Nilimgeukia Selim na kumwambia "mh nipe umbea kimetokea nn?"
"Na ukaniamini kuwa nina umbea"
"Selim umeanza sema bwana "
"Niseme nini wakati nimeshinda ndani umbea ningeutoa wapi"
"Kwahiyo ulivyokuwa unaniambia unaumbea ?'"
"Nilitaka tupate dhambi wote ,we unaweza kwenda motoni peke yako?"
"Bata wewe"
" Paka wewe" tulikaa seblen kwa mda mrefu kisha tukaingia chumbani na kulala ,kesho yake niliamka mapema na kwenda jikon nikaanda chai kisha nikaweka mezani .
Mara mlango ukagongwa nikaenda kufungua nashangaa Nasra ,nilimuangalia juu chini na kumuuliza "Kuna msiba Au mbona asubuhi asubuhi "
Alijichekesha nakujibu "hamna kila kitu kiko sawa ila nimekuja kukusalimia tu"
"Kwanzia lini ukadamkia kwangu kama kijumbe unaenidai?"
"Jamani wewe si ndugu yangu ,anyway nimehamia nyumba jirani so tutakuwa majirani kwanzia sasa " nilishangaa kusikia kahamia nyumba jirani inamaana amepanga au nini"Una maanisha nini kusema umehamia nyumba yapili?"
"Nimepanga nyumba hiyo inayopakana na yako "
"Oooh kwahiyo umetafuta nyumba huko mtaani kwenu ukakosa " kabla hajajibu Selim aliniita na kuniuliza naongea na nani ,nilimjibu na kundelea kuongea na Nasra.
"Mh bi dada asante kwa taarifa nafikili unaweza kuendelea na zoezi lakujitambulisha kwa majirani wengine "
"Aaam hapana nitarudi nyumbani tu maana saizi bado mapema sana kuwagongea watu sio vizuri "
"Kwahiyo sisi ni mbuzi?"
"No sina maana hiyo bwana ,alafu nilikuwa naomba watoto waje nyumbani ili wacheze na Salum"
"Nasra wanangu hawatoki kwenda kokote na naona hicho ndio kimekuleta mpaka huku "
"Oooh sawa samahani pia" aliongea akageuka na kuondoka nikaFunga mlango na kutaka kuondoka nikakuta Selim amesimama huku kakunja mikono huku uso wake ukionesha kukasirika ,nilisogea na kuongea " we vip mbona umenivimbishia sula ?"
"Kwann unafanya hivyo?"
"Nafanya nini tena ?"
"We huoni unachokifanya ?" Niliona huyu analake nikataka kumpita alinishika mkono na kunirudisha "Selim vip bwana "
"Niko serious kwann unafanya hivyo?"
"Unajua unanichosha kama kuna kitu unataka kuongea siuongee tu kuliko kuulizana maswali asubuhi yote hii"
"Kwann unamtendea ubaya ndugu yako "
"Embu niachie kwanza , kuvimba kote kumbe hilo tu "
"Norah niko serious kwann ?"
"Hivi unajua maana ya ubaya au bado una hangover "
Aliniangalia kwa hasira na kunivuta mpaka chumbani hapo nikajua kweli amechukia .
Basi tulifika chumbani akaniachia na kusema "Haya niambie kabla hatujagombana"
"We naona huo ugomvi unau download ,haya minilikuwa naongea na Nasra sasa sijui ubaya gani unaozungumzia"
"Norah hii sio sawa Nasra nindugu yako hupaswi kuongea nae namna ile hata kama aliwahi kukukosea ila yameshapita kwann hutaki kuacha hayo mambo na ukaishi upya , mtu anajitahidi kila siku kukuonesha kuwa anajutia alichofanya na anaonesha upendo kwa ndugu zako ila bado umeshikilia bango "
"Selim haya mambo ni yangu na Nasra kingine sina kinyongo nae ila sitaki mazoea na yeye basi"
"Norah wewe ni mke wangu nakufahamu kuliko unavyofikilia , najua unakataa kuwa karibu nae ukihofia labda atafanya chochote cha tofauti .
"Hivi unajua najisikiaje ? Naona kama hauniamini wala hunioni kama mwanume .
Kwasababu kama ungekuwa unaniamini usingekuwa unafanya yote hayo"
'"Selim hapana nakuamini sana na wewe unafahamu hilo ila kuhusu Nasra ukweli moyo wangu haumuamini tena na sijisikii vizuri pale ninapokuwa karibu nae"
"Kwasababu unahisi anaweza kunichukua si ndio na ukiniangalia ninaonekana kama mwanaume anaeweza kutoka na shemeji yake ?"
"Selim"
"Hapana hii ndio maana yake Norah nakupenda mke wangu na siwezi kufanya ujinga kama huo ,inaniumiza kuona unashindwa kuelewana vizuri na ndugu yako Kwasababu yangu .
Tafadhali embu acha hii kitu basi ,yule ni ndugu yako mmezaliwa tumbo moja siku moja ,jaribu kuthamini hilo basi" aliongea sana mwisho nikaona kweli nakosea .
Basi nikamuomba msamaha na kumuahidi kuwa nitaongea na Nasra vizuri, baada ya maongezi kadhaa nilifanya shughuli chache kisha tukapata chai .
Mchana nilienda kwa Nasra na kumwambia nimemsamehe ,alifurahi mpaka akalia .
Nilimtuliza kisha tukakaa kupiga story ila moyoni sikuwa na amani nae kabisa yani nilifanya vile ili tu kuweka maelewano na mume wangu basi.
Kwanzia siku hiyo tukawa tukitembelea ila sikutaka wanangu waende peke yake.
Wazazi walifurahi kuona watoto wao tunaelewana tena , ilipita miezi miwili baba mkwe akaanza kuumwa tulianza kuhangaika kumpeleka hospital ila hali yake haikurudi kawaida mwisho mapenzi ya Mungu hutimia akamtwaa mja wake.
Ilikuwa pigo kwenye familia hata marafiki ila ndio safari ya kila mmoja wetu tu mavumbi na mavumbini tutalejea.
KWETU morogoro.