Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Ninapenda sana watoto na ndoto zangu siku moja nipate mtoto niweze kucheza naye na awe akicheza nami. Nilimpenda sana msichana fulani, na sikuweza kufikiria maisha yangu bila yeye. Nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni kwa mshahara wa wastani

10th Sep, 2025 Views 23

.

Siku moja msichana wangu alinieleza juu ya tangazo la kazi katika kampuni ya uagizaji na usafirishaji iliyokuwa inalipa mara mbili ya mshahara wangu. Nikaomba ruhusa kwa meneja wangu na nikaelekea upesi kwenda katika kampuni hiyo. Wakati nikiwa njiani, gari lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi na msichana mmoja lilikanyaga miguu yangu(lilinigonga). Kwa furaha niliyokuwa nayo ya kupata hiyo kazi sikutazama pande zote; lengo langu lilikuwa moja tu – nipate hiyo kazi nimfurahishe mpenzi wangu na kutimiza matakwa yake, hasa kwa kuwa alikuwa na mahitaji mengi.

Nilipozinduka nilijikuta nipo hospitalini, nikiwa kwenye kitanda. Niliona msichana mrembo amesimama mbele yangu na maua mkononi, akinichekea kwa upole. Nikamuuliza: “Wewe ni nani? Nipo wapi?” Akasema: “Tuliza moyo, utajua yote kwa wakati wake.” Nikalia nikisema: “Mguu wangu unauma.” Daktari aliingia na kunipa sindano ya kutuliza maumivu, kisha akasema: “Tulikata mguu wako wa kulia kutokana na ulivunjika na kuumia sana juu ya ajali.”

Nilipata mshtuko mkubwa na nikavunjika moyo, nikalia sana. Msichana yule aliketi kando yangu na kusema: “Samahani, mimi ndiye chanzo. Nilikuwa naendesha kwa kasi kubwa, kosa ni langu nisamehe.”

Nikampigia simu mpenzi wangu na kumweleza yaliyotokea. Alifika kwa haraka, lakini alipoona hali yangu, alishtuka na kusema maneno machache: “Samahani, nakutakia afya njema.” Kisha akaondoka. Baada ya nusu saa tu aliniletea ujumbe wa simu akisema: “Samahani, siwezi kuendelea na wewe. Nimeposwa na mchumba mwingine na wazazi wangu wamesisitiza ndoa hii.” Baada ya hapo akakata simu na nikagundua baadaye amebadilisha nambari yake.

Wakati wote huo, yule msichana mrembo aliyenisababisha ajali hakuniacha; alibaki nami akilia na kuniona. Baada ya wiki mbili, daktari alinipa ruhusa ya kutoka hospitalini nikiwa na kiti cha magurudumu, na msichana yule alinishika mkono hadi nyumbani. Nilipoingia nyumbani nililia sana nikisema: “Ewe Mola, kwa nini uliniacha? Kwa nini mpenzi wangu aniache? Kwa nini nimepoteza kazi? Kwa nini unifanye kuwa kilema maisha yangu yote?”

Lakini huzuni haikudumu sana, kwa kuwa msichana huyu hakuacha kunitembelea kila siku. Kila siku ambayo hakufika, nilihisi upweke mkubwa.

Baada ya miezi miwili nilipokea barua ya kuitwa jeshini, lakini nilipimwa na kupewa msamaha wa kudumu kutokana na hali yangu. Rafiki yangu wa karibu ndiye aliyepelekwa badala yangu, na bahati mbaya alikufa kutokana na mlipuko katika ghala la gesi lililokaribia kambi yao. Nililia kwa ajili yake, lakini nikamshukuru Allah kwa kuniokoa.

Kisha nikasikia kutoka kwa marafiki kwamba yule mpenzi wangu wa kwanza ameolewa na jirani yao. Lakini walikuwa na ugomvi wa kila siku kwa sababu aligundulika kuwa tasa, na mimi nilihuzunika kwa ajili yake, ila nikamshukuru Allah kwa kuniepusha naye, hasa mimi nikiwa ni mwenye mapenzi makubwa kwa watoto.

Baadaye nilipokuwa nikisoma gazeti, niliona tangazo kuwa ile kampuni ya uagizaji na usafirishaji ambayo nilitaka kujiunga nayo ilikuwa imefilisika na wafanyakazi wake wote wakafutwa kazi. Nikasema “Alhamdulillah” kwa rehema ya Allah.

Katika kipindi chote cha zaidi ya siku 70, msichana yule mrembo hakuwahi kuacha kunisaidia – aliniletea mahitaji yangu yote ya nyumbani. Hapo ndipo nilipoamua kumuomba tuoane, ila nilihofia atanikataa. Wakati fulani, nilitaka kumueleza hisia zangu, lakini kabla sijafungua kinywa, yeye mwenyewe akasema: “Je, utakubali kunioa mimi?” Nikashangaa na mwili wote kunitetemeka nikasema: “Umesema nini?” Akarudia: “Je, utakubali kunioa mimi?” Nikasema: “Mimi sikubali huruma kutoka kwa mtu.”

Akanijibu: “Wallahi hii si huruma, bali nimekupenda kweli na siwezi kuishi bila wewe.” Nikamwambia: “Lakini mguu wangu uliokatwa utakuwa kizuizi katika kazi.” Akasema: “Wewe utakuwa meneja katika moja ya kampuni za baba yangu, kazi yako itakuwa ya ofisini tu, haitahitaji kusogea sana.” Nikashangaa na machozi yakaanza kunitiririka nikisema: “Ewe Mola, nisamehe kwa kuwa nilipingana na hukumu yako na uoni wako wa mbele.”

Kweli, lau isingekuwa ajali hii ningekuwa:

1.Nimeoa mwanamke tasa, mwenye kujipenda pekee, ambaye Allah alinifunulia hakika yake kabla sijachelewa.

2.Ningeingia jeshini na kufa kwenye mlipuko. Allah aliniokoa kwa kuniondolea mguu na kunipa uhai.

3.Ningejiunga na kazi isiyodumu, lakini sasa Allah amenipa kazi yenye mshahara mkubwa zaidi kuliko nilivyotarajia.

MAFUNZO MUHIMU

1.Kila kilichopotea kina hekima ya Allah – Unaponyimwa kitu, usione ni hasara tu. Huenda Allah anakuepusha na shari kubwa au anakutayarishia kheri kubwa zaidi.

2.Watu wa kweli hujitokeza katika shida – Yule mpenzi wa kwanza alimuacha kijana alipopatwa na matatizo, lakini msichana aliyesababisha ajali ndiye aliyebaki naye mpaka mwisho, akawa chanzo cha faraja na furaha.

3.Mipango ya Allah ni bora kuliko mipango yetu – Kijana aliona ajali, kupoteza kazi na kupoteza mpenzi kama majanga, kumbe yote yalikuwa njia ya Allah kumlinda, kumuepusha na balaa, na kumpa kazi bora pamoja na mke mwema.

🌟Mwongozo:
Mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa ukurasa wa Sufian Mzimbiri , amini daima kwamba Allah huchagua bora kwa ajili yako. Usihuzunike pale Allah anapokuondolea kitu; bali amini kwamba atakupa kitu kizuri zaidi. Ukipatwa na mtihani usilaumu mapema tulia hapo Allah amekuokoa na balaa kubwa ambalo lingekupata 💜

Endelea kufuatilia ukurasa wangu ujifunze mengi zaidi, like, comment na share na wengine uwanufaishe,

Follow ukurasa wangu uwe wakwanza kusoma♥️📚

Mungu akuepushieni na mitihani na mabalaa.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Ninapenda sana watoto na ndoto zangu siku moja nipate mtoto niweze kucheza naye na awe akicheza nami. Nilimpenda sana msichana fulani, na sikuweza kufikiria maisha yangu bila yeye. Nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni kwa mshahara wa wastani  >>> https://gonga94.com/semajambo/ninapenda-sana-watoto-na-ndoto-zangu-siku-moja-nipate-mtoto-niweze-kucheza-naye-na-awe-akicheza-nami

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest