"Amepatwa na nini ?" Aliuliza Elian
" Amepata ajari "
alijibu dactari mmoja
" Amepata ajari gani mbona yupo hivi ?" Aliuliza Elian huku ameshika mkono wa Winnie
" Unaundugu na mgonjwa mbona unauliza maswali mengi tunaomba utupishe tumpeleke ndani akafanyiwe huduma laa sivyo atapoteza mtoto wake "
madactari walimuingiza Winnie ndani na muda huo riffat alifika na gari lake
" Riffat "
aliita Elian lakini riffat hakumsikiliza aliingia ndani ya hospital kujaza taarifa za mgonjwa Elian alimfuata nyuma
" Unajua ana mimba ya miezi mingapi ?"
Dactari mmoja alimuuliza riffat
" Ndiyo ni miezi mitatu Sasa kama na week mbili , tafadhali dactari naomba umuokoe Winnie na mtoto wake" riffat alimuomba sana dactari, Elian yeye alibaki kushangaa
" Tutafanya chochote tunachoweza kuwaokoa wote wawili"
alisema dactari kisha aliondoka
" Ina maana mtoto ni wa kwangu ?"
Elian alijiuliza mwenyewe
" Wewe kwanini umefanya hivi Elian nina uhakika watekaji wataKuwa walikutafuta kwanza wewe na sio mimi "
riffat alimshika shati Elian
" Sikuwa najua kama ni mtoto wangu "
machozi yalimtoka Elian
" Hata Kama sio mtoto wako Elian ulitakiwa kuwa na ubinadamu hata kidogo Nina uhakika ungeweza kumsaidia milioni 5 sio kitu kwako ,nataka uondoke Sasa hivi Winnie ni jukumu langu kwanzia leo nenda kwa mwanamke wako "
riffat alimfukuza Elian, Elian alitembea akiwa na mawazo hakujua hata amefika vipi kwenye chumba alicho pumzishwa loveness
" Elian vitu nilivyokuagiza viko wapi ?"
Aliuliza loveness
" Aaah ngoja nikanunue sijui imekuwaje sikununua "
Elian alitaka kuondoka loveness akamzuia
" Elian haupo sawa niambie nini shida ?"
" Ni Winnie yupo hapa hospital ameumia vibaya sana na ana mimba yangu , loveness sijui nafanya nini "
" Nenda ukajue Hali yake ukiendelea kukaa hapa utazidi tu kuumia na kusongwa na mawazo "
Elian alienda alikuta Winnie anatolewa chumba Cha huduma na kupelekwa wodini
" Winnie nisamehe najua nimefanya kosa kubwa sana lakini nahitaji msamaha wako "
Elian alitaka kumshika Winnie, Winnie akausukuma mkono wa Elian
" Doctor nataka kuwa mwenyewe waambie watoke "
Winnie aliongea kwa sauti ya chini sana ni wazi alikuwa na maumivu makali
" Mtoke nje Sasa ili mgonjwa aweze kupumzika "
doctor alitoka nje ya chumba akiwa na riffat na Elian
" Anaendeleaje kwa Sasa yeye na mtoto ?"
Aliuliza Elian
" Maendeleo ni mazuri kidogo kwa mama ataendelea ku recover lakini amempoteza mtoto wake ndomana anahitaji kupumzika zaidi "
doctor aliondoka
" Haya yote ni makosa yangu "
Elian alianza kulia , riffat alimkumbatia
" Sasa unalia nini na unatarajia mtoto mwingine kutoka kwa loveness"
" Loveness ni kama rafiki tu kwangu na yule mtoto sio wa kwangu riffat ni story ndefu "
Elian alimuelezea riffat kila kitu
" Ulitakiwa kusema mapema ona Sasa na mimi nikaanza kukuchukia "
" Nilitaka iwe Siri mpaka tutakapofanikiwa kumpata Collins, natamani kurudisha masaa nyuma ili nimuokoe Winnie pamoja na mtoto wetu "
" Unajua kabisa Hilo haliwezekani kwa ushauri wangu subiri apone utajaribu kuongea nae "
" Hawezi kunielewa kabisa anauchungu wa kumpoteza mtoto"
" Acha kukata tamaa mapema mimi nitakusaidia kuongea nae "
aliongea riffat huku analipiga piga bega la Elian
" Nitashukuru sana kaka "
Zilipita siku nne Winnie akiwa bado yupo hospital na siku hiyo alikuwa anaruhusiwa kwenda nyumbani akiwa anashuka ngazi alikutana na loveness pale pale hospital
"Mambo Winnie,nimesikia ulipata ajari pole "
loveness aliongea lakini Winnie hakumjibu chochote badala yake alimkaba loveness
Riffat na Elian walifika wakakuta watu wanashangaa Winnie amemkaba loveness
" Winnie acha kufanya hivyo ni hatari "
alisema Elian
" Hatari ? Unajua mimi nilinguka sehemu hatari kiasi gani hahaha " Winnie alicheka kama chizi
" Nitamsukuma kwenye ngazi mtamlipa mtoto wangu kwa mtoto wenu "
Winnie aliongea kwa kupiga makelele
" Winnie tafadhali usifanye hivyo unaweza kuniumiza mimi kama unataka lakini sio loveness Wala mtoto wake"
alisema Elian
" Wow hongera sana binti inaonekana unapendwa sana " Winnie alimsukuma pembeni loveness kisha alianza kuondoka.
" Winnie "
Elian alitaka kumfuata Winnie , riffat akamzuia
" Ana hasira sana kwa Sasa utaongea nae siku nyingine "
riffat alimfuata Winnie
Ilipita week nzima ndipo Winnie alirudi kwenye Hali yake ya kawaida
Na kwa upande wa Elian alifanikiwa kumpata Collins
" Mbona unatabasamu sana umefanikiwa kurudiana na Winnie ?" Aliuliza loveness
" Hapana ni habari njema kwako ,nimefanikiwa kujua Collins Yuko wapi " aliongea Elian huku anatabasamu
" Wow thank you so much Elian "
loveness alienda kumkumbatia Elian
" Kesho tunatakiwa kwenda London amesema anataka kukutambulisha kwa shangazi yake na mjomba ake watu pekee waliomlea na baada ya hapo atakuja Tanzania kwaajili ya ndoa "
" Yani natamani twende hata Leo "
loveness alifurahi sana
" Anza kufanya mandalizi mimi natoka kidogo Kuna mtu naenda kuonana nae "
" Tunaenda wapi riffat ?" Winnie alimuuliza riffat wakiwa kwenye gari
" Kuna sehemu nzuri sana tunaenda utajua tukifika "
walifika nje ya jumba moja kubwa sana walipaki gari na kuingia ndani
" hii nyumba ni nzuri sana afu inaonekana mpya kabisa unataka kununua nyumba kwaajili yako na Tracy mkifunga ndoa ?"
Winnie alimuuliza riffat
" Hapana utajua Sasa hivi nisubiri kidogo narudi endelea kuangalia mazingira ya nyumba " riffat alitoka nje Winnie akiwa anaendelea kuangalia mazingira ya nyumba alisikia mlango unafunguliwa
" Riffat hii nyumba Iko Bomba sana kama unataka kuiacha sikushauri kabisa ingekuwa sio huu ufukata wangu ningeinunua hii kwaajili ya wazazi wangu " Winnie aliongea bila kugeuka nyuma akijua aliyeingia ni Riffat
" Umeipenda?"
Ilisikika sauti ya Elian nyuma ya Winnie Unafanya nini hapa,?" Winnie alimuuliza Elian kwa ukali
" Nipo hapa kukuomba msamaha Winnie tafadhali misikiliza kule nitakachokwambia " Elian alitaka kumshika Winnie , Winnie alimsukuma
" Sitaki kusikia chochote kutoka kwako na kingine jiheshimu kwani wewe si una mke na unaenda kuwa baba hivi karibuni " Winnie alitaka kuondoka Elian alimvuta akamkumbatia kwa nguvu
" Nisamehe sana Winnie sikuja hapa kugombana na wewe nataka tu kuongea maneno machache na wewe "
" Niachie Elian nitakun'gata Sasa ivi " Winnie hakuwa anatania aliun'gata mkono wa Elian , Elian alimuachia alitoa karatasi na kumpatia Winnie
" Unanipa hizo karatasi za nini ?"
" Ni hati ya hii nyumba inaonyesha wewe ndo mmiliki wa hii nyumba kwanzia leo "
" kwanini unipe hati ya hii nyumba na sio loveness ?au unataka kunifanya niwe mchepuko ? Hilo sahau " Winnie alimtupia Elian ile hati ya nyumbaA
Offer offer offer
Soma yote kwa sh 600
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.