Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NIMEKUSAMEHE ILA SITOSAHAU SEHEMU YA 02

17th Sep, 2025 Views 13



WHATSAPP 0675137453

FULL STORY TSH1000
"unasemaje sijakuelewa?" nilimwuliza Magreth
"nimesema hivi mbona jana nimemkuta mdogo wako na shemeji yake kwenye mazingira yasiyoeleweka"

"mdogo wangu gani?"
"kwani una wadogo wangapi hapa mjini Rebecca unaoishi nao?"
"nina mdogo wangu mmoja tu, Diana"

"basi huyo huyo"
"mazingira yasiyoeleweka kama yapi?"
"eeh wewe chunguza tu mwenyewe sitaki kufungwa mie bure"
"hujaachaga tu uchonganishi Margrth rafiki yangu unakumbuka ulitaka kusababisha ndoa ya mzee wa kanisa yule mama kuvunjika kanisani?"

"lakini si lilikuwa la kweli lile jambo nililoongea Rebecca au nilikosea jamani kuufichua ukweli?"

"umewafananisha tu mdogo wangu Diana alikuwa chuoni kwenye sherehe na rafiki zake na shemeji yake alikuwa kwenye kikao cha dharura ofisini kama wangekuwa wote basi wangerudi pamoja hata wangesingizia tu kuwa wamekutana njiani sipendi maneno maneno mimi sikuhizi Magreth"

"mh haya nileteage mie hiyo hela niende zangu, mdomo koma!" Magreth aliongea nikatikisa kichwa kumsikitikia kwa tabia yake ya umbea mpaka sikuhizi nimepunguza uswahiba nae tofauti na zamani nilipokuwa swahiba wake mkubwa, yote kutokana na mdomo wake huo uliokuwa kama cherehani, halimpiti jambo kashalijua na kulisambaza hasa kwangu, sasa isije ikawa na yangu anayasambaza kwa wengine hivyo nikawa simwambii kila kitu kuhusu maisha yangu

Niliingia ndani na kuchukua kiasi cha pesa elfu thelathini nilichokuwa nacho, nikatoka na kumpatia, akanishukuru na wala sikutaka anilipe kwa sababu tulisaidiana sana hasa kipindi kile nilipokuwa sina kitu nilipoolewa na kuhamia kanisani kwao ambapo alikuwa anasali mume wangu kabla hajanioa

"leo nimezaliwa mwenzio" .
"waaoh dah happy birthday to you shoga yangu ila siku imenikalia vibaya sina hata zawadi jamani?"

"usijali we njoo tu baadae jioni zawadi ya pekee ninayoitaka kutoka kwako ni kukuona baadae jioni nitaandaa chakula kizuri sana"

"vipi kitimoto itakuwepo?" alininong'oneza sikioni akiwa ni mpenzi sana wa kitoweo hicho

"sikupanga lakini kwa sababu nina uhakika upo nitatengeneza special for you yaani"

"uuuwiii lazima nije kuchambua mchele kabisa utanipigia basi ngoja niende nikalipe lipe najua sitakosa elfu ishirini"

"haya kwaheri" nilimuaga huku nikibaki natabasamu nikafunga bomba la maji na kurudi ndani kuendelea na mipango mingine ya usafi nikisaidiana na dada wa kazi Aisha

Siku ilienda hivyo nikiwa nimeshinda nyumbani tu sijaenda kwenye biashara yangu ya saluni kwa sababu ya mambo kadhaa ambayo hayajakaa sawa na siku chache zilizopita niliumwa umwa, mdogo wangu Diana alirudi kutoka chuoni tukasalimiana na moja kwa moja akaingia mpaka chumbani kwake, nikiishi nae na kumsomesha mimi mwenyewe tangu sekondari, kidato cha tano na sita mpaka sasa yupo chuoni mwaka wa mwisho

Nilipita chumbani kwake na kumsikia akiongea na simu maana nilitaka kumuita nimuagize

"mh kaninunulia bonge la simu yaani ngachoka, nilidhani itakuwa zawadi ya kitoto sijui ya vi infinix sijui nini shoga siyo infinix wala tekno wala samsung yaani simu ya hatari wanayotumia mastaa mbona chuoni nitavimba" nilimsikia nikavutiwa na maongezi yake kama dada mtu nikataka umbea kidogo nikafungua mlango na kumkuta amekaa kitandani kwake haraka akakata simu aliyokuwa anaongea na rafiki yake huyo

"yaani Diana hata kunionyesha mimi dada yako hayo mambo mazuri unaanza kwa marafiki jamani, shemeji yangu nini?" nilimchungulia mlangoni sikuingia kabisa
"utaiona dada yangu wewe tena"

"mbona hunionyeshi hata kwa picha shemeji yangu nimjue umelete hata nyumbani siku moja tule nae chakula maana anajitahidi kaka wa watu kila siku nakuona na magauni ya bei mbaya na maviatu, utulie Diana usiruke ruke kijana wa watu utamuua kwa presha"

"hahaha dada bwana kwani unaniona mimi mcharuko au??" alicheka na kijikaratasi kimoja kikapeperuka kutokana na upepo wa feni aliyoiwasha kikanifikia mguuni nikakiokota na kukisoma, ilikuwa ni risiti, ilionyesha bei ya simu na aina ya simu, vyote vikanishtua nikamtazama Diana ambae alipogundua nimeshika karatasi yake akaja na kuninyang'anya

"Diana simu ya milioni mbili??"
"dada kawaida tu unaionaje si Iphone macho matatu hii tena kuna toleo mpaka la ngapi sijui huko" alinionyesha boksi la simu hiyo

"hela unapata wapi?"
"si mchumba wangu nawewe?"
"sasa si ungemwomba akufungulie biashara"
"atanifungulia tu hili trela"
"mh haya, hayanihusu chakula kipo jikoni"
"nimeshiba dada nataka nilale tu"
"sawa" nilimjibu na kuufunga mlango wake na ndipo nilipokutana na mume wangu Dawson nae alikuwa ndo anaingia, nikampokea begi na kulipeleka chumbani nikalitua na kutaka kumfungua vifungo vya shati

"acha tu nitavua mwenyewe" aliniambia
"pole na kazi mume wangu"
"asante" alinijibu akavua suruali yake wakati anataka kuitundika kwenye henga kijikaratasi kikaanguka akiwa hajakiona mimi nikainama na kukitazama kilikuwa ni cha maelekezo ya jinsi ya kutumia simu lakini simu yenyewe niliyoina kwenye kikaratasi hicho ni kama ile mpya niliyoiona kwa mdogo wangu Diana sambamba na eyerphones zilizoandikwa jina la simu lilelile kama ya Diana....

Full Story TSH1000 tu
Whatsapp 0675137453.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIMEKUSAMEHE ILA SITOSAHAU SEHEMU YA 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/nimekusamehe-ila-sitosahau-sehemu-ya-02

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest