Abby alikaa kando ya Kamila, macho yake yaliangalia uso wake kwa muda mrefu, akimchunguza kwa upendo , kamila alionekana kuwa na hofu
βHivi umeshawahi kujiuliza hii bahasha imefika je hapa ndani? Na umepata jibu la swali lako?β aliuliza Abby, sauti yake upole .
" Nilijiuliza hilo swali lakini sikupata jibu kuwa imefikaje hapa ndani .
" Kama haijaleta wewe au mimi atakuwa kuleta nani?
" Sijui.
" Kama sio wewe itakuwa mimi na kama ni mimi itakuwa ina maana gani mimi kujichongea kwa mabaya?
Kamila alikaa kimnya kwa muda kisha akamuangalia Abby usoni.
" Unamaana atakuwa ni. Rehema ?
" Sijui , au anaweza kuwa kijo.
" Kijo anawezaje kuingia hapa ndani?
" Hapo ndio tujiulize hayo maswali.
Wote walikaa kimnya kwa muda wakitafakari.
" Labda cha kufanya ufuate hayo maelezo ili kujua hiyo siri ambayo mimi na kuficha.
Abby alinyanyuka na kutoka nje.
Alikuwa na hasira sana maana alijua kijo anamfanyia mchezo mchafu
Akiwa anaendelea kutafakari afanye nini Rehema alienda na kukaa karibu yake.
" Abby naona unaumiza kichwa kwasababu ya kusingiziwa mambo ambayo haijafanya hivi haijafikia kuwa kamila amekuchoka au amepata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi yako
Abby alimuangalia Rehema .
" Ulikuwa unafuatilia si ndio?
" Akuuuu....
" Kumbe umejuaje kama hatupo sawa?
" Dunia haina siri .
" Usitake niamini kuwa wewe ndie uliweka ile bahasha chumbani.
" Akaaaa.... Rehema aliruka fiti mia . Abby alimuangalia kwa macho yenye mashaka.
" Abby acha nikwambie kitu kimoja ambacho utakuja kunishukuru badae.
Abby alikaa kimnya akawa anamuangalia
" Najua sasa hivi mambo yako sio mabaya ,una kazi nzuri na unajiweza kwanini sasa ukae hapa iteseke na mapenzi wanawake tupo wengi tunaweza tunaondoka hapa na kwenda kuanzisha maisha yetu muache kamila ahangaike na maisha yake. Wanaume kama kijo ndio wanaume wa hadhi yake.
Kwa maelezo ya Rehema abby aligundua kitu.
Alinyanyuka taratibu na kuingia ndani.
Zilipizlta siku mbili kamila alipata picha ya abby akiwa na wanawake tofauti tofauti.
Siku hiyo kamila alikosa amani siku nzima alikuwa analia na kusema kuwa hana bahati ya mapenzi.
Abby alitlrudi kutoka kazini akamkuta kamila amelia saba mpaka macho yamevimba.
" Mpenzi mbona unalia hivyo kuna tatizo?
Kamila alimsukuma akanyanyuka na kwenda kuchukua zile picha na kumtupia.
" Angalia ushetsni wako unaoufanya .
Abby aliokota zile picha na kuziangalia kwa makini .
" Kamila unaamini huu mpango wa kijinga?
" Kwanini niliamini wakati huyo kwenye picha ni wewe?
Abby alijitetea sana lakini kamila hakutaka kumuelewa kabisa.
Nyumba ilikuwa chungu hakukuwa na maelewano hata kidogo.
Rehema alikuwa akimpa taarifa kijo . Kijo alifurahi na kujiona mshindi.
" Kijo hizo zote ni jitihada zangu naomba pesa yangu.
" Tulia mtoto wa kike mpango ukikamilika mbona unakuwa tajiri wewe.
" Sasa ile wako unidhirumu.
" Tulia Mapepe mtoto fanya kazi hiyo.
Baada ya siku kwenda na maelewano kuwa mabaya Abby aliamua kutaka kujua moja.
" Kamila huniamini sasa.
" Nikuamini vipi wakati una mambo ya kijinga, hujiheshimu, unashika pesa sasa unakuwa hayawani.
Maneno ya kamila yalimuumiza sana Abby ukizingatia alikuwa kipaombele kuhakikisha mpenzi wake anakuwa na furaha na kumpatia kila kitu alichokuwa anataka.
" Sawa nakubali shutuma zako zote ila kuna jambo moja nataka kujua. Mapenzi yako kwangu yapo au yameshakufa?
Kamila alinyamaza kimnya.
Abby aliongeza swali lingine.
" Upo tayari niendelee na maswala ya ndoa au niache?
Bado kamila alinyamaza.
" Kamila kimnya nacho ni jibu acha nichukue maamuzi , ila kumbuka sijawahi kukisaliti na mapenzi yangu kwako yalikuwa ya dhati. Nakupenda na nitaendelea kukupenda hata kama nitaanzisha maisha na mwanamke mwingine lakini wewe bado utabaki moyoni mwangu sitaacha kukumbuka.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments