Mwanzo….
Ni katika vita kali vinavyopigana majira ya usiku kati ya wanajeshi na waasi .
Wanajeshi wengi wanapoteza maisha katika vita hiyo, James ambaye ni captain wa jeshi anawaambia wenzake sita walio salia wakimbie sababu tayari walikuwa wamezidiwa nguvu na waasi .
“ Kiongozi tukimbie wote, hatuwezi kukuacha hapa pekeyako ….” Wanajeshi walikuwa wakimwita James kwa sauti ya juu lakini james anaamua kubaki kupambana peke yake .
“Hii ni amri kutokakwa mimi captain wenu kimbieni , kumbukeni familia zenu zinawahitaji msihofu kuhusu mimi “ aliongea James kwa sauti ya juu akiwa anaendelea kufyatua risasi .
Wenzake sita waliobaki wanaanza kukimbia.
James anaendelea kupambana na waasi akiwa peke yake amejibana nyuma ya
Mti .
Taratibu waasi wanaanza kumshinda nguvu james na kuanza kusogea katika ule mti aliojibana .
Kuna kumbukumbu mbaya inamjia James akiwa yupo kwenye ule mti .
Baada ya kumbukumbu hizoJames akajitokeza kwa hasira akiwa na mitutu miwili kwenye mikono yake na kuanza kumimina risasi kama kichaa .
“Haaaaaaaaaaaaa……” James alipiga kelele kwa hasira akiwa anawashambilia waasi akisuri tu umauti umfike maana waasi walikuwa ni wengi zaidi na zaidi.
Mitutu ya James aliyokuwa ameishika katika mikono yake miwili inabaki kutoa sauti tu badala ya risasi.james anaharuki na kugundua risasi zilizokuwa ndani ya silaha zake zimeisha
Waasi wengi alikuwa tayari amewaangusha lakini waliobaki ni wengi zaidi ya waliokufa .
Hapohapo waasi wanamzunguka james wakiwa na siraha kubwa ambazo zote zilielekezwa katika kichwa cha james ikisubiriwa amri ya kiongozi wafyatue risasi.
James anamtazama kiongozi kwa macho ya hasira sana akiwa katikati ya waasi .
Kiongozi anatoa amri kwa sauti kali “ uwaaaaaaaa” ghafla sauti nyingine ya kike inasikika nyuma yao.
“Subirini …” Ilikuwa ni sauti nyororo sana iliyowafanya waasi wote wageuke kutazama ni nani?
INAENDELEA……
Mambo ni moto
Je, james atapona mbele ya waasi ?
Mwanamke huyo ni nani?
Kumbukumbu gani mbaya zilizomjia james na kumpa hasira ?
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments
EPISODE 1