NIPE YOTE DADYπππ31
Nilienda ofisini kwa selim kwa lengo la kwenda kumwelezea hali halisi ilivyo ili angalau aweze hata kunifarijiπ’π’
Baada ya kufika huko nilikuta mambo tofautiππnilimkuta Jeni akiwa amekumbatiana na selim wanapeanaππnilibaki nimesimama tu nawaangalia..
Waliachiana baada ya kuniona Jeni akatoka na kuja kunikumbatia kwa furaha huku akisema kanimiss, nilizuga na kujifanya nafuraha ili asije kuhisi tofauti.
Tulikaa na kuanza kuulizana za siku na mambo
mengine, mda huo Selim alikuwa akijifanya
kuwa bize wala sikutaka hata kumsumbua
nilivyoona nimekaa kaa mda mfupi niliaga na
kusema kuna mahari naenda kisha nikatoka na
kuingia kwenye gari.
Moyo wangu ulijaa uchungu na hasira nilihisi kila mmoja ananiumiza tuππwapi pa kwenda kuipata faraja??kama ilivyo kawaida yangu nikiwa katika hali ile huwa natamani walau nipate mtu wa kuongea nae ili nipanguze machungu,
nilitamani Selim aje walau nimwambie alafu nilieee kisha nitakuwa sawa ila ndio hivyo yuko na mtu wake..
Niliegemea usukani wa gari kwa mda mrefu nikawa nalia tu peke yanguππnililia sana bila kupata mtu wa kunipa pole..nilimaliza kulia nikainuka na kuwasha gari nikaenda fukwe moja ya bahari na kukaa huko..
Wakati nikiwa nimekaa macho yangu Yakiwa
bize kuangalia mawimbi ya bahari huku
machozi yakishuka misri ya mvua nilisikia mtu
akinishika mgongoni haraka nikageuka nakumtizama aiseeππalikuwa Skyler.
Sikufikilia mara mbili niliinuka haraka na
kumkumbatia si mnajua wale team ukiambiwa
una shida gani badala ujibu unaangua kilio
kama kunamtu kadanja basi ndio mimi
Skyler aliuliza nini shida niaangua kilio hicho bahati nzuri hakukuwa na watu wengi.
Skyler aliendelea kunikumbatia huku akinituliza
Taratibu, nililia mno na hii rangi yangu ilivyo
nilikuwa kama hoho nyekundu na mafua juu.
Baada ya kulia kwa mda nilinyamanza na
kukaa Skyler akaniuliza kimetokea nini?
Niliwaza kwa sekunde nikaona si vyema nikamwambia kinachonisibu kwasababu si mtu
wangu wa karibu kiasi hicho..
Basi nikaamua kumdanganya kwamba
nimeachwa masikin kaka wawatu akanipa pole
na maneno kadha wa kadha nikawa najibu
sawa nitajaribu, kwakweli alifanya kazi kubwa
mpaka kuhakiksha nacheka tena.
Sasa bwana kumbe Wakati nimetoka ofisini
kwa Selim.. Selim alinifuatilia mpaka nafika kule ufukweni nayy alikuwa yuko nyuma yangu ananifuatilia..
Alihisi kuna kitu hakiko sawa kwa bahati mbaya alipofika kule ufukweni alinikuta na Skyler hivo akaamua kutuangalia na kuondoka..
Karibu kutwa nzima nilishinda nikiwa na Skyler
jioni niliagana nae na kurudi nyumbani sasa ile
nafika tu nyumbani nikakutana na mabishano makali kati ya Selim na baba yakeπ³π³
watu wote walikuwa seblen kutokana na
vurugu sikuweza kusalimia nikabi nashangaa
Jabir alisogea na kuninong'oneza sikioni kumbe
ugomvi wao ni kuhusu Selim kutaka kuondoka
pale nyumbani.
Baba mtu alitoa kauli moja tu akamwambia
Selim"Kama umeamua kweli kutaka kuondoka
hapa nyumbani kwa lengo la kutaka kuwa na
mji wako sawa nenda ila kabla haujaenda achakila kitu ambacho unajua nicha kwangu na
uende ukaanze upya
Kauli hiyo iliwaacha watu midomo wazi sio watu
tu hata mimi nilibaki namshangao, wakati tukiwa
bado kwenye mshangao Jabir alinifinya
kunitaka nigeuke nyuma hatua za miguu ya
watu wakija upande wetu zikafanya nigeuke
haraka hee nilishangaa baada ya kumuona baba yangu anakuja akiwa ameongozana na Nasraπ³
Kusema kweli nilishtuka sana na kujiuliza wamekuja kufanya nini?Baba mkwe baada ya kumuona baba yangu alitulia na kuwakalibisha kwa furaha Selim alitaka kutoka baba akamwambia selim naomba uwepo wako tafadhali
Mara zote Selim humu heshimu baba hivyo
alikaa japo uso wake ulionesha hasira,nilimuangalia Nasra namna
alivyokuwa akiniangalia nikahisi Hawa
wamekuja kumwaga mboga kama nilivyo hisi
ndivyo ilivyokuwa.
Baada ya Salam baba aliomba kuongea kila
kitu lakin hakusema kuwa kamleta Nasra ili
abaki bali alisema ameona jambo alilofanya sio
zuri hivyo kaona ni vyema aje aseme na
kuomba msamaha kwa rafiki yake ambaye ni baba yake selim..
Baba alianika kila kitu mezani waliokuwa hawajui walibaki midomo wazi Kutokana na mchafuko wa Hali uliokuwa tayar umetokea pale ndani jambo lile lilikuja kuongeza hasira,baba mkwe alikasirika na kufoka kwa hasira Sanaa
upande wa mama mkwe akawa anasema ndio
maana natabia chafu sijui nilijua tu huyu sio
yeye maana Nasra ni binti mtiifu na mwenye
heshima
na huyu Norah ndio kaniharibia mwanangu maana kwann atake kuondoka wakati akiwa nae mbona alipokuwa bado hajaingia kwenye maisha yake alikuwa hana hata wazo huyu ndio chanzo cha yote.
Alivyosema hivyo nikama alimzibua masikio
baba mkwe kibao chote kikaniangukia mimi
Selim alisimama na kunitetea aunt pia akakaa
upande wetu fujo zikawa nyingi Nasra
alisimama huku akijifanya mpole na kusema "
Baba ni kweli swala la Selim kutaka kuondoka
limesababishwa na Norah na kumbuka mara
ya mwisho kuonana nae kipindi ametoka
honeymoon alikuwa akisema hapendi maisha
yakuishi na familia ya mume"
Nilimuangalia Nasra kwa mshangao mimi huyu
Norah nilini nikasema kitu kama hicho ukweli
nilishindwa hata kuongea nikabaki
ninacheka, kama mnavyojua ukicheka wakati
watu wanaongea ni dharau kubwa sana basi
hilo nalo likajumuishwa.
Baada ya mabishano kuwa mengi baba mkwe
alisimamaa na kusema "Bwana Khalid kwa
jambo hili umetukosea sana tena zaidi ya sana
na imeniumiza mno, sisi kutaka Nasra aolewe
katika familia hii ilikuwa ni kuendeleza na
kudumisha undugu wetu
pia tulimchagua yeye kwasababu tulimuona ni binti mwenye heshma mtiifu na kila aina ya tabia njema alikuwa nayo.
Hiyo ndio ilikuwa sababu tukamchagua yeye na
sio huyo ambae amekuwa na tabia chafu hata
macho yake ukiyaangalia anaonesha kabisa
hafai hata kuwa mke wamtu hasa kwa kijana
wangu.
Na kwakua hakutakiwa kuolewa yeye basi hata
hii ndoa ni batili haipo kabisa "Baba alikaa vizuri na kumjibu mzee mwenzake akasema "Nikweli ndugu yangu nimekukosea sana na unayo haki ya kuamua lolote juu ya hili ila kikubwa ninachokiomba kutoka kwako ni msamaha ili amani iendelee kuwepo"
"Amani na msamaha vipo na vitakuwepo ila hii
ndoa mimi siitambui tena na kwaanzia sasa
binti yako huyu atafutwa kwenye familia hii na
hii ndio kauli yangu ya mwisho hii ndoa
haitakuwepo tena talaka zitatolewa na kila kitu
kitafutwa.
Hivi ulishawahi kukaa na kuona maisha yako
kama movie?basi siku hii nilikuwa na angalia
huku nikiona kama picha la kihindi sio siri
niliwaona wazee wote wale hawana akili Selim alisimama na kunishika mkono kisha
akasema
"mmeongea sana na kutumia nguvu
nyingi mkasahau huyu ni mke wangu mimi na
mimi ndio niliemuoa si nyie, labda niwambie
kitu huyu mnaemuona ni mchafu wa tabia ndio
mwanamke wangu mke wa maisha yangu."
"Nampenda na tabia zake hizi hizi na najivunia yeye hivyo siwezi kumuacha kwa namna yoyote ile iwe umesema wewe baba au hata aseme mkuu wa dunia siwezi kumuacha Norah."
Alivyoongea hivyo selim Mama yake alisimama na
kusema "Selim baba yako anaongea
unasimama kupinga ? Kama alivyokwisha
kusema hii ndoa haipo kwasababu yeye
hakuwa mlengwa hii ndoa ni batili..Batili hivi mnajielewa? Mwanamke nimeishi
nae miezi leo mnamuona hafai??
Tumefanya kila kinachotakiwa kufanyika kati ya mume na mke alafu mnasimama na kusema batili?
Lakin siwalaumu hivi ndivyo mlivyo roho zenu
zimejaa ubaguzi na ubinafsi wa Hali ya juu
hamuwazi kuhusu watoto wenu bali mnawaza
maslahi yenu.
Na wakati huu sitoruhusu hilo kwenye maisha
yangu nikweli mlengwa hakuwa yeye lakini tayar
nimke wangu na nililijua hilo toka siku ya
kwanza namuoa na huyo mnaemuona nyie
kwamba ndio mke bora ni mchafu kuliko uchafu
wenyewe hiyo sura aliyonayo ni fake.
Na kama anabisha aseme haiwezekani hivi inawezekanaje kwa mwanamke mwenye akili zake timamu kumtamani mume wa dada yake ,kama alikuwa ananipenda kweli angalijitunza lakin alikuwa akibadilisha wanaume na kugawa tupu yake kama vile karanga za kuonjesha au unataka niseme machafu yako yote Nasra?"
"Selimmmmm hata siku moja usije kuthubutu
kuongea uchafu wa namna hiyo mbele yangu
unanielewa? Binti yangu nimemlea mimi
namjua vizuri hawezi kuwa na uchafu wa aina
hiyo"
aliongea baba kwa hasira sana sikatai lakin je kama ni msafi ikawaje akapata mimba tena ya dereva wako je una habari kuwa hata rafiki yako nae alikuwa akitoka na huyo binti yako mtukufu? Je unajua kwann aliachika na una uhakika ile mimba iliharibika ?"
"Selim nimesema kaa kimyaaa...kumbe Inauma kuona kipenzi chako akisemwa vibaya ee basi nikiwa kama Selim nasema Norah ndio
mke wangu mimi haijalishi anatabia mbaya
kiasi gani ila ndio wangu na atabaki kuwa
wangu,
na kama bado mnataka Nasra awe
mkwe kwenye familia hii mnaweza kwani vijana
wapo ila sio mimi" selim aliposema hivyo Jabir
nae akadakia "hata mimi simtaki"
Baba mkwe alichukia namna ambayo
ukimuangalia anatisha ila hasira zake
hazikubadilisha kitu Selim alinishika mkono
tukaingia chumbani tulipofika nilitaka kuongea
ila akanambia"Norah panga nguo tuondoke"
kama kuongea tutaongea mbele ya safari. "
Sikutaka kuwa mbishi nilipanga nguo nayeye
akaweka nguo zake kisha tukashika mabegi
yetu hadi sebleni,
baba mkwe aliinuka kamavile haamini naona alimwambia selim aondoke na kuacha kila kitu kwa lengo la kumtisha lakin kijana hajatishika..
Basi tulipofika seblen Selim aliweka kila kitu mezani yani funguo za gari sijui vitu vya ofisini na
Vingine vingi kisha akasema "niko tayar kuanza
upya hivi ni vitu vyako vyote asante na
kwakheri"
alinishika mkono akanambia
"twende mke wangu"
Nilimtizama sana Selim yani mpaka muda ule nilikuwa sielewi ni kwanini ananitetea kiasi kile na ilihali mimi nayeye wala hatujawahi hata kuonjana..
Je ni wapi wataelekea wawili hawa?. Na kwanini selim kagoma kumuacha Norah?? Je anampenda??
Endelea kufuatilia
Full ni 1000
WhatsApp 0742133100.