Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

NIPE YOTE DADY 58~59

10th Aug, 2025 Views 86



Nililia pale chini akaniaga nakuondoka kwa maringo, nilimchukia Selim kuliko kawaida yani nikheri angeniacha kipindi kile kuliko kuja kuniacha saizi .

Nilikaa pale nje kwa mda mrefu mpaka Jabir alivyorudi maana wakati ananifikisha nyumbani aliingia ndani na kutoka , alisimamisha gari na kuja kuniuliza shida nini mbona niko nje tena nalia .

Sikumjibu nikampa talaka niliyokuwa nimeishika mkononi ,aliiangalia kawa kama hajaelewa na kuniuliza maswali lakin bado nilikaa kimya .

Alivyoona siongei akainuka na kuingia ndani nikawa nasikia akigomba kwa ukali , hakuchukua mda akarudi nje na kutaka kunichukua ili aniriudishe ndani niligoma na kuinuka nikawa naondoka ila akanizuia sikutaka kumsikiliza nikawa nimeondoka kwa hasira .

Nilirudi nyumbani na kumkuta baba akisoma gazeti alivyoniona akainuka haraka na kuja kuniuliza nini shida maana nilifika na kukaa kama mzigo kwanza hata nguo sikubeba niliziacha pale pale nje.

Basi baba aliuliza shida nini nae nikampa talaka ,alisoma zote na kuuliza na kuniuliza "umefanya nini mpaka Selim akachukua hatua hii" nilimuangalia na kujibu.

"Sijafanya kitu ila amemchagua mwanao badala yangu"

"Unamaana gani kusema hivyo"

"Baba Selim kaniacha kwasababu ya Nasra ametembea na dada yangu nabado akaniadhibu kwakubiacha " baba aliinuka haraka bila hata kuongea kitu akatoka nje na kupishana na mama mlangoni na kumuacha akishangaa.
Baba alienda kwa Selim akafika na kurusha zile talaka na kuuliza "Hiki ni kitu gani kwann umefanya hivi?"

"Mzee nimefanya hivi kwasababu hiyo ndio njia sahihi na salama kwangu na wanangu"

"Nenda kwenye point nikitu gani amefanya hadi kumuacha ghafla namna hii tena kwa talaka tatu"

"Nimemuacha kwasababu hana sifa zakuwa mke wangu na sio mimi tu bali kwa manaume yoyote yule hafai kuwa nae kama mke "

"Selimmm unathubutuje kuongea kauli kali namna hiyo ?"

" Mzee huu ndio ukweli lakin simshangai au kumalaumu maana nimtaka mwenyewe ,so kwasababu nimeshindwa sina budi kumuacha dunia imfunze maana hata kwa wazazi alishashindikana ."

Baba alichukizwa na kauliza Selim akajikuta akimpiga kibao cha nguvu na kumpa onyo juu ya kauli zake ,sasa wakati yanaendelea hayo yote Nasra alikuwa chumbani na mama mkwe wakijipongeza kwa ushindi walioupata mara wakasikia kelele za mabishano baina ya baba na Selim ikabidi maka mkwe atoke Nasra akabaki ndani.

alitoka tu na kukuta kofi likitua kwenye shavu la kijana wake kitu ambacho kilimkwaza na kuanza kuongea kwa hasira, sasa katika maneno yake akasema kuwa mimi ni malaya nilikuwa silali nyumbani , baba hakuelewa wala kuamini akaondoka nakurudi nyumbani ikabidi sasa kaka zangu wakenda tena kwa Selim mda wote huo Nasra kajificha chumbani maana alijua akitoka itakuwa vita haswa .

Basi kaka zangu walienda mpaka kwa Selim na kutaka kuongea kwa utulivu , haikuwa rahisi Selim kukubali ila mwisho alikubali na kukaa kuongea na ndipo aliposema sababu iliyomfanya achukue maamzi ya kuniacha .

Sababu yenyewe ilikuwa kuwa nimemsaliti kwakutoka nje ya ndoa na ushahidi alikuwa nao ,kaka zangu baada ya kuona huo ushahidi hawakuongea wakaomba samahani na kurudi nyumbani.

Nikiwa nimekaa chumbani alikuja kaka yangu wa kwanza na kuniweka kofi alooh naweza kusema toka nimezaliwa sikuwahi kupigwa kofi zito namna hii.

yani kofi moja hadi nilitokwa na damu puani sasa mama akawaka kwann anipige si ndio akaongea kilichotokea mama akanigeukia na kuniweka kofi lingine aisee siku ile ilikuwa mbaya kuliko siku zote .

Nikikataa na kujitetea kwamba sijawahi hata siku moja kumsaliti mume wangu ila hakuna alienielewa nikabaki kuonekana muongo na mzinzi, baba alichukua uamzi mzito na kunitimua kama mwizi tena akasema nisikanyage nyumbani tena .

Nilitoka pale na kwenda kwa Amaira akanipokea vizur hapo ni usiku wa saa nne kutokana hali niliyokuwa nayo hakuweza kuniuliza maswali zaidi alinipa chumba nikalala .

Kesho yake asubuhi nikiwa bado sijatoka kitandani nikasikia sauti ya Jabir kwa mbali ikabidi niamke na kutoka hadi seblen kweli alikuwa yeye pamoja na aunt Suna .

Aunt alinifuata na kunikumbatia akanipa pole pale kisha akaniambia nimueleze ukweli bila kuficha nikamueleza kila kitu .

Alikaa kimya kwa mda kisha akasema "Norah huu ni mchezo umechezwa naamini Selim hawezi kufanya vitu kama hivi alafu na kwann akutuhumu kutoka nje ya ndoa je kuna mtu yoyote uliewahi kuwa na mazoea nae sana labda akakukanya ila hukusikia?"

"Aunt mimi sijawahi kutoka nje ya ndoa yangu hata siku moja na kuhusu kuwa na mazoea na watu wengine hamna sijawahi kabisa ila sijui kwann ameamua kunifanyia hivi , sawa tuseme aliona simfai tena si angeongeza mke wapili tu au hata angechikua mtu yoyote ila sio dada yangu, namchukia sana Selim wala sitokaa nikamsamehe"

Aunt alinituliza na kuendelea kukataa kuwa Selim aliemlea katika mikono yake hawezi kufanya kitu kama kile , ukweli sikuelewa wala kutaka kusikia kwasababu niliamini kweli amefanya vile na kila nikikumbuka matendo yake napata kuamini kuwa ni kweli ametoka na Nasra.

Jabir aliniahidi kupambana kadr ya uwezo wake kuturudisha pamoja tena , nilimwambia asijisumbue maana haiwezekani .

Mawazo yakitawala akili yangu maumivu yakaufunika moyo wangu nikawa hata kula nakula kwa kulazimishwa nikweli nilikuwa nakosea kama binadamu ila pamoja na makosa yangu sikustahili lile ,upendo uligeuka chuki nilimchukia Selim kuliko kawaida simimi tu hata yeye alinichukua kiasi chakuzuia nisiwaone watoto.
Nasra nae alikuwa proud Kwakile alichofanya na kwakuwa alitaka kupata antension ya Selim akajifanya anataka kuondoka akidai hawezi kuendelea kuwepo wakati mm sipo Selim akakataa na kumwambia akae .

Ilipita wiki siku hiyo nikavaa vizuri na kumfuata Selim ofisin ,kwakuwa walikuwa wakinifahamu nikaruhusiwa kuingia moja kwa moja .

Nilifika na kukaa kwenye kiti kisha nikasema .............
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY 58~59  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-58-59
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest