Basi tulilala kweli kwenye gari, asubuhi na mapema tuliwahi ile foleni tukawa wa kwanza kuingia yule babu alivyotuona akaanza kucheka akasema mbona mmenikazania sana vijana mnadhani mi natania eeeh??
Alex akamwambia tunajua unaweza kutusaidia babu tunakuomba sana utusaidie , akasema siwezi kijana embu ondokeni huyo mgonjwa wenu anaweza kukaa naweza mfanya akafa hapa hapa kwahiyo ondokeni
Niliogopa kufa tena wakati nimeanza kupata matumaini ya kupona , inno akamwambia alex tuondoke alex alikuwa mbishi kama alitaka kupanic lakini inno alimzuia
Tulikaa ndani ya gari hapo wanajadili jinsi ya kufanya muda huo kama mungu alipiga simu zakia
Alex aliweka sauti ili wote mule wasikie
"Alex mpo wapii??" aliuliza zakia
"Bado tupo kwa huyu mzeee hataki hata kutuona"
"Sikia alex zipe pesa zoteee, nilizo mpa Juddy amempa huyo babu et asiwasaidie na amemwambia kuwa ndio huyo aliemfunga kwahiyo msitumie nguvu huyo babu hana utani , tafuteni njiaa ya kupita ambayo ni salama asije kuwadhuru"
Alex akasema sawa zakia Asante, baada ya kukata simu walitazamana na inno
"Tunafanya ninii??" Aliuliza inno
"Naona tutumie pesa zile zile hakuna mtu anaweza kwenda kinyume na pesa "
"Lakini sio.kwamba tulikuwa tunataka bure hata hivyo"
"Hapana yaan hapa tuweke pesa mbele kabla ya maongezii"
"Kama shingap??"
"Ye katoa laki tano , nitatoa ml 5 cash"
Inno alishusha pumzi akasema
" nitaongeza mil 5 walau achanganyikiwe kabisaa".
Wote walicheka kwa jinsi inno alivyoongea hiyo kuchanganyikiwa, hata mimi nilicheka ila ndo hivyo nachekea kwenye chupa tenaaa hakuna mtu anaona
Alex akamwambia inno aende kuleta pesa haraka sana wakati huo ilikuwa inakimbia kwenda jioni , yaan alex anamwambia ahakikishe pesa inafika kabla ya jua kuchomoza
Tulikaa pembeni inno akaondoka na subira na Garii, alex alibaki ananiambia kama kawaida yake yaan mke wangu hapa lazima upone laa sivyo.huyo babu nakata kichwa chake walai naapa namkata kata atajua yeye huko ...
Baba mkwe alitupigia simu ni kawaida watu wa nyumbani kupiga simu mara kwa mara kuuliza kuna nini kinaendelea alex alimwambia kuhusu kusubiri pesa na vile zakia alituambia
Baba akasema ye atatoa ml 5 yaan tumpe mil 15 , pesa zilikuwa nyingi mnoo yaan pesa zilikuwa nyingiii mpaka nikawa namchukia huyu mganga mpuuzi kweli kweli mbwa kabisa mungu awaangamize mbali watu wa namna hii ..
.tuliomba sehemu ya kulala mana usiku nao ulikuwa tayari umepiga hodi afu inno hakuwa amerudi , tulimuahidi yule babu kuwa kesho tutaondoka akasema sawa
Alituonesha pa kulala palikuwa pachafu hata hapatamaniki lakini watu wamelala hivyo hivyoo na sie tutafanya nini sasa , Alex aliniweka chini akawa amenikumbatia hakuna hata mmoja kati yetu ambae usingizi ulimpia
.sijui alex alikuwa anawaza nini lakini mie niliwaza tu hili liishe salama hela ifanye kazi kama imani imemshida yule mzeee ..
Alfajir nakumbuka ndio inno alikuja , haraka tuliwahi foleni
Alex akamwambia inno na subira wasiingie tuingie mimi na yeye tu
Akasema anahitaji kumshawishi huyo mtu mana pesa peke anaona kama hazitoshi
Zilikiwa ml20, embu fikiria mtu ameniroga yeye anapewa pesa nyingi hivi ili tu kufungua uchawi wake
Namlaani huyu mzee kila siku kwenye maisha yangu pesa anayokula ni ya dhambi na ninaamini alishahukumiwa huko alipo mpuuzi yulee
Tuliingia na alex alipo tuona akasema nyie mbona mnanipoteza muda sanaaa
Alex hakusema kitu alisongea mbele ya yule mzee akiwa na kile kibeg cha hela kisha akapiga magoti akamwambia
"Mzee mi najua wewe ni binadamu na kwamwe hauwezi kudhuru mtu asie na hatia hata mbigu haiwezi kuvumilia hilo
Lakini wewe sio mkamilifu kiasi kwamba mtu aje aseme shida yake na ujue kuwa anakuongopea
Pesa hizi baba yangu lakini kabla ya hizi pesa naomba unisikilize vizuri ndio.ufanye maamuzi mke wangu akipona nitakuongez ml 20 zingine "
Jamani nyie pesa ni sabuni ya roho naapa niliona koo la yule babu anavyomeza mate mana mpaka mikono yake ilikuwa inatetemeka nilijua wazi anatamani kushika zile pesa
Nina uhakika hata ml1 hakuwahi kushida kwa pamoja kwenye hiyo kazi
"Enhee nakusikiliza kijana" alimpa ruksa alex aendelee kuonge , nilishusha pumzi nikasema hili sasa mungu lifanye liwe jepesi tuvule hapaa
Babu... kuna bint aliwahi kuja hapa zamani kidogo anaitwa Juddy alikuja kwa sababu anataka kumdhuru mwanamke aliemchukulia mwanaume wake
Mwanamke huyo ni salma ambae ni huyu na huyo mwanaume ni mimi hapa
Nafikiri hilo unalijua vizuri sanaaa!!!"
"Naaaam!!! Bila shaka"" yule mzee alijibu huku anatikisa kichwa nilipata hasiraaaa mjinga huyooo
Alex akaendelea kuongea wakati alikuwa bado amepiga magoti yake maskini na machozi kabisa yanamtoka mhu nyie hii dunia acha
Unamuomba mtu aliekufanyia vibaya kuutoa ubaya , unamuomba kwa magoti na machozi na bado unampa pesa yako aisee huyu mzee nilikuwa naomba mungu baada ya kumpa pesa akafie huko mbali mbwa kabisaaa
"Mzee yule.juddy kweli alikuwa mwanamke wangu, tena nilimpenda sana lakini ni mtu ambae hakuwa kuthamini upendo wangu, kama isingekuwa huyu salma ile siku kama sio kufa basi ningejeruhiwa vibaya sana na raia na yote kwa sababu ya huyo juddy mwanamke aliejawa na tamaaa tu"
"Ki vipii" aliuliza huyo mzee huku anajitengeneza vizuri macho yake yalikuwa juu ya zile pesa tuu yaan mate anameza
ITAENDELEA....
0657171961
KWETU morogoro.