Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️ Mwisho s1 16 To 20

23rd Aug, 2025 Views 58


𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄
::::

SEHEMU YA 16

Trisha Aliweka Vitu chini Haraka Haraka akatoka Nje Kufata Njia Aliyoambiwa Kapita
Alex
Alitembea Mpaka Mwisho wa Mtaa wao lakini Hakumuona
Akarudi Nyumbani Kwao
"Nimefurahi Tu kukuona Trisha Upo mzima lakini Hutakiwi Kutembea tembea Bado sio salama Sana kwako"
Alex alikua Yupo Sehem Anamtazama Vizuri Trisha Mpaka Alipo Rudi Kwao
Aliinuka Na Kuondoka Eneo lile Kurudi kwenye Makazi Yake

"Yule Jamaa Ni nani Na Kwanini Yupo Karibu sana Na Trisha Natakiwa Kumjua Zaidi Ni Muhimu hilo"
Alex alikua Kalala Fikra zake Ni KWA Trisha Hakua Anawaza Chochote Tena Tofauti na kumlinda Trisha Alimkumbuka mama Yake Na Maneno yake
"Sorry mom"
Alex alisema akiwa anapapasa Shingo yake Ili Kushika Kidani Chake Chenye Pete

Alishikwa Na Mshangao Baada Ya Kukuta Shingo yake Ni Tupu
Aliinuka Haraka Huku Kachanganyikiwa
Alianza Kutàfuta Kwenye Nguo zake Zote lakni Kidani Hakikuwepo kabisa
Alex alizidi Kupata Mshtuko
"Au paleee"
Alex alikumbuka Siku ya Tukio Alipo pigwa risasi

Haraka Alichukua Nguo Kuvaa na Kutoka Haraka Sana Kwenda Pale Garage mitaa ya Trisha.

Alex Alifika Pale Usiku Huo Pakiwa Kimya Akaanza Kutafuta Kila Eneo Ni Wazi Kuwa kama Ilikua Pale basii Ilishaokotwa Mana zimekua Siku Nyingi zimepita Tangu Tukio lile na Trisha Ni mtu ambae Huja Pale mara KWA Mara Nyakat za Usiku Pakiwa Kimya akiamini atamuona Mtu anaehisi Kumpenda Sana mtu aliegusa Nafsi Yake

"Unatafuta Hii"
Alex Alisikia Mtu Alimuuliza Nyuma Yake
Aliitambua Vizuri sana ile sauti lakini Hakutaka Kugeuka

"Kwanini Uliahidi Uongo Sàsa Kama Ulikua Hutaki Kwanini Ulinambia Utarudi Kwangu Tena Kwanini Si Ungeenda Jumla sasa"
Alex Alisikia Mtu Nyuma Yake Akiongea Huku Analia

Alianza Kutembea Kufata Piki Piki yake Ili aondoke Maeneo Hayo Hakutaka Mtu huyo amuone
************

Trisha Usiku Usingiz haukuwepo kabisa
Alikumbuka Siku Ya Tukio Baada Ya kaka Jambazi Kuondoka Eneo lile alijiona Mikononi ana Kitu kama Cheni Baada Ya kurudishwa Nyumbn na Aizack Alitunza Ile Cheni Yenye Pete
Aliinuka mpaka Alipo Itunza Na Kuichukua
Alikua Na Ham Kubwa Sana Ya Kutaka Kumuona Huyo mtu
Sàsa Kwenye Mikono yake Kulikua Na Cheni na leso
Aliinuka Taratibuu Akatoka Nje Na Moja KWA Moja Alielekea Garage

Na KWA Macho yake anamuona Mtu Ameshika Tochi anatafuta Tafuta Kama Kuna Kitu amepoteza Kutokana Na Mavazi ya Mtu Huyo kufanana na ya Mtu Ambae anamtafuta sana aliamini ndie yule yule Jambazi kama Watu wote wanavyo muita

Sàsa Trisha na Alex ana KWA ana

ITAENDELEA.....
NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️
❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️
MUTUNZI 𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄


SEHEMU YA 17

Trisha Hakuamin Yule mtu Aliekua akimsubri siku zote Leo Yupo mbele Yake
Wakati Alex Hakua Tayari Trisha Amjue
Trisha aliongea huku akisogea Alipo Alex Machozi yalikua Yakimtoka tu
ALEX alianza Kutembea Kufata piki piki yake KWA Tafadhali Ili Trisha asije Kumjua
Trishaa Aliona Hilo akasimama
"Kwahy Unataka kunikimbia Tenaa na Leo 😢We nani Ambae Hutaki mi nikujue Kwanini Unakuja mgongoni kwangu Tu"
Trisha alianza kulia Tena
Wakati Alex kasimama anatafakari Maneno Ya Trisha
Gafla Alihisi Kukumbatiwa Kwa nguvu nyuma Yake
Ni Wakati Trisha alipona Mtu wake kasimama yeye alitumia nafasi Hiyo Haraka Alikimbia KWA kasi na kunkumbatia Alex kwa nyuma
Alex Hakuweza Kuvumilia Labda Nae Ndo Kitu pekee Alichokua anahitaji KWA Wakati Huo
Aligeuka na Kumkumbatia Trisha
Wawili Hao walikumbatiana KWA Zaidi ya Dakk 5 Trisha akiwa Analia
"Kwanini Sasa Ulienda Jumla ,, Huku nipa Hata Taarifa Unaendleaje Uliumia KWA Ajili yangu hukusubiri Hata Niseme Asantee Haukurudi Hata Kuangalia Mi nipo Vipi Kwanini Sasaa"
Trisha aliongea Bila Kutoa Hata Nafasi ya Kujibiwa huku Akilia

Alex Alitabasam Tabasam Lenye Uhai Na kufanya Sura yake Nzuri iongezeke Mvuto mara Dufu Mashavu yake Yaliyobonyea Kwa Mbalii yaliongeza muonekano Katika sura yake
Laiti kama ingekua mchana na ukafanikiwa kumuona Hauta Tamani Kutoa Macho yako KWA Alex
Sasa alikua kwenye Mikono ya Trisha Bila Hata Kutumia nguvu Nyingi Moyo wake Ulidunda KWA jina La Trishaa Bint ambae Hajui Chochote Kumuhusu Alimjua vizur baada ya kupewa deal Kumuua Kama Shahidi Dhidi yake
Deal Inazaa Mapenzi Ambayo Hajui Yametoka Wapi Mpaka sasa

"Ni kweli Ulikua na Wasi Wasi Kuhusu mimi Trisha"
Alex Alimuuliza Trisha kwa Sauti Nzito tam Iliyozama Kwenye Moyo wa Huba

Trisha ni kama Alishtuliwa kwenye Hiyo Ndoto Haraka Alijitoa Kwenye Kifua cha Alex
Alex nae Mawazo ya Kujificha Ili Trisha asimjue Alisahau Akajiachia
Trisha Kumuangalia Mtu wake Usoni

Macho yalimtoka
"Weweee"😳

Aliongea Huku akirudi nyuma Mtu aliekua Mbele Yale Huenda sie Aliekua Akimkusudia
Alex Nae Ndo akashtuka Kuwa Trisha Anamjua ki Vingine
Haraka Akamsogelea Lakni Trisha alimpiga Stop
"Simamaaa!!!"

"Trisha Nisikilize Nitakwambia KILA kitu Tafadhali Usiondoke Kama Hvyo"
Alex alimtuliza Trisha Bila Mafanikio
"Nimesema usinisogelee Mtu ninaemsubir Sio Wewe Samahani Imetokea tu Kutokuelewana"

Trisha aliongea Huku akigeuka Kuondoka Eneo Lile

"Noo Trishaa It's Me please"

Alex Alikimbia Na kumshika Trisha KWA Nyuma
"Trisha ni mimi ni Mimi Trisha Huyo Unaemsubiri Ni Mimi Nitazame Tafadhali Trisha Sikujua kama Niwewe Nilie Kupa Leso Ile Siku Trisha wala Sikujua Kama ni wewe TulieKutana Siku ile Usiku Mbezi Wakati Nimeacha Piki Piki Eneo Lile Trisha Mpaka Nilipo Kuona na Kitambaa Changu Kule Mwisho wa Mji ile Siku Sikukuacha KWA Kupenda Trisha Nilishtuka Baada ya Kuona Kitambaa Muhimu Sana Kwenye Maisha Yañgu Unacho Wewe Na unakijali Sana Nilishindwa kuja Mapema Niliogopa hili Kutokea Tafadhali Trishaa Usiondoke Hvyoo"

Maneno Ya Alex yalimuingia Sana Trisha Alijigeuza Taratibuu Kwenye Mikono ya Alex Iliyoshikilia kiuno Chake vyema kabisa Alimtazama Usoni Alex
Kisha Akamfunua Shati kwenye Bega Mahari Alipo pigwa Risasi
Alex Alivua Kabisa Shati
"Unataka Kuona Hii "
Alex alimuonesha Jeraha Trisha Ambalo Halikua limepona Kidonda Kilikua Kibichi Kabisa Tofaut na alivyozani Mda Ulikua Umepita Sana kingekua kimeanza hata Kupona kama Sio Kupona kabisa

TRISHA hakujibu Gafla bila Kuelewa Alijikuta Ametua midomo yake kwenye midomo Ya Alex 😘

Kitu Ambacho Alex Hakuwah Kukifanya Kwenye Maisha yake Yote Trisha Bila Hodi Akaanza Kuiba mate Ya mwenzie🙈 Alex Mwili wake Ulipigwa ganzi Bila Taarifa Kwa Sec5

ITAENDELEA.....
NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️
𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄
::

SEHEMU YA 18

Alex Alijikuta Anaonesha Ushilikiano Kwa Trisha 🥰 Kazi yao Kubwa Ilikua Kubadilishana Juice asilia ya Mungu iliyotiwa Kwenye midomo yao
"I really Love You Trishaa"
Alex Aliongea Huku akimtazama Usoni
Walitazaman KwaDakk Nzimaa Japo Giza Lakin macho yao Yalionana vyema

Usiku Huu Ulikua Ni Usiku Mkubwa Sana Kwao Ulikua Usiku Wa Historia maishani mwao Ni Usiku Ambao waliusubiri KWA Miaka Mingi kabla ya Kukutana Kwao

"Hata Siamin bado Kama Ni wewe Wa Mchana Nawew huyo huyo wa Usiku Nakupenda Sana Mr Handsome"

Trisha Alitoa yake Ya Moyoni KWA Napama Stini Akiwa Yupo kwenye Miguu Ya Alex Aliekaa Chini kwenye Majani Mafupi hata Hawakujali pachafu au Pa Safi
"Naitwa Alex Niite Alex "
Alex Alimtambulisha Jina Lake Halisi Trisha
"Wooh Jina Zuri Kama Wewe Ulivyo ILa Wewe Umezidi U_handsome Siwezi Vunjwa Kiuno Kweli Na Wapenz Wako "
Alex Alikua akicheka Cheka tu Ukizingatia Ni Mgeni Kabisa Kwenye Mapenz,,,
Ye Na Mapenzi Wapi na wapi
Sàsa moyo wake KWA Mara Ya Kwanza umeanguka KWA Trisha bint mbichi Na Mwenye Urembo wa asiri Asie na Mengi

"Mpenzi wangu Trisha najua Hawezi Kujivunja Miguu 😘"

Alex Alimbusu Trisha kumtuliza Mtoto Aache Wenge Yupo Peke yake

"Mbona Hujaniuliza chochote Kuhusu Usiku Ule Kwanini Unaniamini Trisha"

"Noo! Bby nimapema Sana Kwanini Tusiongelee Mapenz yetu Haya Ndo Tumeyaanza Leo Alafu Tuanze Kuongea habar za Watu Wengine We Kwanini uliniamin Unajua wazi KILA Mtu ananitafuta Mimi Ili Kukupata wewe na Wewe ulinisaidia Mpaka Hapo sitakiwi Kukuamin"

"Lakini T mimi Ni muua.....😘
Kabla Hajafikisha neno Lake Alex
Trisha alimpa Busu la Mdomo Kuashilia Anyamaze

"Kwao wewe Ni JAMBAZI Lakin Kwangu Wewe Ni Gentleman Kwasasa Sitaki Kuharibu Furaha Yangu Plzz Alex najua Kuna story Nyuma Lakn Niahidi Kama Kweli Umefanya basi Hauta Fanya nitatembea nawewe kwenye Vipindi Vyote Hata Kama kwenye Tanuri la Moto Nitavua Viatu tupite Wote Nakupenda Sana Alex"

Alex Hakuweza hata Kujibu Akimkumbatia Trisha Huku Machozi yanamtoka
"I Found That Women Mama (mama Nimempata Yule Mwanamke) Alex Aliongea Mwenyew Kiasi Mpk Trisha Alisikia
"Ukoo sàwa Alex "
"Naomba Unisamehe sana Tumekutana Vibaya"
"Hapana Alex Ilikua Lazima iwe Hivi Alafu Tukutane Kipenz "

Walikuja Kushtuka Waadhini wa Alfajr wanaita Walio amin Waenda kumshukuru Mungu Wao
"Mungu Wangu Mbona Leo Pamewah Sana Kukucha"
Trisha Alishangaa hata Hajatosheka Kukaa na Mpenzi wake Mpya Mda Umeisha
"Trisha Baby Naomba Tuondoke Nitarudi Tena Kuwa Makini Sitaki Kukuona na yule Mtu Jamaa Simpendi Na Simjui ni nani Ila Sitaki Kukuona ukiwa karibu nae "

Alex Alimchimba mkwara Trisha Kuhusu Aizack
"Tuna Mengi sana ya Kuongea Trisha Nitunzie Siri Yangu "

"Siri Yako ni siri Yangu Alex Wewe ni mimi Kwasasa Nakupenda"

Hatimae Watu walianza Kupita pita Maeneo yale Si Trisha wala Alex Hakuna Hata Mmoja Alitaman Kumuacha Mwenzie

Walibaki wanaagana Na kuagana Alex alinkumbatia wakakumbatiana Watu Walio Kuwa Wachache wanapita Maeneo Hayo walibak Kuwatazama Tu
"Mpenzi Wangu Nataman Kubaki Hapa lakini wacha Niende Nikaweka mazingira sàwa Nitakuja "

"Usiende Jumla Tafadhar sina Pa Kukupata mie Nipe Hata Namba Ya Simu basii "

Alex Alitoa Namba Ambayo anatumia Na boss Wake Alex hakua Na Simu KWA Sababu hakua Na Mtu wa Kuwasiliana Nae
Simu yake Ilikua Moja Ya kazi Na ina_namba Moja tu 8 ya muajiri Wake

Sàsa Inaingiza namba ya pili ambao ni Trishaa wake

Kishingo Upande sanaaa waliagana mana pamesha Kucha

Trisha Alifika nyumbn Akiwa anacheka Cheka Tu alikua Ni mtu Mwenye mood Nzuri Ambayo Pengine Hajawah Kukutana Nayo kwenye MAISHA Yake
"TRISHAAA"
Alipo Karibia Maeneo ya Kwao Alipokelewa na Sauti Kali ya Ray

Alikuja Aizack Haraka Akamkimbilia
"Vipi Upo salama Trishaa Ulikua wapi"
Aliongea Aizack akionesha mtu Mwenye wasiwasi sanaaa
"We nae asubuhi asubuhi Hivi Vipi Nyumbani mwa Watu"
Trishaa alimuuliza Aizack Badala ya Kujibu

"Yaan Wewe niwaajabu kweli Mtu Tumemsumbua KWA ajiliyako Afu Hujali wala Nini Unajua Tumeanza Kukutafuta sangp?"
Da T alimkalipia Trisha
Trisha Alisogea Mpaka Alipo Dada yake Akamshika Mikono KWA Upole Kabisa
"Nisamehe dada Nilitaman tu Kutoka Niwe Sehem Kutuliza Akili Naomba Mnisahe sana Sàsa Hivi nipo Vizuriiiii Kuanzia Leo Nitakua Happy Nimeamua Kuacha KILA kitu Sàsa"

Trisha Alidanganya Hakutaka Wajue Kwanza Nini anafanya na amefanya
"Aizack asantee kwa Kujali "
Alimgeukia Aizack
Wakaingia Ndani Kikao Hicho cha Dharula kilifanyiwa Nje ya Geti lao

Alex Hakuenda Nyumbani Baada ya Kuaga Na Trisha
Alihakikisha Trisha Anafika kwao kwanza bila Trisha Kujua KILA kilichoendelea Pale Alikishuhudia Lakini Hakusika Maneno
"Huyu Jamaa ni nani? Kuna Haja Ya Kufatilia Taarifa zake "
Alex Aliongea Mwenyew na Baada Ya Kuona wameingia Ndani Alianza Kuondoka
(Umefika Sweetie)
Msg iliingia Kwenye Simu Yake Akiwa Bado Yupo Maeneo Hayo ya Kina Trisha
Jina Lililotuma Msg Hiyo Limeseviwa My Queen❤️

Alisimaisha Pikipiki na Kutulia Amjibu Bibie
(Ndio Queen Vipi Wewe Umefika Salama )
(Yeah Nmekuta Wananitafuta tu)

(Na Jamaa Yako Yule Yupo nae)
Alex Alituma Akimaanisha Aizack
(Nimemkuta ndio Lakini Usijali Kipenz Changu Nitakaa nae Mbali Alex Nimekumisi sana my love Fanya Uje Tena nikuone)

Alex Aliachia Tabasam 😍
(Toka Nje my Queen Utanikuta)

Trishaa Alitoka Haraka Kwenda nje asiamini kama Kweli
KWA Mbalii Alimuona Alex Yupo Akiwa Anamtazama
Alianza Kukimbia kumfata Alipo

Simu ya Alex iliita Kabla Trisha hajamfikia
Namba Ilikua mpya Kabisa
"Usifanye Ujinga wowote Huyo bint Anafatiliwa na Police Haraka ondoka Hapo Ninakuona Na Nitampga Shaba Huyo Bint "
Alex aliishiwa Nguvu Penzi ndo KWanza lina Siku Moja Tena masaa

Alipiga Hesabu za Haraka Haraka

Trisha Alishuhudia Piki Piki Ikiondoka kwa Kasi Sanaaa Eneo Lile Alex Anapotea Kabisa Kwenye macho Yake

ITAENDELEA.....
NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️
𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄
::

SEHEMU YA 19

TRISHA Alishuhudia Alex Akipotea kwenye macho yake Hakujua Kwanini Alibaki Kuipiga Simu ya Alex Iliita Bila Kupokelewa Hakuelewa ILa Moyo wake Ulihisi Hatari kwa Jinsi alivyoondoka pale
Alikaa Chini Kabisa Kama Mtu asieelewa Afanye Nini
Akiwa Pale Chini Alisikia Mlio wa Pikipiki Ukija KWA Kasi Sanaaa
"Alex"
Aliinuka Haraka huku akitaja Jina La Alex AnajuaUendeshaji Pikipiki wa Alex kama Kichaa Akabidhiwe Rungu Ndivyo Alex Akikabidhiwa Piki Piki Mwendo wake Wa Hatar hatar Mda Wote
Trishaa Aliinuka Kuangalia Hakuamin Alex Yupo mbele yake

Alex Aliona Kuliko Kukimbia Tatizo Bora asimame Kupambania Mapenz yake Kwa Trishaa Alipiga Break ya Gafla Sana Hata waliokaribu yake walimlaani Sanaa na Kurudi kwa Trishaa wake

Alifika Na Kumkumbatia🥰🥰

Wakati Yote hayo yakiendelea Kuna Watu Walio Kuwa wakifatilia kwa ukaribu sana Wapendanao Hao wapya Mjini

Aizack baada ya Kuona Trisha Yupo bize sana na Simu Alijitahidi Sanaa Kuona Anachati na nani Aliona Jina Limeseviwa My King❤️
Na alivyotoka Haraka Haraka Aizack alimfatilia Nyuma Kujua anaonana na Nani

Muddy Wakati Huo Alikua Anaenda KWA kina Trisha Kabla Hajafika alimshuhudia Trisha akitoka Mbio kuelekea Nje ya Nyumba Yao Alisimama Kuangalia anaenda Wapi ?

Kulikua na Mtu mwingine kabisa Huyu mtu Ndie aliempgia Simu Alex akumpa Onyo Yeye aliwashuhudia Wote wanaomfatilia Trisha na Huyu mtu Alitumwa na boss wa Alex Kufatilia nyendo Zote. Za Alex Hata ile Kukesha Alex na Trisha Alikua amekesha nao pia

Alex na Trisha wao Hawakujali Walioneshana Upendo wao wa agape mbele Za Watu Kabisa
"New Day Has Coming My Love(Siku mpya Inakuja Mpenzi wangu) "
Alex Alimwambia Trisha
"Umeniacha Dkk2 Tu nishaboleka Twende Wote"
Trisha aliongea Huku akijiweka Vizur Kifuani kwa Alex
"Mimi ndege wako manati Ya Nini"
Alijibu akimpa Busu

Alex alimrudisha Trisha mpk nyumbani kwao Ray Alishangaa sanaaa Trisha na mr handsome Imekuaje tenaa
"Shoga we Ugemsubiri Tu huyo kileso chako Huyu mr Handsome Ungeniachia Mie "😃 Ray Uvumilivu Ulimshinda akaropoka KILA Mtu alicheka
Wote walifurahia Ujio wa Alex Lakin Aizack Alichukizwa Sanaa na Ujio wa Alex pale Laiti angejua Huyu Ndo Hasimu wake Mtu ambae Anamtafuta KWA Miaka Zaidi ya Miwili Basi kazi yake Ingekilikua Rahisi Sanaa

"DaT mi Nampenda Sana Trisha Nipe Tu baraka Zake niondoke nae Kabisa"
Alex Alimwambia Dada ake Trisha
"Ndo wanaoaga Hvyo Huyu Haendi Popote mpaka Ndoa "
Alijibiwa Alex na Kufanya Wote wacheke
Alex Alishinda kwao Trisha Siku Hiyo

Jioni Alex Aliondoa mpaka Sehem ambayo Ameweka Makazi
Ni Jengo Moja Kubwa na la Kifahari Ni Hotel ya Wageni wenye Hadhi inayomilikiwa na Bwana Makregani
Katika Chumba Kimoja Kilicho Ghorofa ya 8 ndio Alimuhifadhi Alex KWA Miaka Zaidi ya minne Tangu Alipo Mkomboa Kutoka Blazil

Alex Siku Hii Alirudi Akiwa Sio muuwaji Tenaa Alirudi kama kondoo alepotea KWA Mchunga wake Nasasa amelipata Zizi lake
Hakuitaji Kazi Wala pesa
Akili Yake Iliwaza ni Vipi atamlinda Trisha Na Atatoka Vipi kwenye mikono ya Boss wake
Kitendo alichokifanya Alijua wazi Kuwa Makregani Hawezi kukubali Kumuacha Akiwa Hai
Alitoa picha ya Mama yake huyo Pekee Ndie aliekua Rafiki yake Huongea na Picha Ya Mama yake Kipindi Chote Akiwa na Huzuni

Leo Ilikua Tofaut KWA Miaka Yote Aliyowah Kuishi Duniani
"I found a women mom Stronger than anyone I know She Shares My Dream,😰 mom I found a Love To carry More Than just my Secret 😓To carry love To carry Children of our own,,I found Girl Beautiful and Sweet (Mama Nimepata mwanamke Shupavu Kuliko yeyote niliewahi Kumjua nitashea Nae Ndoto zangu Mama Nimepata mpenzi ambae Atabeba Siri Zangu ,Atabeba Upendo wangu ,Atabeba watoto wetu Nimepata Mschana Mzuri Sana )" Machozi tu yalilowesha Picha Aliona mtihani Mzito Na Hatari Iliyo mbele Yao Dhidi ya Penzi lake

Alex Aliongea na Mama yake KWA Lugha yao Aliamin mama yake Hajui kiswahili Hivyo huwa hapendi kukitumia sana anapo Ongea na Mama yake

"Well👏🏻👏🏻 Well👏🏻Well👏🏻"
Akiwa Kwenye dimbwi zito la Mawazo Alisikia akipigiwa makofi Nyuma na kusifiwa Baada ya kugeuka Alimuona Bwana Makregani Akiwa Tayari ndani Ya Chumba chake

"Mtihani wa mapenz Hakuna Aliewah kufuzu lakini Wewe Umekua zuzu Kupenda Sehemu Ambayo Hutakiwi Kupenda Kabisa Unajua yule Mschana ni Hatari Kiasi Gani Kwenye maisha yetu UnajiangaliaWewe Sio Unajua Kwasasa nipo kwenye Hatari Kiasi Gani?"
Makregani aliongea huku akimtupia Picha Alex
Picha Hizo Zilikua Za tukio Ambalo amelifanya Alex na Trisha Kuanzia Usiku Ule Mpaka alipo rudi na Piki Piki Picha Zote zilikuwepo

Alex mapokeo Yalikua Tofaut ya Picha hizoKwanza alifurah Sana kuziona Zile picha
Na vile Alijua hata Picha ya Trisha Tofauti na ile aliyopewa na Muddy ikitambulisha sura ya Trisha anaetakiwa Kuondoka Uhai wake

Alifurah sana Kuona Zile Picha Ambazo Wamepigwa Yeye pamoja na Trisha

"Sasa Hivi umekua Unajiachia Unatoka Unavyojisikia Wewe Umesahau kama sura yako kuna Watu wanaijua Vipi Taarifa Zikifika Upo hai Unaniweka Wapi Mimi "

Alex Aliinuka Akamsogelea Boss wake
"Kama ,Kama Ukimgusa Trisha Hata Kwa Kumtazama Na jicho Baya Nakwambiaa NITAKUUA"
Alex aliongea huku akimpiga Piga Kifuani Makregani KWA ujasiri na Sura ngumu
Bwana Makregani Hakuamin masikio Yake
"ALEX"
"YES It's"
"Okay nitamuacha Huyo mwanamke Fine Hakikisha Unamnyamazisha Macho yangu Wakati wote yatakua Kwake "
Bwana Makregani aliongea huku Akiondoka Eneo Lile Na Kumuacha Alex Pekee

Itaendelea....
NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️
𝑩𝒖𝒓𝒖𝒅𝒂𝒏 𝑺𝒊𝒎𝒖𝒍𝒊𝒛𝒊
🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄🔄


SEHEM YA 20

Alex alianza Kumusanya Picha Zile Akiwa na Trisha Na uso wake Ulikua wa Kutabasam Wakati Wote
"I Hope That Someday I'll share Her Home (Natumain Kuna Siku Moja Nitakaa Nitaishi Nae)"
Aliongea Huku akiitazama Picha Iliyoonesha anambusu Trisha

***********

Alex alifanya maamuzi ya kuhama Katika hoteli Ile Alitafuta Nyumba Nzima Maeneo ya Mwenge Akapanga Pesa Alikua Nayo ya Kutosha Kabisa
"Wooh Hapa ndo Nyumbn kwako Sweetie"
"Kwako Wewe Ndo mama Mwenyew Sàsa Malkia Wangu"
Alex Alimfata Trisha kwao na Kumpeleka Makazi Yake aliyoamua Kupanga

"Nataka Kusikia Kila kitu Kuhusu Wewe baby "
Trishaa Alimwambia Alex KWA Sauti ya Kudeka Huku Akiwa analala Kifuani Mwake

Alex Alimuelezea Trisha Maisha yake Tangu Akiwa Mdogo anajielewa Mpka Yale alihadisiwa na Mama yake Wakati Anazaliwa

Wakati Wote Trisha Alikua Akilia Tu KWA Huzuni alimuonea Huruma Sana Mpenz wake

"Nakuahidi Trisha Sintafanya Baya lolote Niko Tayari Kulipia Makosa Yangu Lakini Sio kutengana Nawewe Sio Nikukose wewe Trisha Wangu Nakupenda sanaa Naomba Uje Uwe Mke wangu Naomba Unizalie Ndugu zangu Trishaa Siku Moja Sina Ndg sina Rafiki nina Wewe Trisha Wewe Ni kila Kitu"

Alex Alikua akitoka Machozi Trisha Alitoa Machozi
Hakuna Alieweza kumbembeleza mwenzie

Romeo na Julliet walizaliwa Upya TANZANIA❤️

Mapenzi Kati ya Alex Na Trisha Hayakupimika Kabisa
Alex Alisahau Maisha yake na Majukum yake Juu ya Makregani
Trishaa Alisahau Kuhusu Muddy na Aizack
Walijitazama wao Tu
Makregani Alikua akimfatilia Alex Kila Anacho kifany

ALEX Alifungua Duka Kubwa La Nguo za Kiume Na Alisahau Kabisa Ubabe Na Ukatili

Aizack ni mtu aliepinga sana Mahusiano yale
Alimpenda Trisha Kwa kipindi Kifupi cha Kuonana na Trishaa alivutiwa Nae sana lakn alichelewa Kusema

"Gentleman wako Huyoo Kafika Hivi Hata Anafanya Kazi Kweli Huyuu Kutwa Yupo Hapa "
Ray Alikua akimwambia Trisha Baada ya Kumuona Alex Akija nyumbn kwao
"Ooh Umefika baby"
"Yeah Twenzetu mi Hata Sikai"

Trisha Alikua Ameupara Mwenyew KWA mtoko maarum na Alex wake

Wakati wanatoka Aizack Alikua Ndo Anafika Eneo Lile
Walipishana Baada Ya kusalmia Waliondoka Trisha na Alex,
Aizack Alibaki Na Rey

"Leo Tunaenda wapi Sultan wangu"
"Nataka Twende Mbalii Hukoo twende Tu"

Alex Alikua Na Piki Piki Nyingine kabisa Usafir wake Mkubwa anaoupenda

Waliendesha Mpaka Beach Moja Jijini Dar es salaam Walichagua W/end yao Siku Hiyo Waimalizie Hapo

"Umeona Hapa nitakuchora Tattoo Hapa Jina Kubwaa TRISHA na kopa Kubwaaa nitaweka KWA Hapa🥰😃"
Alex Alikua akiongea huku akionesha Kifuani Pale Wakati Trishaa amemlalia Miguuni Wakiwa kwenye Mavazi ya beach

"Kwenye Moyo wangu kuna Tattoo Kubwaa Ya Alex Unajua Mi sipendi Uwe Unacheka Mbele za Watu wanawake wengi wanakutazama Wewe mi sipendi"

"Heyyy Nyie Msiwe Mnaniangalia Trisha Wangu hapendi 😄😀

Alex Alisimama Akawaambia Watu wote waliokua wakimshangaa
Trisha Alisimama Nae Akawa anamziba Mdomo Vile Alivyo Mfupi Hata Hamfikii Wakageuza mchezo
Trishaa alipona Alex anamwambia KILA mtu pale Beach Usiniangalie Mke wangu Mkorofii 😃
Trisha Akaanza Kumpiga na Michanga Wakaanza Kukimbizana Trisha alichoka Akakaa Chini
Alex Alifika akambeba🥰Kalivyo Kanamwili mdogo Mdogo Akaanza Kukimbia Naye
"Bby Utaniangusha nishushe ,nishushe Plzzz "
Trisha Alikua analalama Huku akipiga Piga Miguu mgongoni mwa Alex

Watu wote waliwaangila na Kucheka Waligeuka Sinema Maeneo Yote ya beach Muonekano wa Alex Ulimvuta Kila Mwanamke kutamani yeye Ndo angekua TRISHA KWA Wakati Huo

Pembeni Kulikua Na wasanii wakitoa Live Show

Alex alienda Kuchukua maiki Moja Kwa Muimbaji

Watu wote walibaki Kumuangalia Trisha Hakuelewa Alex anataka Kufanya Nini

Alex alitengeneza Koo lake Vizur
"Babyy Acha utaniaibisha"
Trisha Alimuwahi Alex Akamwambia KWA kunong'ona

Alex Alimshika Mkono akamrudisha Mpaka Walipo watazamaji wengine bila Kusema Kitu alimtazama KWA macho yaliyomaanisha Honey Tulia💋

Trisha alitulia Kuona nini Alex Anaenda Kufanya

Wakati Yote hayo yakiendelea kuna mtu Aliekua akifatilia KWA Ukaribu sana Mienendo Yote ya Trisha na Alex
Alionekana anachukizwa Sana na Alex
"Hiyo Alama hapo niya Nini??"
Aliangalia sana kovu la Alex Karibu na Bega Akiwa na Ham ya Kujua Hiyo Alama Imetokana na nini?

*Mwisho season one*
.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NI JAMBAZI ILA ANAYAJUA MAHABA 🙈♥️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️ Mwisho s1 16 To 20  >>> https://gonga94.com/semajambo/ni-jambazi-ila-anayajua-mahaba-mwisho-s1-16-to-20

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
majario 23 Aug 2025 06:21
mambo
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest