Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

MY LUNA Simulizi za john 0789 824 178 1000 SEHEMU YA : 12

7th Aug, 2025 Views 71



Zayn alipoingia ofisini asubui ile ya Ijumaa, hakutarajia chochote kipya. Alikua na usingizi bado, kichwa kilimuwasha kwa hasira na mawazo ya Tatiana. Lakini mara tu alipofungua mlango wa ofisi yake, alikutana na sura ya mtu ambae hakutarajia kumuona pale kabisa๐Ÿ™…โ€โ™€๏ธ.

โ€œKevin?โ€ Zayn alipiga kelele akiwa haamini macho yake๐Ÿ—ฃ๏ธ

Kevin alisimama kwa tabasamu akasema, โ€œBro! Surprise!โ€๐Ÿฅณ

Zayn alimkumbatia Kevin kwa furaha mno maana ni mchizi kichizi wake toka enzi za primary๐Ÿซฐ
โ€œDamn! Wewe ulikuwa Seychelles, lini umerudi?โ€

โ€œJana usiku. Nilitaka nikufanyie suprise kidogo nikushtueโ€ Kevin alijibu huku akicheka๐Ÿคฃ.

Walikaa wote kwenye sofa, Kevin akiwa na shauku ya kujua mengi kuhusu mchizi wake
โ€œSasa niambie, mkeo yuko wapi? Leila, yule binti mzuri tuliyehudhuria harusi yake pale St. Maryโ€™s?โ€๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ

โ€œTafadhali usianze na huyo. Sina mpango naye kabisa. Napanga kumpa talaka muda si mrefuโ€ Zayn alikunja suraโ˜น๏ธ

Kevin alishtuka โ€œWait, what? Kwa nini?โ€๐Ÿ˜ณ

Zayn alitingisha kichwa, akavuta pumzi ndefu, โ€œHakuna mapenzi. Niliamua kumuoa kwa shinikizo la familia. Kiukweli moyo wangu ulikuwa na Tatianaโ€

Kevin alinyanyua nyusi, โ€œTatiana? Secretary wako?โ€๐Ÿคจ

โ€œYes. Lakini ananizingua. Amekuwa na mwanaume mwingine. Nimemtoa moyoni! Am done with herโ€Zayn alisema kwa mkazo๐Ÿ˜ก

Kevin alimtazama Zayn kwa jicho la kiuchunguzi, โ€œBro, you donโ€™t look okay. Hata uso wako umejaza stress. You need a break. Tonight, kuna sehemu nataka twende. Club ONE! Kuna madansa wa ukweli. Ni therapy yangu kila mwanzo wa weekend also nimesikia siku za weekend nipa moto kinyamaโ€

Zayn alicheka sana maana Kevin hupenda mno mambo ya club
โ€œUnasema therapy? We jamaa hujabadilika. Lakini poa, twende. Nahitaji kuondoa stressโ€

โ€œNice brooโ€ waliepana tano huku stori za hapa na pale zikiendelea. Ujio wa Kevin uliweza kumchangamsha Zayn mno.

Basi Usiku ulipofika, Kevin na Zayn waliingia kwenye gari aina ya Range Rover Sport, wakaenda hadi Club ONE.

Zayn alijua ni club ya kawaida, hakujali sana, alitaka tu kelele, pombe, na wasichana warembo. Lakini walipofika pale akagundua asilimia kubwa ya watu ni wanaume tena wenye pesa.

โ€œBroโ€ฆ asilimia kubwa ya watu ni wanaume! Hii ni gay bar au??โ€ Zayn alimuuliza Kevin kwa mshangao๐Ÿ˜ณ๐Ÿคฃ.

Kevin alicheka, โ€œHapana bwana! Ni club ya madansa wa kike. Madansa high classic bro! Hii club ni unique. Madansa huvaa masks na Nobody knows who is who! Nimesikia kuna huyo mmoja anaitwa Luna! Nimesikia yupo hot sana but hucheza kila jumamosi na jumapiliโ€๐Ÿ”ฅ

โ€œAah sio mambo yangu haya!โ€ Alisema Zayn๐Ÿ˜ค

โ€œI know! Ila najua uta enjoy just chill manโ€

โ€œOkayโ€

Wakalipia kiingilio cha laki mbili kila mmoja na kuingizwa VIP. Waliketi mbele kabisa, karibu na steji. Muziki ulikua mkubwa ukisindikizwa na disco lights za kutosha, inshort palikua pamechangamka sana.

Ilifika Saa mbili usiku, Boss wa club alikua akitetemeka vibaya mno

โ€œRuby hayupo! Ana homa kali. Hatacheza leo!โ€ ๐Ÿ˜ฐ

Binti mmoja mwingine aliesimama pembeni yake akamuuliza
โ€œSasa tutafanyaje Boss? Wateja wa leo ni wa maana mno?โ€

Boss hakujibu, alienda chumba cha kubadilisha nguo ndipo akakutana na Leila ambae alikua amekaa pembeni akipiga stori na Sinyati baada ya kumaliza mazoezi yao.

โ€œLeila, leo unacheza weweโ€ alisema Boss๐Ÿ—ฃ๏ธ

โ€œMimi?? But huwa nacheza jumamosi na Jumapili?โ€ Leila alishangaa๐Ÿ˜ณ

โ€œNajua, leo kuna emergency! Ruby anaumwa and kuna wateja wa maana mno siwezi wadisappoint hata kidogo!โ€

โ€œBoss lakiniโ€ฆโ€

โ€œNitakulipa vizuri! Jiandae haraka, vaa mask yako kapande stejini, tumeelewana??โ€

โ€œNdio Bossโ€ Leila hakua na namna na hakuweza kuendelea kumkatilia Boss wake kwa hofu ya kuonekana mkaidi.

Sinyati alimsaidia haraka haraka kujiandaa, akampaka make-up, akatengeneza wigi lake kisha Leila akamalizia kuvaa gauni lake na Heels akawa tayari. Mwishoni kabisa akavaa mask yake tayari kwa kazi๐Ÿ”ฅ

Basi Steji ikazimwa taa. Spotlight moja ikamulika katikati. DJ akapunguza sauti ya mziki, akachukua kipaza sauti kwaajili ya kumkaribisha Leila stejini

โ€œGuysss! Leo tuna suprise kwaajili yenu! So Give it up for โ€ฆ. LUNAAAAAAAAAAAโ€ ๐Ÿฅณ๐Ÿ—ฃ๏ธ

Weee watu walishangilia mno hasa Kevin maana walikua wanajua Luna hupanda siku ya jumamosi na jumapili tu! Ilikua suprise nzuri kwao๐Ÿฅณ

Haya Leila alipanda na kuanza mambo yake ya kuchezesha kiuno, kungโ€™ata lipsi na kujitikisa kidogo. Lakini ghafla macho yake yakatua kwa mtu aliyekaa VIP tena mbele kabisa. Si mwingine bali ni Zayn, mumewe๐Ÿ’.

Aliganda na kutoa macho akiwa haamini kile anachokiona. Alitaka kukimbia kwa uoga ila akakumbuka kitu, alivaa mask na sura yake haikua ikionekana.

โ€œHawezi kunitambua. No wayโ€ alijisemea kimoyomoyo na kuendelea kunengua bila uoga๐Ÿ’ƒ

Zayn yeye hakua hata na habari kuwa Luna ndie Leila, macho yake yalikua juu ya Luna akikitazama kiuno chake kilivyo enda, paja na jinsi alivyo tabasamu. Mwanaume akavutiwa na Luna, akahisi hisia ambazo hakuwai kuzipata popote pale hata kwa Tatiana๐Ÿ”ฅ.

โ€œDamn bro! Huyu ni bonge la dancer! Cheki kiuno! Flat tummy iko mahali pakeโ€ alisema Kevin na kumfanya Zayn atabasamu. Macho yake yalikua yameganda kwa Luna.

Hakujua kwa nini moyo wake ulianza kwenda mbio. Kuna hisia aliyokuwa anapata pindi akimtazama Luna! Ni wazi Zayn alichanganyikiwa na yule dansa pale stejini.

Je nini kitaendelea?
Nakujaโ€ฆโ€ฆ...
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY LUNA Simulizi za john 0789 824 178 1000 SEHEMU YA : 12  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-luna-simulizi-za-john-0789-824-178-1000-sehemu-ya-12
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest