Mwandishi; Kitty Fefe
Nilijitoa na kujifuta yale mateyake🙈🙈🙈 nilikuwa nasikia aibu sana🙈 nikasema hivi kwanini nimelegeza mapema hivi mpaka mtu ananipima lita😂😂😂sio mipango yangu kabisa😭😭😭
"Ebu niache huko,nani kakuruhusu kunilisha mimate yako...!?"😩
"I'm sorry.... But your so sweet like honey 🍯my honey"😘😘
"Toka bhana chumbani kwangu"😩😩😩
"Sawa natoka,ila ukiwa na shida ruksa kuniita"
Alitoka pale chumbani,nikabaki mwenyewe.....nikabaki kutabasamu kumbe r😜mance inakuwaga tamu hivyo😂😂😂👐👐👐sijawahi jamani hivyo niliona kama sijui nimepata kitu gani😁😁nilirudia kulala,lakini mama akanipigia simu m,nikajua tu anataka kuniuliza hali yangu
"Hello mama"
"Vipi kullu...!"
"Safi,shikamoo"
"Marahaba,za mida?"
"Nzuri mama"
"Unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri kwa sasa mama"
"Jambo jema hilo"
"Kweli mama,halafu umeongea nini na Hakim?"
"Anhaaa...! mambo tu ya kawaida"
"Yapi mama, umenisema tu najua"😩😩😩
"Wala,tulikuwa tunaongea ya kawaida tu"
"Niambie basi mama jamani"
"Alitaka kujua kuhusu wewe,maana ni kama umeanza kumsumbua huko"
"Hamna mama,mbona tunaishi vizuri tu...!"
"Kwani mimi sivijui visirani vyako? naomba ukae utulie huko,wewe sio mtoto mdogo na wanaume huwa hawapendi kabisa umletee upuuzi.....yaani hata iweje ndio umeshaolewa mimi sitaki unidhalilishe huko....nisisikie tena unasumbua,watu wanajua ushaolewa hivyo ukijirudisha huku utakuwa unajipa aibu mwenyewe"
"Mmmh...! haya mama"🥲
"Ndio hivyo sihitaji kusikia habari mbaya kuhusu wewe"
"Lakini mama unajua mimi ni kama mmeniforce je kama ningekuwa na mtu wangu angenichukuliaje mimi? na wewe mama hata hukunitetea,naolewa kama mmenisusa vile"😢
"Kulthum mimi sihitaji maneno mengi kutoka kwako,na siwezi kukutetea wakati baba ako anachukua maamuzi sikuwepo eneo la tukio na hata ningekuwepo ningefanya nini? wewe naomba tu usinidhalilishe mama yako huko"
"Sawa nimekuelewa mama " sikupenda kwakweli😢😢😢
Yaani mwanaume hana hata kaba kidogo tu kashasema🙄🙄🙌na nitamfanyia visa kiiukweli 😹😹🙌nilishuka kitandani miee nikatafute cha kupika nile, nilimkuta kakaa sitting room nikampita shwaa🚶🏼♀️🚶🏼♀️🥱na kuelekea jikoni nijipikie nile na nilikuta hata hakupika kitu nikawaza sana nipike nini cha haraka haraka🤦🏼♀️🤦🏼♀️🤦🏼♀️mara tena Hakim akaja
''Hivi kwanini unanifuata fuata kama unanyonya...!?"😔😔😔
"Cause unaumwa mamangu,hivyo sio mbaya nikakujali"
"Kwahiyo nikiwa siumwi hutonijali?"🤦🏼♀️
"Nope.....ni wewe tu unajikosesha nafasi hiyo"
"Umeongea nini na mama yangu?"
"Amenambia tu jinsi ya kuishi na wewe"
"Kwahiyo mimi nimeshindikana sana au? Mpaka uelekezwe jinsi ya kuishi na mimi"
"No, amenambia kuwa unapenda sana kununa na kubembelezwa,au kanidanganya?"
"Yaani mamangu amekosa kazi sana mpaka akwambie hivyo"
"Tuachane na hayo,naomba nikuulize kitu "
"Sawa uliza "
"Hujapenda nikuoe kwani?"
"Sasa hapo mbona umejibu tayari..!? Natamani tu uniache yaani nirudi kwetu"🙄😔
"Kwanini? Sababu ya msingi hasa ni nini I'm bad to you "
"Yes....! Halafu tumia kiswahili,hiko kingereza chako utanikosesha focus"🥱🥱🥱
"Hahaha hiki kichwa hapana😹😹😹🙌ila unajua nini Kulthum,yaani nazidi kukupenda na kutotamani kuwa mbali na wewe....the way you talk🥰🥰🥰yaani hizo nyodo na macho unavyoniangalia kwa dharau mimi nabaki kuenjoy tu🥰🥰😘nifanyie chochote mama kiwe kibaya au kizuri ila tu uwe namimi, nakupenda na ndio maana nilikuwa napenda mno kuja Tanga 🤗 amani yangu ilikuwa ni kukuona japo mara moja"
"Sijui hata unaongea nini yaani ndo unazidi kuniudhi😢😢😢mimi sikupendi jamani"😭😭😭mimi sichelewagi kulia nilijikuta tu yanashuka machozi😭😭😭
"Kulthum naomba tuongee kirafiki,very serious ule kwanza ndo tuongee,mimi sipendi kuona unakosa amani eti"
"Niambie tu "
"Ulikuwa na mpenzi wako ambaye pengine mlikuwa na mipango yenu ya mbele huko.mtambulishane kwa wazazi? "
"Hapana mimi sina mpenzi "
"Seriously....!?"
"Ndio"
"Basi naomba nikuambie kitu kimoja,kuna aina nyingi za mahusiano au namna watu walivyoanza mahusiano,kuna ambayo watu waliridhiana kuna mengine ya kuingia bila kutarajia au kulazimishwa.....lakini mwisho wa siku matokeo ndio yana matter sana ....kama wewe ambavyo unahisi shida sana kuwa na mimi,but nakuomba tu fungua moyo wako❤️🔥❤️🔥❤️🔥 hutojutia kuwa namimi,nitakuhandle mpaka ujilaumu why ulichelewa kunijua .....naomba niwe mtu wa kwanza kupendwa na wewe😘😘😘na wa mwisho"😘😘😘
"Ungoje basi hadi nikiamua"😔😔😔
"Sawa mimi wala usijali nitakungoja unipende kwa wakati wako sahihi.... anyway unapenda kula nini nikusaidie maana sijaenda kazini ya kukuangalia wewe hivyo sio vema uangaike"
"Mimi nitapika tu mwenyewe "
"Usiwe mkorofi basi mama,nikupikie nini?"
"Wali samaki"
Nilimuacha pale apike nami nikaenda nje, nikakuta mlinzi ameshakuja(kama nilivyowaambia anakujaga jioni asubuhi anaondoka) siku hiyo aliwahi kweli ilikuwa saa kumi jioni.....nikapiga nae stori sana....mpaka nilivyoona huu muda itakuwa huko mtu kashaivisha ndio nikaenda 🤸🏻♀️🚶🏼♀️kupata msosi kisha nikaoga na kutulizana sasa.hapo najiuliza mawili nimpende nsimpende😹😹😹 😹🤸🏻♀️🤸🏻♀️🤸🏻♀️🤸🏻♀️ ebu tukubaliane ndugu zangu huyu shemu wenu tumpente au tusimpenteee..!?🤣🤣
Saa tatu usiku tumbo likaanza tena kuniuma😢😢😢nashindwa kulala kabisa,basi bhana Hakim akanambia inabidi tulale ote maana naweza kupata dharura ya kuumwa sana🤦🏼♀️🤦🏼♀️Mmmh kulala ote tena....!!!? si kila mtu ana chumba chake lakini😹😹😹😹😹😹lakini hawezi nifanya kitu,ila alale kwenye sofa kwakweli labda...!!!
ITAENDELEAAA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.