Mwandishi; Kitty Fefe
Nilichanganyikiwa🤦🏼♀️🤦🏼♀️🤦🏼♀️nikaona hapa naiona dalili ya kushinda njaa😢😢😢 nilikuwa na hela kwenye simu nikatoka pale ndani na kusema nikanunue tu mkaa nije nipikie nisije washa gesi nikalipua nyumba ya watu😨😨😨🚶🏼♀️nikaenda nyumba ya pili na kwenda kuulizia wapi kuna wakala ili nikatoe hela ninunue mkaa😂😂🤸🏻♀️ nilielekezwa hapakuwa mbali,bahati nzuri nikafanikiwa kuona mahali wanauza mkaa,nikanunua chap na kurudi nyumbani, niulizeni jiko la kupikia nnalo?😂😂😂 Weee kumbe napo jiko hamna dah...! Mbona mkosi humu ndani,nilitafuta sana hata sioni kama wana dalili ya kuwa na jiko humo ndani😭😭😭bora tu ningenunua chips nikala wallah au nile huu mkaa😢😢😢nimpigie nani mimi anielekeze kuwasha gas jamani njaa itanimaliza
Mara nikaona Joel ananipigia nilishukuru ni heri nimwambie anielekeze lilipo jiko,nilipokea
"Hello shem samahani, nilikuwa nimepitiwa usingizi yaani sijasikia siku inaita"
"Sawa usijali, nilikuwa nataka nikuulizie mkaa na jiko napata wapi humu sivioni"🙄
"Mkaa? na jiko la nini?"
"La mkaa"
"Oooh mkaa upo stoo ya nje na imefungwa,hatujapikia siku nyingi sana mkaa na hata jiko lipo huko huko stoo....huwezi kuvipata labda bro angekuwepo akufungulie shem,kwani kwanini utumie la mkaa gas ipo....mimi nishazoea gas yaani jiko la mkaa nilishalisahau kitambo "
"Aaaah yaani nimeanza kupika bahati mbaya gas imeishia" niliongopa😂😂
"Oooh pole,lakini hawa watu watakuwa wameniibia gas nimejaza hivi karibuni tu,pole maskini shem ngoja nimpigie kuna jamaa ndio anatuleteaga nitamwambia na bro sasa hivi tu watakuletea uendelee kupika "
"Sawa nitashukuru sana" niliona tabu ipo palepale🥲😹😂inaletwa gas ingine yarrab mimi nitaishi nayo nyumba ikilipuka si basi jamani😔😔😔
Mara simu ikaanza kuita namba mpya sipendi ila nikapokea tu,
"Hello Kulthum,mimi ni Hakim hapa"
"Sawa niambie"
"Joel amenitafuta na kuniambia kuwa una tatizo hapo nyumbani kidogo,nishasolve kuna mtu atakuletea gas hapo sasa hivi.....pika tu cha kukutosha wewe usiku tutaagiza chakula,ila mbona hukunitafuta nilikupatia namba yangu?"
"Nilisahau nilivyokusave ndio maana nikamtafuta Joel"
"Okay,kuna kingine?"
''Hamna"
"Sawa,uwe na wakati mwema,baadae kidogo"
"Poa" akakata simu
Baada ya dakika kama kumi nikasikia kengele nikajua tu ndio gas imeletwa na wala sikukosea,alikuwa mdada ameleta gas......nikamuomba🙏 anielekeze jinsi ya kuwasha na kuzima,mana sikutaka kabisa kujipendekeza nielekezwe na Hakim, sikutaka ajue kumbe mimi ni azonto😹😹😹afu nna mpango wa kumfanyia visa sitaki kujishusha mapema hivyo🥱🥱🥱ila tatizo kwetu hatutumii haya mambo🙆🏻♀️🙆🏻♀️ningejulia wapi🤦🏼♀️🤦🏼♀️🤦🏼♀️yule dada akanielekeza kila kitu,nilimshukuru akaondoka nikaamua nichemshe ndizi fasta nile😨maana njaa niliyokuwa nayo jamani 😢
Mida ya saa kumi na mbili Hakim akawa amerudi,akanisalimia yaani nilimuitikia kiunyonge sana😔😔😔akaniuliza nini shida....!!!??
"Ujue mimi sijapenda kabisa kile alichofanya baba yangu na ingekuwa amri yangu natamani uniache"😢😢
"Kulthum i know,lakini nimekuhakikishia kuwa sijakubali ile ndoa aliyotufungisha baba yako kwa bahati mbaya,bali nimeiridhia sababu nakupenda❤️🔥❤️🔥❤️🔥sipo na wewe sababu baba yako kataka ila mimi pia nimependa,si mara kibao nilishakuambia hilo?"
"Sasa ndo umeongea nini....!? mimi nataka uniache buana, sikupendi wala nini kwanza wewe ni mkubwa mimi bado kadogo tu tena kila kitu changu ni kidogo"😹😹😹 yaani nilikuwa naona hatuendani kabisa mimi kadogo hivyo na pisi fupi halafu yeye giant mwili wa mazoezi🙌🙌🙌mtu kaenda hewani...mimi kama mdogo wake loooh ...! Siwezi😂😂😂
"Hahahah dah Kulthum una vituko mama,kwamba kila kitu chako ni kidogo?😹😹😹mimi siwezi kukuacha wallah🙌🙌🙌 nakupenda na nitakufundisha kunipenda pia na hutojutia kujuana nami "
"Hivi ukoje? Sikupendi hujui madhara ya kumpenda mtu asiyekupenda,huogopi hata mtu anaweza kukufanya kitu kibaya"😏😏😏
"Wala huwezi kufikia huko mama,pia nikuahidi kitu.....mimi sikuachi wallah wewe ndo yule wangu niliyepangiwa,by the way niliongea na mama akanambia kwakuwa Joel ameondoka hivyo tumlete mtu mwingine wa kuweza kukusaidia kazi hapa nyumbani maana hatujui Joel atachukua muda gani huko kwao mpaka kurudi au tuache?"
"Haina haja"😔
"Sawa itachukua muda gani ndio utakuwa sawa, nahitaji nikupatie majukumu rasmi ya hapa nyumbani na mambo mengine....!"
"Majukumu gani? Yaani ungejua jinsi gani unanikera mimi,sijui kwanini unajipa nafasi sana kwenye maisha yangu,hata huku usingekuja na mimi" nilinyanyuka na kumuacha nikaenda zangu chumbani kwangu
Yaani huyu kaka nisipomfanya kitu kibaya sijui,mimi simtaki bado ananing'ang'ania🥲🥲🥲nimfanye nini....!?🥲🥲🥲 yaani natamani kulia,akaja nigongea kwamba nijiandae tutoke kwa ajili ya kupata chakula cha usiku, nikamwambia nimeshiba mimi,akasema kama sitaki kutoka basi ngoja apike tule,sikumjibu kitu🥱🥱🥱alipomaliza kupika akaja nigongea tukale,nikamgomea🤣🤣🤣eti nimesusa kula🥱🥱🥱na sikutoka kwakweli🤸🏻♀️🤸🏻♀️🤸🏻♀️nikalala na kulala....nilikuja shtuka usiku wa saa saba,njaa inaniuma😱😱😱nikasema ngoja tu nikaangalie chakula jikoni buana kipaji cha kulala njaa sina🤸🏻♀️🚶🏼♀️nikikutwa huko nahangaika na masufuria ndio nitapoonekana sipo serious na mnuno wangu🤣🤣🤣🤣🙆🏻♀️
Nilienda na kukuta alipika tambi nikapakua nikachukua na soda nikaenda kula chumbani,nilipomaliza kula nikaona uvivu kuvitoa vikalala navyo huko huko🤪na saa kumi usiku tumbo la period likaanza kuniuma likisindikizwa na bonge la mvua lenye radi zake😢😢😢mpaka nikawa naogopa wallah😔😔😔tumbo linanyonga nahisi nakfa,ni.heri nimpigie Hakim aje😢😢😢au acha nfe tu,sitaki kumsikia😔😔😔
ITAENDELEA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
MALIPO 0715906120 Mtandao YAS JINA FLORA
Njo WhatsApp 0715906120.