Baada ya Abby kuzichoma moto zile picha, moyo wake ulijaa hasira Alijua kabisa Kijo hakuwa mtu wa mchezo, na kama ameanza huu mchezo basi hakika ataendelea.
“Sitakubali aharibu maisha yangu na Kamila. Mimi ndiye nitakuwa ngao yake,” Abby alijisemea huku akirudi ndani.
Alipofika chumbani alimkuta Kamila amejifunika shuka.
" Umekawia sana ulikuwa unafanya nini huko?
" Nilikuwa naweza sawa zile karatasi si unajua kesho natakiwa kuwahi kazini na kazi ya kuanza nayo ni ile kwenye zile karatasi.
" Kwanini wasingekutumia kwenye email yako?
" Sijui kwanini wameamua kutuma .
Alijibu Abby huku akibadilisha nguo na kuvaa Panama za kulalia kisha akapanda kitandani akajifunika shuka na kumkumbatia kamila.
Alimbusu kwenye paji la uso na kumwambia
' uwe na usiku mwema kipenzi.
" Nawe pia mpenzi.
Usiku huo huo
Rehema alikuwa chumbani kwake akitazama simu yake Ililia mara mbili, meseji ikaingia.
" Kuna nini nimetumia hapo ndani vipi limesha lipuka?
Rehema alisoma ujumbe kutoka kwa kijo akashituka.
" Huyu kichaa anataka kutuuwa wote humu ndani ni bomu gani akilotuma?
Akibinyeza simu yake akiwa anatafuta namba za kijo na kupiga . Simu iliita mara mbili ikapokelewa.
" Hallow.
" Wewe kijo kwahiyo hayo mabomu inayotumia unataka kuniuwa na mimi?
" Hahaha acha ujinga wewe, kuna kitu cha uchonganishi nimetumia hapo ndani vipi hatujasikia kelele za kugombana?
" Mmmmh hakuna kelele wala vilio watu huko ndani wamekumbatiana kwa mahaba yao.
" Basi kesho utanipa jibu.
" Kwani umefanya nini?
" Nimetumia picha kwa kamila , ni picha za Abby akiwa na mwanamke mwingine hotelini.
" Wewe kumbe huyu kaka ni malaya hivi, lakini nilijua tu ipo siku mmoja atakua kwenye haya mapenzi"
" Hapana Abby hana ujanja wa kuwa na mwanamke mwingine huo ni ujanja wangu tu wa kuunganisha picha.
" Umefanya je mpaka ikawa hivyo?
" Ni mambo ya utandawazi ,wewe bado mshamba unafungiwa hapo ndani ukiosha viombo huwezi kujua haya mambo. Kesho mapema utanipa majibu ya kazi yangu.
" Sawa.
Hatimae kulikucha mambo yakienda vizuri wazi walitoka pamoja wakaenda kazini na hata waliporudi walikuwa na amani .
Rehema alikuwa akiwafuatilia kila hatua lakini hakuona tofauti.
" Huyu kijobkasgindwa bomu lake halijalipuka.
Alienda kujibanza pembeni akampigia simu kijo.
" Huku mambo yako shwari yani mapenzi ni kama yameanza leo.
" Unasemaje wewe?
" Mpango wako umefeli baba jaribu tena badae.
Kijo alikaa kimnya kwa muda. Baada ya dakika mbili kupita aliita.
" Rehema...
"Mmmmh...
" Leo usiku ninaomba msaada wako, ukifanikiwa nitakufanya itoke kimaisha yani utaondoka hapo kwenye kivuli cha kamila na utang'aa na kuishi kama unavyotamani.
Rehema alitabasamu ta
“Hatimaye nafasi yangu imefika. Abby na Kamila, furaha yao haitadumu na mimi natafuta furaha yangu.
Kijo usijali kuhusu hilo nipo tayari kwa chochote.
Siku iliyofuata
Asubuhi Abby alimwambia Kamila:
“Mpenzi, leo nataka nikukutanishe na rafiki mmoja muhimu. Yeye ni mtu wa karibu ambaye anaweza kutusaidia kuhusu mipango ya ndoa.
Kamila alifurahia, akakubali bila hiyana. Walivaa vizuri na kuondoka pamoja.
Walipofika kwenye hoteli moja maarufu mjini, walipokelewa na jamaa mwenye suti nyeusi, sura yake ya heshima. Abby alimkumbatia.
“Kamila, huyu ndiye kaka yangu wa karibu, Robert.
Kamila alitabasamu na kumpa mkono wa heshima. Mazungumzo yao yalikuwa mazuri, yalijaa mipango mizuri kuhusu harusi, maisha mapya, na hata kuhusu biashara ndogo ndogo ambazo Abby alikuwa akipanga kuanzisha.
Lakini wakati huo huo, Kijo alikuwa ameketi meza ya mbali kabisa. Hakuwa na kazi ya kufanya kazi yake ilikuwa ni kuwafuatilia.
UsikuKamila alipoingia chumbani kwake, alikuta bahasha ndogo juu ya dressing table. Akafungua haraka. Ndani kulikuwa na karatasi yenye maneno machache lakini yenye sumu kali:
" Unaemuita mwanaume wako, Abby sio yule unaemfikiria. Kuna mambo mengi anakuficha, ukitaka kujua fuata muongozo utakaokuwa kesho.
Kamila alibaki ameduwaa, mikono ilitetemeka
“Mungu wangu hivi Abby ana siri gani nyingine anayonificha? Na hii bahasha imefika hapa ndani kwangu?
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Maoni