Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’•๐’˜๐’ ๐ฟ๐‘œ๐‘ฃ๐‘’๐‘†๐‘ก๐‘œ๐‘Ÿ๐‘ฆ.....: ๐‹๐€๐’๐“ ๐๐Ž๐‘๐ ๐๐€ ๐๐ˆ๐Š๐ˆ๐‘๐€ ๐˜๐€ ๐‡๐Ž๐”๐’๐„ ๐†๐ˆ๐‘๐‹ (๐™‰๐™™๐™ž๐™ซ๐™– ๐™‰๐™œ๐™ช๐™ฃ๐™™๐™ช) ๐‘ฉ๐’–๐’“๐’–๐’…๐’‚๐’ ๐‘บ๐’Š๐’Ž๐’–๐’๐’Š๐’›๐’Š EP 01

9th Sep, 2025 Views 27


Ni mwezi na nusu ulikuwa umekatika tangu Ray alipotoroka na kwenda dar kuishi pamoja na Nasma. Hata hivyo bado kazi walikuwa hawajafungua bado kwa sababu ya kampuni yao bado kutokuruhusiwa kufanya kazi kwani ilikuwa imeenda kinyume cha taratibu, licha ya kwamba mshahara walikuwa wakipokea kwani bado mkataba ulikuwa unasoma ni wafanyakazi wa pale

Raymond na Nasma walikuwa wanapendana na maisha ya kuishi pamoja yalikuwa yamewapendeza wote wakawa na afya safi na kuwa na mashavu kwa kweli.

Ni siku mbili zilikuwa zimepita tangu Nasma akatae kwenda kule salon kwa ajili ya kujifunza suala zima la ususi
"Sasa kwanini umeamua kuacha mke wangu?" Alisema Ray

"Nashangaa nachoka sana halafu hata kazi yenyewe sielewi, kinyaa na kichefu chefu kila nikijaribu kumtengeneza mtu nywele" alisema binti

"Haha, sasa itakuwaje?" aliuliza

"Acha nikae nitafakari mume wangu halafu tutajua la kufanya kwenye kazi nyingine"

"Ok" Alisema Ray na kwenda sebuleni kuangalia TV

Mara sauti

"Ray" Alisema Nasma

"Sitaki" Ray alijibu kwa wivu

"Hutaki nini?" aliuliza Nasma

"Mara ngapi nimekuambia usiniite Ray"

"Hahaa, samahanii nakuitaga mume naogopa, maana hata hatujafunga ndoa"

"Ndoa gani zaidi ya tunayofungiaga kitandani?" Aliuliza Ray

"Hahahaaa okeeey, naomba uondoke ukaniletee ndimu mimi nilambe" alisema binti

"Mmmh mi siendi kama ndo kamimba hako kameanza kusumbua, halafu unajua nini? kesho lazima tuende hospitali ukapime mimba" Alisema Ray

"Sawa"

Ray aliinuka taratibu na kumtazama Nasma usoni, "Vipi"

"Nasikia kichefu chefu" alimuambia

"Ooooh my God unajua nahisi unaumia but mi nasikia raha, ngoja nakuja"

Ray aliondoka akaenda kuleta ndimu akampatia binti akalamba kwa raha zake, hakika maisha yanaendelea

Bila kuaga Ray alitoka polepole kichwani alijua kabisa kwamba akimuaga Nasma hatokubali, alitembea mpaka njiani na kupanda bajaji huyo barabara ya Mwenge halafu sinza

Sinza alikuwa akiishi mfanyakazi mwenzake aitwaye, Joshua, wote walikuwa nyumbani bila kazi maana walikuwa wanafanya kazi katika ofisi moja, na Ray alipofika hivi alimkuta Joshua akiwa anafanya usafi ndani kwake.

"Oiii" Alisema Joshua

"Niaje mwamba" Ray aliongea na kuketi kwenye sofa huku akimuacha ray afagie fagie juu ya zulia alilolitandaza chumbani mule

"Fresh, Shemeji vipi?" aliuliza J

"aamh soon ntaitwa Baba asee"

"Hahaa sure?" aliuliza

"Yes" Ray aliongea huku akitoa simu iliyokuwa ikiita mfukoni

Kutazama hivi ni mama yake anapiga "Mh Bi Mdashi anataka kuniambia nini tena?" Alijiuliza na kupokea "Hello ma"

"Hujambo?" Aliuliza mama

"Sijambo mama shikamoo"

"Marahaba, vipi bwana nimesikia habari zako"

"Habari gani?"

"Umeoa siku hizi tena bila kutupa taarifa sisi wazazi" alisema

"Hahaaa, mama bana acha masihara, mimi nikaoa vipi? Nani amekuambia hayo mambo?" aliuliza huku kidogo akishtuka kwamba Nasma habari zake zinasambaa vipi wakati yeye alikuwa hajamuambia mtu wa nyumbani

"Anita" aliuliza

"Anita????" alishtuka sana na kusita

"Ndio, mbona umeshtuka?" aliuliza mama

"Hamna mama mi sijaoa amekudanganya" alisema

Anita alikuwa ni mtoto wa mama mkubwa wake Raymond hata hivyo Ray hakujua hizo taarifa zimemfikia vipi maana ni za kweli. Mama alikata simu

Baada ya mama kukata simu, mama aliwaza na kupata wasiwasi 'Usikute Ray aliondoka na Nasma' alijiuliza na kuchukua halafu akafanya kumpigia Anita akaanza kuongea naye

"Anita samahani nakusumbua"

"Usijali mama Mdogo"

"Sasa, huyo binti aliyekutafuta na kukuambia ni mke wa Ray, ulijua sura yake?" aliuliza

"Kiukweli sikumjua ila sauti yake kama naifahamu mama, halafu pia kuna siku niliona Ray amempost msichana wako wa kazi yule pia, kulikuwa na binti mwingine pembeni hivyo sikufanikiwa kufahamu ni yupi mke halali"

"Oooh Mungu wangu" alisema mama na kukata simu kwa hasira "Ray usikute unaishi na yule binti mchafu mchafu ohoo" Alisema mama huku akiitafuta namba ya Ray akampigia "Raymond"

"Mama"

"Una wazimu wewe mtoto" Mama alifoka

"Nini mama lakini?"

"Umemuoa yule binti asiyekuwa na mbele wala nyuma?" aliuliza kwa hasira mama

"Mama"

"Usiniite nakuuliza umemuoa Nasma" Ray alishtuka akijiuliza hizo taarifa mama anazipata wapi? Ilibidi akane

"Mama mimi sina mke"

"Sawa kama hauna mke ila nikuhusie tu mwanangu yule mtoto sio aina yako, yaani kwanza Hana elimu, pili ni mchafu, tatu ile dini yao, nne, kabila lake ushaona mtu anajiheshimu huko?" Aliuliza mama

Kwa hasira ray alikata simu ndipo mama akabaki akifoka "Kwa kweli naapa kwamba kama amemuoa basi abaki naye huko huko mimi sio mwanangu" yaani bila sababu mama alimchukia sana Nasma

Ray aliona kwamba azime simu ili mama asizidi kumsumbua zaidi......ITAENDELEA

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’•๐’˜๐’
๐ฟ๐‘œ๐‘ฃ๐‘’๐‘†๐‘ก๐‘œ๐‘Ÿ๐‘ฆ.....: ๐‹๐€๐’๐“ ๐๐Ž๐‘๐ ๐๐€ ๐๐ˆ๐Š๐ˆ๐‘๐€ ๐˜๐€ ๐‡๐Ž๐”๐’๐„ ๐†๐ˆ๐‘๐‹
(๐™‰๐™™๐™ž๐™ซ๐™– ๐™‰๐™œ๐™ช๐™ฃ๐™™๐™ช)
๐‘ฉ๐’–๐’“๐’–๐’…๐’‚๐’ ๐‘บ๐’Š๐’Ž๐’–๐’๐’Š๐’›๐’Š
EP02

Wakati Ray akiwa ametulia anaangalia TV pale kwa Joshua mara alisikia simu ya Joshua imeita ikiwa kwenye chaji juu ya stuli karibu na ukuta, Ray aliitazama

"Oya Simu yako inaita" Alimuambia

"Nani anapiga?" Joshua aliuliza

"Sijui, namba ni mpya kaka"

Joshua aliacha kufanya usafi na kusogea karibu na simu yake kisha akaitoa kwenye chaji huku akiitazama ile namba "Nani huyu" aliongea na kuiweka sikioni kisha akatulia kimya kusikilizia ni sauti ya nani

"Joshua" Sauti ya kiutu uzima ilisikika

"Naam" J aliongea

"Samahani, umenifahamu" Aliuliza mtu huyo

"Aaaah nimekujua, Boss Shikamoo" aliongea kwa furaha baada ya kugundua ni mkuu wake kazini amempigia

"Marahaba, nimempigia Mwenzako hapatikani"

"Yupi Ray au?" aliuliza J

"Ndio" Joshua aliuliza huku akimgeukia Ray akaongea kwa sauti ndogo

"Vipi eti haupatikani?" Joshua alimuuliza Ray lakini Ray hakuelewa hivyo akabaki anamshangaa

"Anyway" Boss aliongea "Kuanzia J3 nawaomba muanze kuhudhuria ofisini kazi ndo tunafungua rasmi" aliongea

"Eeeh???" Joshua aliuliza kwa Furaha bila kuamini

"Jumatatu kazini" Alisema tena Boss

"Oyooo, sawa boss"

"Ok waambie wenzio" Alisema boss na kukata simu

Joshua aliruka ruka, vijana hawa walipenda kazini kwa sababu ya marupurupu, nje ya mshahara walipata pesa nyingi hivyo Joshua alifurahi sana

"Vipi mzee???" Ray aliuliza

"Jumatatu kazini" alisema Joshua Ray akashtuka naye

"Khaaa,,,,, weee acha ufala" Alisema kwa Furaha zaidi huku akiinuka

"Ufala?, J3 jobu mzee"

"Ayaaaa kum....ke Raha sana kubabake" Ray alifurahi mno.

Furaha iliwatawala, hawakuipenda ile likizo kabisa kwani kuna baadhi ya kipato nje na mshahara walikuwa wakikikosa, hivyo basi walifurahi na pia kukaa nyumbani kulikuwa kunaleta upweke na kujihisi wanaonekana wavivu na wazembe.

Unaambiwa, kwa furaha ambayo Ray aliipata, yaani bila hata kuaga, alitoka nje na kusepa kimya kimya huku uso ukiwa wa furaha na simu kashika mkononi

Ray alitembea tembea kuelekea maeneo ya Mwenge kwa Mguu, hii ni kwa sababu ya kutaka magari ya Makumbusho kuwa adimu maeneo yale

Sasa wakati anatembea pale Sinza kulikuwa na barabara inatengenezwa, njiani kulijaa wakandarasi na watu ambao pia walifanya kama wasaidizi wa wakandarasi hao.

Ray alitembea akakuta kundi la wasichana kama nane hivi ambao pia walikuwa wakifanya kazi pale, wote walivalia vikoi vya kikandarasi na walikuwa wanaongea ila Ray alipofika karibu yao, wakatulia kimya.

Aliwasalimia hawakuitika, akasalimia tena hawakuitika kisha akatembea zake huku moyoni akiwatukana kimya kimya, ghafla vicheko vya nguvu kutoka kwa kwao

"Hahahahaaaaaaaa Huuuuuuu.......Halooooo" Walisema, ndipo Ray alipopata hasira na kuwageukia, aliwatazama hivi walitulia akaangalia kwa kukagua ndipo akagundua mmoja wao ni Rose

Ray hakujali sana aliamua kutembea huku akijiuliza kwanini wamecheka au Rose amewaambia nini akapotezea.

Ray alifika mwenge akapanda Daladala iliyokuwa inatokea Tegeta kisha akaelekea Makumbusho, alipofika hivi, alishuka na kuchukua matunda matunda pamoja na vitu vingine akawa anaelekea navyo nyumbani

Ray alifika katika geti la nyumba aliyopanga akakuta Karimu kasimama pale akiwa anawaza sana, mkono mmoja aliuegesha getini na mwingine alishikilia simu lakini pia alikuwa anatazama mbali sana sehemu moja kuonyesha kwamba alikuwa katika lindi la mawazo

"Oiii" Ray alimuita jamaa akashtuka na kumgeukia "Vipi?"

"Daah umenishtua sana boy" Alisema Karimu

"Unawaza nini mzee baba?"

"Daah, nakupigia simu haupatikani kaka"

"Oh, sipatikani simu nimezima kuna mtu ananisumbua vipi kuna tatizo boy?" aliuliza Ray

"Daah, ingia Ndani uone huko" alisema Karim

"Nini tena"

"We nenda" Karimu alisisitiza

Ray alitembea kuingia ndani ya geti, alishangaa, pale nje kulikuwa na kipande cha nguo ya Nasma ikionekana kuchanika, halafu mbaya zaidi ni kwamba ndani kwake kulikuwa na sauti ndogo ndogo na zilikuwa za kike, Ray aliogopa

Ray alitembea mpaka mlangoni kwake akaita "Hodi humu ndani" Alisema

"Karibuu" Sauti ya mpangaji jirani ilisikika alikuwa anaitwa mama Stii

"Vipi jamani" Ray aliongea na kuingia akachungulia chumbani

Kutazama hivi, ni kwamba majirani wa kike wamemzunguka Nasma kitandani "Vipii???" aliuliza kwa mshangao akaweka mfuko wenye vitu chini na kusogea hadi kitandani

Kutazama hivi kitandani, hakuamini, Nasma alikuwa akivuja damu, alikuwa na majeraha kibao usoni, alikuwa anaonekana mwenye kupigwa halafu alipomtazama Ray usoni hivi alianza kulia machozi mazito

"Mke wangu!!!" aliita kwa mshangao huku akimsogelea na kuchuchumaa akamshika kidogo "Umekumbwa na nini?" aliuliza

"Niacheee" Alimwambia kwa hasira Ray akashangaa maana hakuelewa, binti alijisogeza ukutani akiwa anazidi kulia kwa kwikwi

"Kwanini Sasa Naa??" Aliuliza kwa mshangao

"Naomba uniache" Alisema huku akimsukuma Ray, ilibidi Ray abaki mdomo wazi

"Vipi jamani Nasma kapatwa na nini?" Aliuliza Ray kwa watu waliozunguka pale ndani.....ITAENDELEA
Soma muendelezo wa season two yote kwa sh 1000 tu
Njoo WhatsApp 0743433005

๐‘ต๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ ๐’š๐’‚ ๐’Ž๐’‚๐’๐’Š๐’‘๐’ ๐‘ฝ๐’๐’…๐’‚๐’„๐’๐’Ž ๐‘ด ๐’‘๐’†๐’”๐’‚ 0743433005 ๐’‹๐’Š๐’๐’‚ ๐‘จ๐‘ฎ๐‘ถ๐‘บ๐‘ป๐‘ฐ๐‘ต๐‘ถ
๐‘ผ๐’Œ๐’Š๐’๐’Š๐’‘๐’‚ ๐’๐’Š๐’„๐’‰๐’†๐’Œ๐’Š ๐‘พ๐’‰๐’‚๐’•๐’”๐‘จ๐’‘๐’‘ ๐’Œ๐’–๐’‘๐’Š๐’•๐’Š๐’‚ ๐’๐’‚๐’Ž๐’ƒ๐’‚ +255743433005 ๐’๐’Š๐’Œ๐’–๐’‰๐’–๐’…๐’–๐’Ž๐’Š๐’†.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

๐‘บ๐’†๐’‚๐’”๐’๐’ ๐’•๐’˜๐’ ๐ฟ๐‘œ๐‘ฃ๐‘’๐‘†๐‘ก๐‘œ๐‘Ÿ๐‘ฆ.....: ๐‹๐€๐’๐“ ๐๐Ž๐‘๐ ๐๐€ ๐๐ˆ๐Š๐ˆ๐‘๐€ ๐˜๐€ ๐‡๐Ž๐”๐’๐„ ๐†๐ˆ๐‘๐‹ (๐™‰๐™™๐™ž๐™ซ๐™– ๐™‰๐™œ๐™ช๐™ฃ๐™™๐™ช) ๐‘ฉ๐’–๐’“๐’–๐’…๐’‚๐’ ๐‘บ๐’Š๐’Ž๐’–๐’๐’Š๐’›๐’Š EP 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/season-two-lovestory-last-born-na-bikira-ya-house-girl-ndiva-ngundu-burudan-simulizi-ep-01

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest