_______
SEHEMU YA 46
Nilicheka na kujifunika shuka ili nilale akaamka na kusema "Inamaana umegoma kuniambia?"
"Nikwambie nini wewe si umejifanya kununa "
"Sijanuna bwana sasa nitapata wapi nguvu ya kukununia mke wangu "
"Mh kwasababu ya umbea unaongea kwa mahaba yote eeh unaonesha hadi uhindi baba muone "
"Bwanee unaniambia au unanichosha maana naona unaringa kama kitu cha maana vile "
"nyoo eti kama kitu cha maana kingekuwa sio cha maana si ungelala bichwa hilo"
"Kwahiyo unanitukana ?"
" We boya kweli nimekutukana sangap embu lala ukue "
"Okay fresh nimekubali mi ni boya haya niambie basi mliongea nini"
"jamani selim kwani huo umbea umeanza lini mume wangu maana unanimbembeleza kama kitu cha muhimu sana "
hakunijibu akajifunika shuka nikamfunua na kumwambia "haya kaa vizuri nikwambie "
"Niache staki "
"Kwahiyo umejifanya kununa haya usiku mwema "
"We bwege nini unalalaje bila kuniambia "nilicheka na kumuambia kila kitu tulichoongea siku ile haikuishia hapo mpaka umbea wa chuo , akawa anajibu enhe π (nishamuharibu mtoto wawatu)
basi baada ya kumwambia na yeye akanipa ubuyu wake yani umbea kwenda mbele , story zilivyonoga tukaanza kumsema Nasra akasema yote waliyokuwa wanaongea basi tukamteta weee mpaka saa nane ni umbea tunaongea π.
Hii ni kawaida yetu jamani yani hatujawahi kukaa bila kupiga umbea na kuna mda naweza kuwa kazini akanipigia sm unafikili anaongea la maana kumbe anakupa umbea.
Basi tulilala kesho yake asubuhi tukaamka mapema na kusaidizana baadhi ya majukumu kisha tukapata chai na kuondoka na watoto hadi shule ,kisha akanipeleka mpaka chuo na yeye akaenda kazin kwake.
Siku hiyo nilikuwa na kipindi asubuhi na zilikuwa zimebaki dakika chache kipindi kianze , basi nikaingia moja kwa moja ,kufika nikamuangalia Amaira hakuwepo nikamtext akajibu yuko njiani basi nikakaa kusubiri kipindi kianze.
Haikuchukua mda kipindi kikaanza , kituko kinakuja mwalimu aliekuwa akitufundisha alikuwa kituko yani sijui kama alitoka nyumbani kwake akiwa kajiona vizuri au vp sijui maana alivyovaa kituko yani mtu unatumbo kubwa tena lile la uzazi shepu yenyewe kama yangu ee alafu unavaa gauni la mpira tena rangi mbili .
Basi nilivyona umbea nikasema nisicheke peke yangu acha nimcheshe na mchizi wangu Selim ,nilichokifanya nikampiga picha wakati akiandika na kumtumia Selim nikaandika Joker wakike.
Alikuwa online akafungua chap na kutuma emoji zakucheka kisha akaandika "Sasa mbona umempiga nyuma wakati inaonekana mbele unyama "
"Wewe nae hapo nimekupa kionjo picha kamili linakuja so mmbea mwenzangu subiri " niliweka sim pemben kisha nikatulia kwenye kipindi .
Baada ya kipindi kuisha tukatoka na kwenda kukaa kwenye mgahawa ili Amaira apate chai basi tukaanza umbea mara akaja kijana ameshika maua akatusalimia na kumpa Amaira yale maua.
Tukauliza yalikotoka akampoint huyo alieleta aloh nilikuwa nakunywa juice nilipaliwa nusu kufa , Amaira ndo akabaki eeeπ³, nyie kuna watu wanavituko basi tu iko hivi hayo maua yalitoka kwa mkaka mmoja hivi sitaki kumtaja jina kijana wawatu jamani alikuwa amevaa shati jekundu na suluali ya njano tena njano ile yakukolea huku chini sasa alikuwa na viatu vya kijani .
Hayo ni mavazi tu sijasema muonekano wake πnyie sitaki kukufuru uumbaji wa Mungu ila itoshe kusema kazi ya Mungu haina makosa .
Basi bwana Amaira akainuka mwenyewe na kunawa mikono kisha akachukia pen na karatasi akaandika "Asante ubarikiwe '" alivyomaliza akamkabidhi mkaka alieleta maua na kumwambia ampelekee huyu mr cheusi aka mr kachumbali .
Maana kuvaa shati jekundu tai kijani suruali njano hiyo ni nyanya, hoho, na karito yaani kachumbali tosha.
Basi alipopeleka hilo karatasi Amaira akabaki anaongea mwenyewe ooh sijui amenionaje mara hivi mara vile ,mimi mda huo nacheka sina mbavu, jamani sio kwamba nakufuru au vip hapana ila ukimuona huyo kaka utacheka ufe yani mbali na uvaaji wake nimtu mwenye muonekano wa kuchekesha .
Natamani ningewatumia picha yake mkamuona nahisi mngecheka zaidi yangu.
Mda wa chai ulivyoisha tukataka kuinuka si inabidi tulipe bill ,muhudumu si akatuambia tumeshalipiwa na huyo bwana kachumbali.
Kwakuwa ofa ni ofa tukaona fresh tu hela si yake kama ameona atumie kwetu acha tule ila ikifika kwenye malipo tutajuana visogo.
Siku iliisha jioni Selim akaja kunichukua na kurudi nyumbani ,tukiwa njiani akaniambia kuwa kuna rafiki zake wanaotoka nchi za nje wanakuja na anaomba wafikie nyumbani , sikuwa na shida maana nyumba ilikuwa kubwa.
Basi baada ya kukubaliana kuhusu wageni tukaongea swala la msichana wa kazi maana mda wote sikuwa nae na makubaliano yakapita takaona tuajiri mtu .
Basi tukafika nyumbani na kusaidizana kazi huku tukipiga umbea kama kawaida mara Jabir akaja na kukaa pembeni nakusema "Jamani leo nimekutana na kituko hicho " kusikia hivyo wote tukamgeukia kusikia hicho kituko alichoongea wote tukaachia sonyo na kutaka kumtimua .
Utani wa hapa na pale uliendelea mpaka tulipomaliza kila mmoja akapata chakula na kwenda kulala, kesho yake asubuhi ilikuwa jumamos niliamka nikafanya usafi kila sehemu kisha nikatoka kwenda kazin kwangu ( mara nyingi nilienda j moss ila j pili huwa siendi kwasababu ya kukaa na familia yangu) basi nilifanya kazi jioni tukafanya mahesabu pale kisha nikatoka na kwenda kununua vitu kwaajili ya wageni.
Baada ya kununua vitu nikarudi nyumbani na kuendelea na ratiba zingine, siku iliisha kesho yake nikaamka mapema na kuweka nyumba katika hali ya usafi
Nilimaliza kama kawaida tukakaa familia nzima jikoni kila mmoja akashika chake na kuwa bize kupika, hii ni kawaida jamani weekend huwa tunakaa wote jikon watoto wanapewa kazi ya kukata viungo baba mtu anapika mboga mimi juice Jabir anapika wali au vingine tofauti na mboga .
Tukimaliza kupika kinachofuata ni kula baada ya hapo mimi na watoto tunaosha vyombo na kweka jikoni sawa kisha kila mmoja anafanya mambo yake.
Kwahiyo na siku ya leo tulipika na kuandaa mezani tulipomaliza kila kitu wageni nao wakawa wamefika , nikiwa kama mama mwenye nyumba nikawakaribisha kwa heshima zote salamu na kautani kwa mbali vikapita kisha tukajongea mezani kupata chochote kitu.
Basi siku iliisha na kesho yake asubihi na mapema nikaenda chuo ( ila Selim hakutoka )
Sasa kwakuwa nilikuwa mwenyewe nikaona nimpitie Amaira ili tuongozane, nilifika kwake nikakuta kashajiandaa hivyo tukaondoka zetu.
Haikuchukua mda mrefu tuka fika bwana, kwakua siku hiyo nayo tulikuwa na kipindi asubihi tukapitiliza moja kwa moja darasani.
Mda wa chai haoo mgahawani ,sasa tukafika wenyewe na kukaa mara akaja yule bwana kachumbali leo alikuwa kavaa zake suruali nyekundu na shati la blue ya shule chini lapiga viatu vyake vya jana , basi akafika na kumsalimia Amaira kwa upendo .
Amaira nae hakutaka kuleta mambo mengi akajibu na mimi nikasalimia nikajibu hapo niko najifanya kuwa bize na sm ili nisicheke maana nikimuangalia jinsi anavyovaa nitacheka alafu ajisikie vibaya buree.
Basi bwana baada ya kujibu salamu kijana akaomba akae sisi ni nani tumzuie ,Amaira akasema kaa tu , sasa kusikia hivyo aliachia tabasamu kama vile kashinda kesi ya milasi π.
Mmh uvumilivu ukanishinda nikainuka taratibu na kwenda kuchekea pembeni ,nilipoona kicheko kimeisha nikarudi na kuanza kumsemesha" Mesha naona umeshazoea mazingira bwana "
"Hahaha ndio hivyo bwana sister nishazoea "
"Naona alafu inaonekana unapenda sana rangi za viungo"
"Yeah napenda sana siunajua viungo vinafanya mboga iwe tamu "
"Nikweli mboga kiungo na "kabla sijamalizia Amaira aliamka na kuondoka nikanuangalia bwana kachumbari nikatabasamu na kuinuka nikashika vitu vyangu huyoo mpaka alipoelekea Amaira nafikia tu anaanza kufoka .
"Hivi huyu Mesha ananitakia nini mimi ee ,kutwa kunifwata fwata mtu mwenyewe amekaa kama jokers kazi kunitia aibu "
"Eeeh dada si unapendwa wewe au "
"Kupendwa na huyo mpuuzi ? Alafu ngoja nitakuja kumchamba hata amini maana naona ninavyoongea nae kiupole ananiona fala" nilitaka kuongea akanishika mkono kwa nguvu huku akimuangalia mkaka mmoja hivi handsome wa chuo .
Nilikaa kimya nakubaki namuangalia tu ,yule kaka alivyosogea karibu akaniachia chap na kwenda kumsalimia , kwani alijibiwa π mkaka ananata kama Jojo.
Dada kikamshuka shuuuu π,nikasogea na kumpa kitambaa " unaweza kulia kama ukipenda " alinikata jicho hilo kisha akaondoka
Full 1000
Whatsapp 0657171961
KWETU morogoro.