni kuoga, kisha alivaa suti yake na kushuka chini akaelekea jikoni. Huko alimkuta Vanessa tayari amevaa apron yake, akihangaika na vyombo huku sauti ya muziki wa taratibu ikicheza. Harufu nzuri ya kahawa ilitawala jikoni.
Vanessa aliposikia hatua, aligeuka na kumwangalia.
"Good morning boss wangu.
Leo nimekuandalia kahawa na toast Au bado unaendelea na hasira ya jana?"
Damian alimpotezea, akavuta kiti na kukaa kimya. Vanessa alimmiminia kahawa na kuiweka mezani kisha akaegemea mezani huku akimuangalia.
"Boss kuna kitu kinakutesa?

"Vanessa, sitaki maneno yako ya asubuhi subuhi.
"Sawa boss, lakini kumbuka sio kila anayekuchokoza anakuchukia. Wengine wanataka ujue hisia zao moja kwa moja.
Damian aliinua macho, akamkazia Vanessa kwa sekunde kadhaa, kisha akanywa kahawa kimya kimya. Alinyanyuka na kuchukua begi lake.
"Leo sitaki vituko vyako, Vanessa. Ukiendelea utajuta."
"Asante kwa onyo, lakini bora ukaondoka na moyo wako ukiwa mweupe hasira zote ziache hapa nyumbani.
Damian alimtazama kwa sekunde mbili, akatikisa kichwa kisha akatoka nje na kufunga mlango kwa nguvu. Vanessa alitabasamu kwa ushindi mdogo, kisha akarudi jikoni kuendelea na kazi zake huku akiimba kwa furaha.

Baadaye jioni, Damian aliporudi nyumbani, alipokelewa na harufu ya chakula kilichopikwa vizuri. Alikuta meza tayari imeandaliwa , taa za sebuleni zimezimwa na mwanga hafifu wa mshumaa uliwaka na red wine ilikuwa mezani .
" Huyu Vanessa kafanya haya kwaajili ya nani?
Ngoja nimfuate hukohuko.
Kabla hajapiga hatua Doreen alitokea ghafla kutoka chumbani akiwa amekunja sura yake
"Hi baby, kumbe upo hapa? Damian alimsalimia.
"Hi. Huyu house girl wako anataka kuwa first lady wa hii nyumba au?
" Kwanini, akifanya nini?
" Ameniambia mambo ya ajabu sana .
" Unatakiwa kumpuuzia. Alafu nimefurahi sana kwa haya maandalizi ukiyonifanyia. Pia leo kwa mara ya kwanza nitakupa chakula nilichokuwa na mpenzi wangu.
"Hii meza imetandikwa na huyo maid wako kana kwamba ni Valentine!"
" Vanessa ndio kafanya haya yote?
" Ndio inaonekana kuwa wewe na yeye ni wapenzi na sijui kwanini unaning'ang'ania.
" Hakuna kitu kama hicho yeye ni mfanyakazi tu. Kwanza achana na mambo yake njoo tule.
"Hapana Damiani, kashaonyesha tabia yake. Mimi leo sili hapa. Nitaagiza chakula changu."
Doreen alirudi chumbani na kujifungia. Damian alikaa kimya, akainua grass ya wine na kunywa kidogo huku akimwangalia Vanessa aliyekuwa amesimama pembeni kwa tabasamu hafifu.
"Ningesema pole, lakini najua hutaelewa ni pole ya nini" Vanessa alisema.
"Vanessa... mimi ni mtu mzima. Sina muda wa michezo. Acha kunipima."
"Sijakupima, boss. Wewe mwenyewe umejiweka kwenye mizani."
"Sasa unataka nini kutoka kwangu? Umekuwa kama kivuli changu. Kila nikigeuka, uko hapo."
Vanessa alisogea karibu naye, akaegemea mezani huku macho yake yakimtazama kwa jicho la kutaka kuingia ndani ya moyo wake.
"Mimi sitaki pesa zako. Sitaki mali zako. Nataka kitu ambacho kila mwanamke wa kweli anakitaka... moyo wa mwanaume anayempenda."
Damian alibaki ameduwaa. Hakutarajia kauli kama hiyo.
" Unamaana gani wewe mwanamke mjinga?
Usiniambie kama unanitaka.
Vanessa alicheka kwa sauti kubwa
" Damian utakimbia leo, kesho na keshokutwa. Lakini moyo wako siku moja utachoka kukimbia na siku hiyo, nitakuwepo karibu yako.
" Sasa tabia zako zinaanza kujidhihirisha .
Damian alimsogelea karibu na kumshika kwa nguvu wakawa wanaangaliana usoni.
" Niambie umetumwa?
" Na nani?
Damian alimtingisha mpaka Vanessa akajikuta anamkumbatia.
Mara Doreen alitoka chumbani na kuwakuta wamesogeleana karibu. Vanessa alitingisha mikono yake na kumkumbatia vizuri Damiani.
Damian alijikuta akamuachia.
" Wewe unafanya nini?
" Kwani hufurahii kupata joto langu?
" Hebu niachie basi.
Kabla hata Vanessa hajaniambia wakasikia makofi yanapigwa. Damiani alijitoa kwa nguvu na kuangalia kwenye hati akamuona Doreen anashuka kwenye gari huku akiwaangalia na kupiga makofi kama vile kuwapongeza.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY CRAZY HOUSE GIRL* *______________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-crazy-house-girl-______________________________________-sehemu-ya-kumi-na-moja

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest