Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SALMA WA MTAA WA SABA FINALY SEHEMU YA ISHIRINI*

22nd Aug, 2025 Views 139


Baada ya kuachana pale hotelini Maya hakuacha kumsumbua Fariss mara kwa mara alikuwa akimpigia simu na kulalamika kuwa anamfanya apitie kipindi kigumu moyo wake bado ulikuwa inamuhitaji na hakuwa tayari kumuona anakuwa na mwanamke mwingine zaidi yake.

Siku moja Fariss na Meyael walikuwa wakiandaa kwaajili ya harusi maana zilibaki siku tatu tu. Waki wanakaribisha nguo zao za harusi Fariss alimwambia Meyael kinachomsibu.
" Meya unajua Maya wanasumbua sana na amesema yupo tayari kufanya chochote bili kuharibu ndoa yangu na Salma.
" Fariss wewe ni mkubwa sasa na una maamuzi sidhani kama kuna mtu anaweza kutoka huko na kukutoa kwenye lengo lako . Baki kwenye msimamo mmoja ukiyumba utapoteza kila kitu.
" Ni kweli sasa nifanye nini kuhusu Maya maana Salma akijua inaweza kuniletea shida.
" Acha ndoa ipite baada ya hapo utamueleza Salma kila kitu kuhusu usumbufu wa Maya na kama ukishindwa niambie mimi niongee nae maana Salma ni shemeji yangu wa nguvu mwenyewe namkubali malkia wa mtaa wa saba alieweza kukutuliza na kukunyima usingizi.
Fariss hakuwa na alisema zaidi ya kutabasamu tu

Hatimae siku zilienda harusi ilifungwa mtaa wa saba nyumbani kwa kina Salma . Kama kawaida muoshwa huoshwa watu walikusanyika na kucheza ngoma huku mama Salma alituzwa zawadi kama alivyokuwa akifanya kwa wenzie. Ilikuwa ni sherehe iliyofana sana . Wenye chuki walibaki na chuki zao Salma ndio alikuwa kashaolewa hivyo.
Baada ya ndoa kupita sherehe nilienda kufanyika ukumbini watu wengi walihudhuria sherehe yao na maharusi walikuwa wamependeza mno.

Wakati sherehe zikiendelea Maya alikuwepo ukumbini huku akiwa kalewa , akilia na kuongea maneno yasiyoeleweka akimlaumu Fariss kwa kutokutoa nafasi na kulaani Salma kwa kumchukulia mwanaume aliyempenda.
Watu walimchukua na kumtia nje.
Salma alimuangalia Fariss ambae alikuwa katulia kimnya.
" Fariss yule si ni Maya wa Spain mwenye kuongea kingereza kingi? Salma aliuliza kwa sauti ya chini.
" Mke wangu tulia leo ni siku muhimu sana kwetu.
" Sasa kwanini aje kuharibu shuhuri yangu? Kumualika?
" Hapana.
" Sasa kafikaje hapa?
" Sijui jamani hebu tuachane nae.
" Tutaenda kuongea vizuri tukifika nyumbani.

Basi shuhuri iliendelea vizuri mpaka ilipofika saa sita usiku maharusi wakienda nyumbani kwao, kwenye nyumba yao mpya ambayo ndio walipanga kufanyia Fungate yao .Salma alikuwa kakaa kitandani alivua gauni lake.
Fariss ....
" Nimelichoka hilo jina niite mume wangu sasa.
" Sawa mume wangu unaweza kuniambia Maya kafikaje pale ukumbini.
Fariss alikuwa alivua suti yake ilibidi aache kwanza.
" Mke wangu leo ni siku yetu ya furaha naomba usiongekee mambo ya kukera nataka tufurahie saba yetu kwa mambo mazuri baada ya hapo utaniuliza unachotaka.
" Sawa , siku hazigandi saba itaisha tu.
Fariss hakujali alishamziea mke wake kwa maneno alivua nguo zake kisha akaenda kumsaidia mke wake kutoa gauni la harusi kisha wakaangushana kitandani na kufurahia usiku wao wa kwanza kwenye ndoa.

Baada ya siku tatu kupita Fariss alikuwa bafuni Salma alikuwa kakaa kitandani mara simu ya Fariss iliita , Salma alipoangalia aliona jina la Maya.
" Maya anapiga simu kwa mume wangu anataka nini usiku huu?
Salma aliamua kupokea.
" Hallow.
Maya aliposikia sauti ya kike alitulia.
" Najua wewe ni Maya nataka tuongee.
" Sina shida ya kuongea na wewe mpe simu Fariss.
" Sikiliza wewe mimi sitaki vita wala Shari na wewe ila nataka kukwambia jambo moja tu. Naomba uachane na Fariss na ukibaki kuwa Fariss ameitwa na mimi ndio mke wa halali wa Fariss.
" Wewe unaongea tu unajua nimetoka wapi na Fariss.
" Fariss ameniambia kila kitu. Historia yenu ilishakufa, hata mimi nilikuwa na historia na mwanaume kabla ya Fariss lakini Mungu amepanga tuwe pamoja na tumerudhiana. Pia kila mtu ana riziki yake hata wewe fanya Subra utapata wa kwako ambae utampenda zaidi ya unavyonpenda Fariss Tafadhali usitake kufanya tuwe maadui kwasababu ya mapenzi.

Maya alikaa kimnya kwa muda,kwa mara ya kwanza aliona aibu na maneno ya Salma yalimuingia na kujiona ana hatia .
Wakati huo fariss alikuwa ametoka bafuni akakaa pembeni ya Salma akawa anasikiliza wanavyoongea.
" Asante nimekuelewa. Alijibu Maya kwa upole.
" Karibu na nina kutakua kila la kheri.
Salma alikata simu na kuirudisha alipotoa.
Fariss alimsogelea na kumkumbatia.
" Asante mke wangu kwa kunisaidia.
" Ni jukumu langu ila kama haujanielewa basi yeye ni sikio la kufa.

Maya aliyatafakari sana maneno ya Salma akagundua kweli alikuwa anafanya makosa kumng'ang'ani Fariss ikiwa ni mwanaume wa mtu mwingine. Aliamua kuachana naye kabisa na ili usiwe usumbufu aliamua kuifuta namba ya simu .

Siku zilienda maisha yalikuwa mazuri wivu ulipungua kwa Salma alimuamini mume wake na kumwambia.
" Sasa nakuamini hata wakija wanawake wangapi hawawezi kuichukua nafasi yangu nakuamini mume wangu.
" Nakupenda mke wangu. Pia nimeamini kila kilichopangwa hutokea wewe ni zawadi kubwa maishani mwangu.

MWISHO.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SALMA WA MTAA WA SABA FINALY SEHEMU YA ISHIRINI*  >>> https://gonga94.com/semajambo/salma-wa-mtaa-wa-saba-finaly-sehemu-ya-ishirini

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
majario 22 Aug 2025 08:09
BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘20
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest