Sanga:“Sasa, uko tayari kuona uchawi tuliofanya?”
Mteja (msichana): (anacheka kwa upole, anajishika mdomo kwa kidole) “Aah, lazima nione! Umenifanya nijisikie kama malkia mbele ya kamera.”
Sanga: (akimkazia macho kwa bashasha) “Wewe ni malkia. Ila nadhani ulikuwa unahitaji msukumo kidogo tu. Kamera inampenda sana mrembo mwenye kujiamini kama wewe.”
Mteja: (akizungusha nywele kwenye kidole chake) “Labda ni vile ulivyokuwa unaniangalia ndio maana nilijisikia hivyo. Ulifanya nione kama niko kwenye picha za sexy za jarida fulani.
Sanga: “Mmhmm, sikuweza kujizuia. Kila click ilikuwa kama—bam. Nguvu, mtazamo, mvuto wa kipekee. Ulinipea kila kitu.”
Mteja:“Ahh… usifanye hivyo! Unanifanya nicheke na kuonea aibu!”
Sanga: (akicheka kwa utani) “Kwanini niachie wakati aibu inakupendeza sana? Umechanganya haya yote—aibu na kujiamini—mchanganyiko wa hatari.”
Mteja: (anacheka, anavuta pumzi kwa raha) “Wewe ni mchokozi! Sawa, naomba. Tafadhali, nionyeshe jinsi nilivyopendeza.”
Sanga: (anakandamiza kitufe, picha zinaonekana kwenye skrini) “Haya, angalia sasa. Kumbuka tu, huu ni mwanzo”.