Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

NIPE YOTE DADYπŸ’žπŸ’ž26~27

19th Jul, 2025 Views 21

NIPE YOTE DADYπŸ’žπŸ’ž26~27

Baada ya Nasra kunipigia nilienda chumbani kwa ajili ya kwenda kuzungumza naye..nilishangaa sana kwa yale aliyonielezea😰

Nasra aliniambia mimba imeharibika na kibaya
zaidi kapigwa talaka tatuπŸ₯ΉπŸ˜°

NilichokaπŸ₯Ή nilitamani kujua kimetokea nini ila
hakutaka kuongea kiundani zaidi, Selim aliniuliza
shida nini.??

Kutokana na namna tulivyo na Selim sikuona
sababu ya kumficha nikamwambia kila kitu
akanambia nijiandae twende wote tukamuone..

Niliingia bafuni nikajiandaa kisha tukatoka na
kwenda kwa Nasra tulikaa huko siku nzima tukarudi usiku..

Wakati tuko njiani Jabir alitupigia simu akatwambia mko wapi mmeondoka bila kuaga huku nyumbani mambo yamechemka mnasubiriwa nyinyi tu..

Tulijaribu kumuuliza kilichotokea akakataa kusema tuliogopa tukaanza kuulizana kuna nini??Jabir alituambia tuwahi maana mambo si mazuri huko nyumbani..

Selim aliongeza mwendo wa gari tulifika nyumbani tukashuka kwenye gari haraka tukaelekea ndani..ile tumefika tu mlangoni baba mkwe akainuka na kuondoka..

Tuliangaliana na Selim kisha akaniuliza "mke
tuingie au tukaswali kwanza?
"Tuingie kuswali baadae" tuligonga tano na
kuingia..

ukweli tulijifanya wababe ila moyoni tulikuaa
tunatetemeka Selim akawa anani nong'oneza
eti unafikili kuna nini ila kama kimenuka
tutaondoka usiku hu huu mi nikajibu sawa😩

Tuliingia Seblen tukakuta watu wote wamekaa
macho yote kwetu, tukasalimia wakajibu mama
na aunt mzee akakausha basi tukaaga na kwenda
chumbani.

Tulifika chumbani tukaanza kuchekana mimi namwambia Selim nimuoga na yeye anaiambia eti mimi ndo muoga.

Basi selim alimuita Jabir akaja tukamuweka kati
kwann atudanganye akasema alitaka kutupima
imani walichimbana mikwala pale kisha
wakiishia kucheza gemu.

Mda wa kulala ulipofika Jabir aliaga na kuondoka selim aliniangalia na kusema "Unajua huyu mpuzi
kanishtua sana yani roho ilikuwa juu juu nilikuwa nishaanza kuwaza mengine"

Nilicheka na kusema"nilijua tu na tulivyojivika
ubabe kumbe mioyo inatokota"Usiniambie kwamba na wewe ulikuwa unaogopa?"

"Ndio kwani mimi nina moyo wa jiwe kwanza
nilikuwa nawaza kuna nini au tumefanya kosa au ndo imewadia siku ya kufukuzwa🀣🀣ila tukifukuzwa si umejipanga eh?? Akasema ndio"

Tulicheka kwa pamoja kisha tukapanda
kitandani na kupeana mgongo usingizi ukachukua
nafasi yake...

Kesho yake asubuhi Selim aliwahi kuamka
akajiandaa kisha kabla ya kuondoka akaniamsha
niliamka kichovu nikaangalia mda ulikuwa
umeenda nikamuuliza "Mbona mda umeenda
sana umeshakunywa chai kweli?"

"Ninywe chai uliyoipika usingizini, mwanamke
mvivu wewe muone"
"Nimekuuliza kwa upendo we unanijibu shombo
unataka tukiwashe ee upendo gani Norah upendo unalala umenigeuzia mgongo kweli?? Hutaki hata nikusogelee huo ndo upendo??"

Nilikaa kimya selim aliondoka nikaamka na
kuingia bafuni nikaswaki kisha nikarudi na kukuta
sim yangu ikiita niliichukua na kuiangalia kwa
mda kisha nikaipokea..

"Hello Nasra nambie"
"Poa mdogo wangu umeamkaje?"
"Mmhh kwanza Nilitoa sim
sikioni na kuangalia huyu ni Nasra huyu au naota??imekuwaje tunaanza kupigiana simu asubuhi asubuhi na kuitana mdogo wangu hii imeanza lini?."

Nilijibu nimeamka salama kisha akauliza na shem
je mmhhh nikaguna kimoyo moyo nikajibu yuko poa mara ameshaenda kazini? Nikajibu ndio akasema sawa kisha akaniaga na busu juu..

Nilibaki nawaza mbona kama kuna kitu
anakitafuta maana haijawahi kutokea akanijali wakati maisha yetu yote huwa tunaishi kama
Tom na Jerry inakuwaje ananibadilikia ghafla hivi

na hizi shem kaamka mara kashaondoka vp
subiri isije kuwa anataka ku..... hapana sidhani
lakin ngoja.

Nilichukua sim na kumpigia Zuu msichana wetu wa kazi nikamuuliza kama nasrah amekuwa mtu wa tofauti usikute kuachwa kumemnyoosha zuuh alipokea simu nikamwambia Samahani jana nilipokuja hapo nilikosa muda wa kupiga umbea na wewe..

nilikuwa nataka kujua Nasra siku hizi yukoje namaamisha maendeleo yake na tabia zake maana kanipigia sim anaongea kama mtu aliebadilika sana kabla Zuu hajanijibu nilisikia sauti nyuma yangu ikiuliza

"Inamaana wewe sio Nasra?" Mungu wangu nilikata simu haraka Nikageuka huku natetemeka mwili mzima kimoyomoyo nilijisemea toba kimeumana"

Alikuwa Aunt Suna nilitoa macho na kukosa
cha kuongea alisogea na kuuliza "nijibu swali
langu inamaana wewe sio Nasra?"

Nilipata kigugumizi mara sm yangu ikaita
kuangalia ni Nasra na ubaya wa sim yangu
ikiita inataja jina la mtu anaepiga...pamoja na kwamba chumbani kulikuwa na AC lakini niliswet mwili mzima..

Aunt akauliza tena "Nakuuliza inamaana wewe
sio Nasra?" Aisee za mwizi ni arobaini basi hii
ndio ilikuwa arobaini yangu,

nilikaa kwenye sofa na kumuomba Aunt akae ili tuweze kuongea uzuri huwa ni mwelewa akakaa kwanza kabla ya kukaa alirudishia mlango maana ulikuwa wazi...

Baada ya kukaa nilishusha pumzi na
kusema, "Aunt nisamehe kwasababu najua
nikosa ndio mimi sio Nasra bali ni Norah

alitoa macho na kusema "unasema kweli?"
"Ndio Aunt mimi ni Norah "
"Mungu wangu imekuwaje ukaolewa wewe
wakati alitakiwa kuwa dada yako na kwann
mlificha??"

kwa swali hilo sikuwa na lakumficha
nikamwambia kila kitu hadi kufikia hatua mimi
kuchukua nafasi ya Nasra.

Alishusha pumzi na kusema"ama kweli watu
tuna siri yani mda wote huo tumekaa tukijua we
ni Nasra kumbe sio? Ila kuna mda nilikuwa
nikikuangalia nilikuwa napata hisia kuwa kuna
kitu hakiko sawa ila nikawa napuzia kumbe
nilikuwa sahihi.

Na vp kuhusu Selim anajua hili?"
"Ndio Aunt anajua japo hakuambiwa na mtu
yoyote hivyo sijui alijuaje"

"Selim ni mjanja sana sio mtu wa kudanganywa
kirahisi ndio maana alitambua, sasa sikia hili
swala ni zito najua ikija kumfikia Mohammed
itakuwa kesi na unaweza kutokea hata ugomvi
maana familia yako imefanya makosa.

kama ilitokea hivyo wangekaa na
sisi na kuongea ukweli naamini tungejadili hili
swala na kupata mwafaka ila kwa hili hakika
sio sawa.

Kwa maan hiyo unatakiwa kuhakikisha
halijulikani haraka, mimi najua mahusiano yako
na Selim hayajakaa vizuri bado hamjawa na ile bond hivyo ikitokea mitikisiko tu itakuwa rahisi
kuvunja uhusiano wenu.

Sijui unanielewa? Norah"
"Ndio Aunt nakuelewa"
"kwasasa hakikisha unamuonesha upendo
wa Hali ya juu mwenzio na hakikisha unashika nafasi yako vizuri umenielewa??

Ndio Aunt nakuelewa lakini..hakuna cha lakini Norah na hiki ninachokueleza kifanyie kazi hakikisha unamkamata selim masikio nakuhakikishia siku wazazi wake wakijua kuwa wewe siyo Nasra watakutimua hapa kama mbwa..

Mkamate selim kwa kila kitu simaanishi kitandani tu no bali kwenye kila kitu tengeneza urafiki ili uweze kuwanae kwa kila kitu duh Aunt angejua hata penz tu hatujawahi kupeana😒

But nilimwambia ni sawa nitajitahidi..aliniambia sawa Usijali,sasa natakiwa kuanza kuwaangalia
vizuri ili niwajue maana nitakuja kuchanganya
mafaili

Niliinuka na kuchukua sm niliyokuwa nimeiweka kitandani kisha nikaingia kwenye picha na kuanza kumuonesha Aunt tofauti yangu na Nasra..

Iko hivi mimi na Nasra tofauti yetu ya
kwanza ni kope mimi kope zangu ni ndefu na
nyingi Nasra zake ninyingi ila nifupi.

Kingine mimi nina alama kwenye mkono ila
Nasra anayo shingoni kwanyuma sema huwezi
kuiona kwasababu anajifunika mda wote,

kingine ni tabia mimi naongea sana Nasra anaongea taratibu sana na kwaupole.
Cha mwisho meno kama ukimuangalia Nasra
vizuri utagundua meno yake hajang'aa kama
yangu alafu yeye ni madogo kiasi basi hivyo
Ndio vitu ambavyo tunatofautia,

najua ningumu kutofautisha kwasababu ni vidogo vidogo aunt aliniambia Usijali nimeelewa yani hivi ulivyoniambia ndio nimeelewa ila kwa haraka haraka mtu anaweza kushindwa kutambua tofauti yenu maana mnafanana sana..

Basi tuliongea kidogo kisha tukainuka na
kwenda jikon nikamsalimia mama mkwe kama
kawaida yake akaitikia kama hataki Aunt
alinishika mkono tukatoka mara tukakutana na
Jabir akiwa anaamka alivyotuona tu akaanza
kucheka tulisimama huku tukiangaliana maana
hiki ni kituko..

Aunt akamuuliza "We Jabir unashida gani
mbona unacheka kama chizi "
"Mama nimeota tukiwa tumekaa mezani alafu
mjomba akaja kwa bahati mbaya alivyotaka
kukaa kiti kikavunjika basi akadondoka sasa
hivyo alivyodondoka ndio kituko yani natamani mngekuwa kwenye hiyo ndoto na mimi mkaona ilivyokuwa🀣🀣🀣🀣

"Mfyuu nikisema we ni tahira nitaonekana
nakuonea embu tupishe muone kubwa zima
akili nusu"

Tulitoka nakukaa kusubiri mama mtu amalize
kupika, wakati nikiwa nimekaa uliingia ujumbe
kwenye simu yangu nilifungua na kusoma
alikuwa ni Zuu dada wa kazi wa kule nyumbani kwetu..

meseji yake ilikuwa inahusu tabia za Nasra, zuuh aliniambia kiukweli nasrah amebadilika
sana anamambo ambayo yeye mwenyewe hamuelewi...

Je ni mambo gani???je nasrah anamtaka Selim?? Norah atakubali kumuachia??

Full 1000

WhatsApp 0742133100.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADYπŸ’žπŸ’ž26~27  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-26-27
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest