Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

PAKA WA MAMA KIZIBO. SEHEMU YA KWANZA

24th Aug, 2025 Views 16

.

Kunako majira ya saa tano na nusu za usiku wakati kijana Bakari Msukanondo anajiandaa kwenda chumbani kulala simu yake iliita. Alipoiangalia akakuta inapigwa na bosi wake mkurugenzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya karanga bwana Arsenal Patel

Haikuwa kawaida ya bosi huyu kumpigia simu baada ya saa za kazi; hivyo moyo ulimdunda Bakari na kuhisi kuwa lazima simu hiyo itakuwa na walakini.

Huku mikono ikimtetemeka Bakari aliinua simu na kuipokea. " Haloo Boss shikamoo"

"Marahaba. Samahani kwa kukustua usiku. Nilichotaka kukufahamisha ni kuwa Mkurugenzi wetu wa Bodi atasafiri Jumatatu kwa ndege ya saa sita mchana kwenda Uturuki hivyo hakikisha unayaandaa yale maboksi yake. Ataondoka nayo. Sawa ?" Bwana Pater Alimaliza ujumbe wake na kukata simu kabla hata Bakari hajasema kitu.

Kijana Bakari baada ya kupokea simu hiyo alijikuta karudi sebureni na kukaa kwenye kochi.

Hakuwa na shaka yoyote juu ya maelekezo aliyopewa ila kilichomshangaza ni kwanini kaambiwa siku ya Ijumaa kuandaa kitu cha kusafiri Jumatatu mchana. Kama ni kuandaa maboksi angeweza kuambiwa hata Jumatatu asubuhi. Akashangaa imekuwaje aambiwe usiku ule.

Taarifa hii ilimnyima usingizi Bakari. Kila alivyozidi kuwaza ndivyo hofu ilivyokuwa ikimzidi. Usiku huo hakulala kabisa; na alfajiri na mapema ya siku ya Jumamosi alikuwa wa kwanza kuingia kiwandani hadi walinzi wakamshangaa.

Baada ya kutia saini kitabu cha mahudhurio alipitiliza moja kwa moja hadi stoo.

Kama anayekimbizwa Alitoa ufunguo na kufungua mlango wa chuma wa stoo. Alipoingia akaenda moja kwa moja kwenye kabati la kwanza ambamo ndimo alimokuwa ameyaweka Makasha hayo akafungua kuangalia; hakukuwemo na boksi hata moja.

Kama mwehu akafungua kabati lililofuata; hakukuta maboksi. Akaendelea hadi kabati la kumi na mbili; mote humo hakukuwepo na maboksi aliyokuwa kapewa kuyahifadhi.

Bakari hakuamini anachokiona. Akarudia upekuzi mara sita. Hatimae akili ikamrudia na kukubaliana na ukweli kuwa yale maboksi ya mwenyekiti wa Bodi yalikuwa yametoweka.

Kijasho chembamba kilianza kumturirika bwana Bakari. Kijasho kilimtoka kwa sababu nyingi. Kwanza, yeye, Mwanamtama na Bosi Patel ndio waliokuwa wakijua uwepo wa maboksi yale. Pili, yeye peke yake ndiye aliyekuwa na ufunguo wa stoo. Tatu, mlango wa stoo haukuwa umevunjwa. Nne, maboksi hayo yalikuwa yameletwa wiki tatu zilizopita na yeye toka alipokabidhiwa kuyaweka hakuwahi kuyakagua kama yapo au la hivyo haieleweki yalitoweka lini. Tano, hakuwa anajua yana nini ndani na yana thamani gani. Sita, maboksi yalikuwa mali ya Mwenyekiti wa Bodi ambaye neno lake moja anakuwa kapoteza kazi na pengine akaenda jela.

Taratibu alitoka nje na kufunga mlango wa stoo akaenda kwenye ofisi yake na kujitupa kwenye kiti akiwa hoi bin taabani.

Kwa karibu dakika kadhaa ubongo wa bwana Bakari ulivurugika. Alikuja kuzinduliwa na Mwanamtama dada mmoja Afisa Manunuzi ambaye alikuwa na ofisi jirani na yake.

"Vipi kaka yangu una homa; nakuona macho mekundu na umelowa jasho ?" Mwanamtama alimwuliza Bakari huku akimtazama kwa huruma na mashaka.

"Hapana Dada. Nimechanganyikiwa kwa sababu nimekwenda stoo kukagua nimekuta yale maboksi matatu ya Mwenyekiti wa Bodi hayapo. Na mbaya zaidi anahitaji asafiri nayo Jumatatu. Kwa hivi unavyoniona mbili haikai wala moja haikai." Ilibidi Bakari amweleze ukweli Mwanamtama ambaye urafiki wao ulikuwa kama undugu.

Mwanamtama kusikia habari hiyo akaruka kwa mshangao. " ....ina maana huyo mwizi kaingia kuchukua hayo maboksi tu; alijuaje kuwa yamewekwa stoo......au kuna mtu ulimwambia ?"

" Hapana Dada yangu. Tunaojua habari hiyo ni mimi, wewe na Bwana Patel " Bakari alieleza kwa uchungu huku machozi yakimlengalenga.

TUMEONA HILO TUKIO LA MABOKSI YA MWENYEKITI WA BODI YAMETOWEKA STOO WAKATI YANATAKIWA YASAFIRI NA MWENYENAYO KWENDA UTURUKI. UNGANA NAMI KATIKA SEHEMU YA PILI UJUE BWANA BAKARI ATAFIKWA NA NINI KUFUATIA UPOTEVU HUO..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

PAKA WA MAMA KIZIBO. SEHEMU YA KWANZA  >>> https://gonga94.com/semajambo/paka-wa-mama-kizibo-sehemu-ya-kwanza

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest