Baada ya chakula cha usiku, Abby na Kamila walikaa sebuleni wajawa wanaangalia movies ya love story.
Kamila alikuwa amelala mapajani kwa Abby akili ya kamila haikuwa kwenye movie alikuwa akimuangalia Abby
“Baby... Kamila alimuita huku akishika kidevu cha Abby.
“Naam, niambie mama”
“Nahisi kama ndoto yangu imekuwa kweli. Mimi na wewe hapa… na hakuna mtu anaweza kututenganisha.”
Abby alimtazama kwa macho ya upendo, kisha akashika kiganja chake kwa nguvu.
“Naomba uamini maneno haya, Kamila… hakuna atakayeweza kututenganisha. Hata kama dunia nzima itasimama kinyume nasi, mimi na wewe tutapigana pamoja.
Wakati wanaongea Rehema alikuwa anapita karibu yao na kusikia maneno yao.
" Mmmh hivi Abby anajisahau kuwa alikuwa ni mlinzi wa getini. Muone pale alivyojiachia kama baba wa familia nae ipo siku atakuja kuachwa tu.
Rehema alienda chumbani kwake akachukua simu yake na kutuma messege sehemu kisha akaweka simu yake pembeni ya kitanda na kutaka kubadilisha nguo ili alale. Mara simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni kijo.
" Hallow.
" Kwahiyo kuna mpango gani unaendelea hapo ndani?
"Ni mapenzi mazito tu yani hawaachani wanafuatana kama kumbikumbi.
Kijo aliposikia hivyo alishusha pumzi.
" Hallow..
" Najisikia Rehema.
" Boss kijo pambana nafasi yako urudi nyumbani kwa mke wako.
" Niache kwanza nitajua nini cha kufanya mimi sio mtu wa kushindwa kirahisi.
Wakati wanaongea kumbe kijo alikuwa nje ya nyumba ya kamila kwenye kona yenye giza, alikuwa kasimama nje ya gari moja dogo Ndani yake alikaa mwanaume mmoja akivuta sigara.
Macho ya kijo yalilenga kwenye dirisha la chumba cha Abby na Kamila, wakati huo taa ilikuwa inawaka mara ghafla taa ilizima
“Kwa sasa unafurahia Abby,” aliongea kwa hasira
“Lakini nakuhakikishia, muda si mrefu nitakufundisha kuwa hakuna mtu anayeweza kunidhalilisha na kuninyang’anya kile kilichokuwa changu.”
Alizima sigara kisha akapanda kwenye gari, dereva aliwasha gari na kuondoka kwenye lile eneo.
Asubuhi ilipofika
Kamila aliingia jikoni akiwa na tabasamu huku akiimba alipika chai .
Abby alienda kimnya kimnya na kwenda kumkumbatia kwa nyuma na kumbusu shavuni na maeneo ya shingoni.
" Kwanini umeniacha Mwenyewe kitandani?
“Baby acha kwanza nitamwaga maziwa haya.
“Siwezi kuacha,” Abby alimnong’oneza karibu na sikio.
“Hata ukipika, bado wewe ni wangu, Unanipa amani ya ajabu.
Mara Rehema aliingia jikoni alipowaona wapo kwenye mahaba alinunua midomo na kutaka kutoka.
" Rehema hebu njoo iandae hiki kifungua kinywa.
" Sawa . Rehema alienda kuandaa mezani na wao wakaenda kukaa mezani na kuanza kupata kifungua kinywa.
" Mpenzi wangu leo nataka twende sehemu.
" Wapi tena mpenzi? Nilijua leo ni siku ya mimi na wewe kupumzika hapa nyumbani.
Abby alilidhika kiganja cha mkono cha kamila na kukibusu.
" Mpenzi naomba leo tubadilishe mazingira.
" Kwakuwa umetaka mpenzi mimi napata wapi nguvu za kukataa.
" Mwaaaa ndio maana nakupenda mke wangu.
Walimaliza kula kifungua kinywa kisha Abby akaandaa safari ndogo ya kumpeleka Kamila sehemu ya kupumzika.
Siku hiyo kamila alikaa pembeni na Abby alikuwa dereva maana alikuwa kashajifunza kuendesha gari.
“ mpenzi nataka nikufanyie surprise nyingine siku ya leo. Abby alisema akiwa anaendesha gari.
“Surprise tena? Hivi unataka kunizoesha kulia kwa furaha kila siku?” Kamila alijibu huku akicheka.
" Kwakuwa ni machozi ya furaha basi tia tu mpenzi.
Safari iliendelea kwa utulivu, upepo safi ukipuliza kupitia dirisha la gari. Kamila aliegemea kiti huku akimtazama Abby kwa macho ya mapenzi yasiyokuwa na kifani.
“Baby, unajua unanifanya nijione kama niko kwenye sinema ya mapenzi.” Kamila aliongea kwa sauti ya upole.
Abby alitabasamu bila kumuangalia moja kwa moja, akashika mkono wake uliokuwa kwenye mapaja yake.
“Naomba sinema hii ishi milele, mpenzi wangu. Na sasa nataka nikukumbushe kuwa wewe ni zawadi kubwa zaidi maishani mwangu.
Walipofika sehemu moja ya kupendeza kando ya ziwa, Abby alisimamisha gari. Kisha akamshika mkono Kamila, wakashuka na kutembea taratibu kuelekea ufukweni. Kulikuwa na mandhari ya kupendeza meza ndogo yenye maua mekundu na vinywaji kila kitu kilikuwa kimeandaliwa vizuri
“Abby! Umeandaa haya yote kwa ajili yangu?” Kamila aliweka mikono mdomoni kwa mshangao.
Abby alikuwa ameweka mikono yake mfukoni mwao suruali ,alicheka kisha akatoa mikono mfukoni na kisha akapiga goti moja chini. Moyo wa Kamila ulidunda kwa kasi huku akiwa anamuangalia Abby kwa mshangao
“Kamila sihitaji mwanamke yoyote kwenye hii dunia ninaemuhitaji ni wewe tu.
Je, utaniruhusu niitwe mume wako wa milele?” Abby alitoa pete ndogo ya dhahabu yenye kito cha kung’aa.
Kamila alishindwa kujizuia, machozi yakaanza kumtiririka.
“Ndiyo Abby… Ndiyo mara elfu! Nitakuwa mke wako wa milele.
Baada ya kamila kukubali Abby akimvalisha ile pete. Kisha akasimama
walikumbatiana kwa nguvu, wakiwa na furaha kubwa huku kamila akiwa haamini machozi ya furaha hayakuacha kutoka aliangalia pete yake kwenye mkono wake wa kushoto.
Lakini wakati huo huo, mbali kidogo, macho mawili ya hasira yalikuwa yakiwatazama. Kijo akafumba mikono yake kwa nguvu huku akisema kwa sauti ya chini:
“Hamtadumu Abby, umechukua kitu changu. Na nitahakikisha hiyo pete unayomvalisha leo ndiyo mwanzo wa uchungu wako mkubwa.”
Aliwasha gari lake na kuondoka kimya kimya, bila kamila wala Abby kugundua.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Maoni