Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

NIPE YOTE DADY๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž SEHEMU YA 16~17

19th Jul, 2025 Views 38

NIPE YOTE DADY๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž

SEHEMU YA 16~17
Baba yangu alitoa amri kuwa nijiandae tuondoke alichukizwa sana na lile tukio Selim alivosikia habari za kuondoka alichanganyikiwa..

Ikabidi aanze kuomba msamaha ila baba alikuwa
kakasirika mno hakutaka hata kumuona selim mbele yake๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐ

Kila mtu ilibidi aanze kujieleza kule ndani baada ya mama Selim kujieleza na baba kutokuelewa baba Selim na Selim waliungana na kumuomba baba msamaha walimbembeleza mwisho akakubali.

Alitoa onyo kwa selim na kumwambia iwe mwisho kuninyanyulia mkono kama ndoa imeshindikana anirudishe nyumbani sio kunipiga..

Baada ya hapo baba hakutaka maongezi mengine aliondoka bila hata kusema ni kipi kilichomleta katika ile familia hakika alichukizwa sana..

Baada ya baba kuondoka kesi ikabaki kwa Selim na
mama yake aisee Baba selim aliongea kamavile
hatoongea tena selim alifokewa kama mtoto ugomvi ulikuwa mkubwa mpaka mzee akasusa kula na kuondoka..

Selim alivoona baba yake kaondoka nae akasusa akasepa Mama yake nae akaunga,mimi na aunt tulikaa mezani tukala nilipomaliza niliinuka haraka na kwenda chumbani..

nilipofika huko nilimkuta selim kajilaza kwenye kochi kama kawaida yake..nilipanda kitandani nikajifunika kisha nikaanza kulia๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญnililia mno hiyo siku๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

Nililia hadi kwi kwi selim uvumilivu ulimshinda aliamka na kuja kitandani akalala na
kunishika mgongoni kisha akaniambia "

"nisamehe nilikuwa na hasira sana wala
sikukusudia kukupiga " sikutaka kuongea chochote aliomba msamaha hadi akachoka na kulala pale pale pembeni yangu๐Ÿ™ˆ..

Nyiee๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆet akanikumbatia kabisa na kunisogelea zero distance ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆbasi namimi nikatulia tuli๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆtukalala mpaka asubuhi

Kulipokucha tu mimi ndo nilikuwa wa kwanza kuamka nikakimbilia bafuni๐Ÿ˜๐Ÿ˜nilifungulia maji kisha nikakaa pembeni nikawa nawaza usiku mzima selim alivolala pembeni yangu๐Ÿ˜Œ๐Ÿ˜Œ

Basi mawazo yalienda mbali nikasahau kabisa habari za kuoga๐Ÿ˜๐Ÿ˜lisaa lizima lilikata maji yanamwagika tu mimi niko pembeni..

Selim aliendelea kulala akawa anasubiri nitoke bafuni akashangaa mbona sitoki lisaa la pili lilikuwa linaenda kuisha๐Ÿ˜Œ๐Ÿ˜Œilibidi aje kunigongea kwani nilisikia?. Nilikuwa nawaza vitu vingi kiasi kwamba hata ukisimama mbele ya macho yangu naweza nikakwangalia lakini nisikuone๐Ÿ˜

Selim aliita weee akachoka akaamua kusukuma mlango na kuingia kule bafuni huku akiwa na presha za kufa mtu..sijui alijua nimejiua??

Aliingia akanikuta niko zangu pembeni tu nawaza hata kuoga sijaoga๐Ÿ˜Œ๐Ÿ˜Œalinisogelea akanigusa begani akaniuliza shida nini??

Wala sikumjibu nilianza tena kulia๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญakakazana kunibembeleza huku akiomba msamaha nikamwambia "Selim nimechoka na haya maisha natamani tu unirudishe kwetu๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

please naomba tu uniache niende kwetu" masikini alinikumbatia๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆakawa anashindwa hata cha kuongea ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆaliniangalia kwa muda akaniambia "Noraha naelewa kwamba hunipendi ila tambua familia zetu ndo zilitaka hivi sisi hatuna budi Norah naomba tu ubaki namimi please.."

"Selim siwezi mimi nimechoka siwezi kuendelea kubaki hapa๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญhunipendi mama yako hanipendi ndo maana mnashirikiana kunipga mtakuja kuni ua siku moja๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ"

Nisamehe Norah najua unaongea hivi kwasababu nilikupga jana please niambie nifanye nini ili unisamehe๐Ÿฅน๐Ÿฅน

"Nataka uniache niende mbali nawewe ukifanya hivo kweli nitakusamehe๐Ÿฅน๐Ÿฅนselim alipiga goti akaniambia No siwezi kukuacha Norah siwezi"

"kwann?" aliniangalia kwa mda kisha akataka
kujibu akasita baada ya kusikia sauti ya baba
yake ikimuita aliniinua tukatoka mle bafuni
akaniacha chumbani na kwenda kumsikiliza baba yake...

Alitaka kuniambia kitu gani?. Alafu mbona hataki kuniacha niondoke?? Au selim ananipenda???Nilibaki nikijiuliza maswali mimi mwenyewe๐Ÿ˜‘

Selim na baba yake sijui waliongea nini ila Selim alirudi chumbani akiwa amepoa sana nikaona nimuache nisimletee drama nitaendelea kumuumiza๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐ

Basi aliingia bafuni na kwenda kuoga alimaliza akatoka nikamfuata nikamuuliza unataka
kula nini nikakuletee akanambia kuwa hataki
kitu nilimhurumia maana usiku wa jana alilala njaa nilimwambia please niambie unachojisikia kula..

Alibaki ananiangalia tu๐Ÿ™„๐Ÿ™„nilimpapasa usoni kidogo nikamwambia basi acha mi nikakuletee chochote..nilitoka mpaka jikoni nikaandaa chakula cha selim kisha nikampelekea chumbani..

Alikula akamaliza akaniambia asante Norah..siku hiyo selim hakutoka kwenda sehemu yoyote
zaidi alikuwa chumbani tu na kazi zake alizifanyia
nyumbani..

Zilipita wiki mbili tukiwa na amani selim alibadilika sana namimi nikakaa kama mke mwema sikutaka kuleta fujo wala drama zozote..

Siku moja mchana tulikuwa wote chumbani mimi na Selim..Selim alianza kulalamika njaa nikamuuliza unajisikia kula nini nikakupikie?.

Bado mimi na Selim tulikuwa hatujaanza kuishi kama wanandoa lakini amani ilikuwepo tulikuwa na masikilizano ya amani sana..

Selim aliniambia chakula anachotamani kula nikatoka mpaka jikoni nikaenda kuandaa nilipika vizuri wakati napakua kwenye hotpot mara mama mkwe akaja pale jikoni..

Ni harufu ya nini hiyo aliuliza akiwa ameshika kiuno alisogea na kuangalia akaniuliza..
"umepika nini hiki"
Nikamjibu kuwa nimepika lost ya maini na wali
wamaua...

Kabla hata sijamaliza kujibu nikashangaa mama anakimwaga kile chakula chote๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณaiseee nilipatwa na hasira mpaka nikawa natetemeka..Ivi mnajua kwa hiko kipindi mimi na Selim ni kama tulishaanza kupendana fulani hivi..

Hata hiko chakula my wenu nilijipinda kukipika vizuri ili nimfrahishe selim sasa why mama akimwage chakula changu lakini๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

Nilimuuliza "mama unamaana gani kumwaga
chakula hiki chakula nimempikia mme wangu"
"Mama aliniambia nilikwambia hii sio nyumba ya baba yako kwamba unajiamlia tu nini ufanye nini upike hapa sio kwenu๐Ÿ˜จ๐Ÿ˜จ"

"Kama ni chakula ulitakiwa ufuate ratiba ya leo inasema nini ratiba inasema tambi nyama wewe unaenda kupika huu ujinga wako nani alokupa ruhusa?"
"Lakini mama mimi nimepika cha mume wangu tu na mwanao ndio kaniomba nimpikie hivo lakini kwanini umenifanyia hivi mama๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ"

"mwanangu tangu lini akala maini toka nimemzaa selim amekuwa akiyachukia maini
inakuwaje leo akutume umpikie?.."
"swala la kutokula maini silijui ila mimi
nimefanya kama alivyotaka basi๐Ÿฅน๐Ÿฅน"

"Nasra nakujua vizuri na ninajua ni namna
gani mama yako kawalea vibaya acha tu leo kwambie Nasra hutakaa uishi kwaamani kwenye hii nyumba lbda niwe nimekufa"

Aisee Mama selim aliamua kunionyesha wazi ni kwa namna gani anavonichukia๐Ÿ’”๐Ÿ’”niliishiwa nguvu๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญhata kale kaupendo nilikoanza kuwa nako moyoni juu ya selim nilikaondoa..

Niliona kabisa kwenye hii nyumba sitokaa nikubalike bora niishi tu kama Norah na niwe tyr kuondoka hapa muda na wakati wowote..

Baada ya yote hayo nilianza kupiga hatua mdogo mdogo nikawa naondoka kule jikoni๐Ÿ’”๐Ÿ’”moyo wangu ulikuwa umegawanyika vipande sielewi nini nachotakiwa kukifanya...

Wakati naondoka mama alinistopisha na
kusema "Unaenda wapi rudi hapa upike "Dah nyieee sikutaka ubishi nikarudi na kumuuliza "sawa mama unataka nipike chakula gani "

"kwani haujui kusoma " nilijibu sawa kisha
nikatoa nyama kwenye friji nikakaa kusubiri
iyeyuke ili nianze kupika wakati nasubiri mama aliniita akanambia " kuna
nguo zimeanikwa nje nenda kazianue na
uzikunje "

"nilimuangalia na kumuuliza "zile
nguo walizofua wadada wakazi " alijibu ndio
nikasema sawa na kutoka nje nikaanua za
Asma wifi yangu na zakwake za baba mkwe nikaziacha"

alafu nikamwambia msichana azianue maana
niliona sio sawa mimi kushika nguo za baba
mkwe wangu wakati mke wake yupo.

Sasa kitendo cha mama kumuona msichana
akipeleka nguo za baba chumbani kwao ikawa kosa kwann aniambie mimi kitu alafu mimi
nimwambie mtu mwingine.

Alinifuata na kuanza kunitukana nilimuuliza swali moja tu "je nisawa mimi kuanua nguo za baba mkwe wangu na kupeleka chumbani kwenu ikiwa upo na hauumwi?"

Mama alichukia akaanza kufoka kwamba
namfundisha namna ya kuishi kwenye nyumba
yake nikaona anatafuta ugomvi wa lazima nikamucha na kuingia jikon na kuanza kupika.

Alisubiri nimemaliza kupika akaja kufunua vyakula
akasema baba hali vyakula vyenye sukari wala
hatumii nyama nyekundu sasa nikamuuliza
nimekuuliza mnapika nini umeniambia nisome kwenye ratiba๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ

nimesoma ratiba nakupika sawa sawa na maelezo yaliyopo kwenye ratiba alafu saizi unakuja kusema sijui mumeo hatumii nyama nyekundu mimi ningeota??

kama sukari mbona anakunywa kwenye chai
kila siku asubuhi nyiee yalizuka mabishano pale jikoni๐Ÿฅน๐Ÿฅนmama akaniamuru nitoe kuku nipike haraka kabla baba hajarudi..

Nilijifikiria sana nikasema inafu is inafu hivi kwenye hii nyumba ninafanya nini?? Hakuna ninachofaidika nacho kwenye hii nyumba zaidi ya manyanyaso..

Niliamua kuacha kila kitu nikatoka kule jikoni mama alinizuia na kuniambia ni lazima nifanye anachotaka nifanye...

nilimwangalia nikamuuliza mama hivi ukiniangalia unaona ni kama ninaweza kuvumilia hivi vitimbwi vyako..???au kwasababu unaona nakuwa mpole basi unanichukulia kama mjinga?..

sasa sikia nikwambie kitu sipiki chochote yule
ni mume wako wewe ingia jikon pika vile
anavyopenda"

Baada ya kumwambia hivo mama nilishituliwa na bonge moja la kofi๐Ÿฅน๐Ÿฅนsikutaka hata
kumcheleweshea aisee tulianza kuzichapa kule kule jikoni๐Ÿ˜Œ๐Ÿ˜Œ

Nilimpiga yule mama hatokaa anisahau๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅna siku hiyo watu ni kama walizibwa masikio huko vyumbani kwao hakuna aliesikia hata kelele za ugomvi..

Nilimkalia chini nikawa nampa kipigo huku namziba mdomo kelele zisitoke nje๐Ÿ˜ฉ๐Ÿ˜ฉyani nilimpa kipondo cha mwanaukome nilivochoka nikamwachia akatoka mimi nikabaki jikoni..

Nilijua tu atakachokifanya ni kwenda kuwaelezea watu kilichotokea sasa kabla ya yote nilipakua kwanza chakula nikala ili wakija kunirudisha kwetu nirudishwe nikiwa nimeshiba..

Nilijua kabisa ule ndo mwisho wangu na selim na ule ndo mwisho wangu kwenye ile nyumba..

Je itakuwaje?? Ni kweli ndoa ya vipenzi vyetu ndo itaishia hapo?. Selim ataamua nini?.

Full 1000

WhatsApp 0742133100.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž๐Ÿ’ž SEHEMU YA 16~17  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-sehemu-ya-16-17
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest