Salma alikaa kimya kwa sekunde kadhaa huku moyo wake ukidunda kwa kasi. Alijiuliza maswali mengi: "Nitamvutia kweli mama yake Fariss? Atanipokea kama mke wa mwanae? Je, akijua mimi ni mtoto wa uswahilini niliekuwa na maisha atanikubali kweli?"
Alijiuliza maswali mengi sana lakini hakutaka kumuonyesha Fariss hofu hiyo.
" Vipi mpenzi mbona upo kimnya?
"Ni sawa mpenzi tutaenda. alisema kwa sauti ya chini.
"Nitakuandalia kila kitu. Usijali, Fariss alimhakikishia hilo.
" Sawa, naenda saluni basi kesho asubuhi utaniambia tunaenda muda gani.
"Sawa. Nataka uvae kistaarabu, bila make up nyingi. Mama yangu ni mtu wa heshima sana, hapendi vitu vya kisasa kisasa sana.
Atapenda kukuona ukiwa na ngozi yako asili maana nimekupigia sana mbele ya mama yangu.
" Angalia sifa zako zikawa hazipo sahihi.
" Kwenye urembo wako nipo sahihi kabisa.
" Sawa mpenzi asante.
Salma alikata simu alafu alitabasamu.
"Hii ni nafasi yangu ya kuonyesha thamani yangu," alijisemea.
Kesho yake, Salma aliamka mapema, akaenda saluni. Nywele zake zikaoshwa na kutengeneza vizuri.
Alivaa abaya lake safi la rangi ya blue akafunga mtandio wake vizuri , akapaka mafuta mepesi usoni, na mdomo wake ulipaka mafuta siku hiyo hakupaka lipstik wala wanja.
Majira ya saa tano mchana, Fariss alifika kumchukua.
Alimkuta Salma akiwa tayari, amekaa sebuleni akiwa ametulia akimsubiria.
Fariss alipomuona alishangaa maana hakuwahi kumuona hata siku moja akiwa kajistiri vile.
"Mashaallah ,mrembo wa nguvu! Umependeza sana.
Salma alimuangalia akatabasamu.
" Hebu simama nikuone vizuri mpenzi.
Salma alisimama. Fariss alisogea karibu zaidi na kumkumbatia.
" Waoooo , Salma haujawahi kunifurahisha kama ulivyonifurahisha siku ya leo , sasa haya ndio mambo anayotaka mama yangu na harufu ya udi hapo ndio umeuwa kabisa.
Fariss alisema huku akimkazia macho .
"Usinifanye nicheke," Salma alisema huku akicheka kwa aibu.
"Wacha nikupeleke ukakutane na mama yangu, najua atakupenda."
" Unavyonipa moyo sasa.
" Usiogope mpenzi twende ukamuone mkwe wako.
Waliondoka ndani wakaenda kuingia kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Fariss ikaaza. Nyumba ya mama Fariss ilikuwa Sinza, eneo tulivu lenye nyumba za kisasa. Walipoingia mlangoni, walipokelewa na mlinzi ambaye alifungua geti kwa heshima.
"Karibu mama,"mlinzi alimkaribisha Salma.
"Asante kaka," alijibu kwa heshima na kusalimiana
Mama Fariss alikuwa amekaa sebuleni akisoma kitabu cha dini .Aliposikia watu wakiingia, aliweka kitabu juu ya meza na kunyanyuka. Mwanamke huyo wa makamo, alisogea mpaka mlangoni na kuwakaribisha.
" Karibuni ndani.
" Asante.
Waliingia na kwenda kukaa kwenye makochi ya kisasa huku Salma aliangalia mazingira kwa kuibia.
Baada ya kutulia kidogo Fariss alianza kumtambulisha Salma
"Mama, huyu ndiye Salma yule binti nilie kwamba ," Fariss alisema.
Salma alinyanyuka kwenye kochi akapiga magoti kidogo. Na kusalimia kwa heshima
"Shikamoo mama."
"Marahaba," mama alijibu kwa sauti ya upole lakini yenye mamlaka.
"Karibu sana mwanangu jisikie upo nyumbani.
" Asante.
Mama Fariss aliwatazama wote wawili kwa makini, kisha akamwelekeza Salma kukaa.
" Salma njoo ukae karibu yangu.
Salma alinyanyuka na kwenda kukaa pembeni yake.
Mama Fariss alimuangalia kisha akasema.
" siku hizi wanawake wengi wanataka wanaume wenye hela lakini hawana heshima kabisa, sasa sijui wewe ni wa aina gani, Salma?"
Salma alitulia kidogo akameza mate kisha akasema
"Mimi nimetoka kwenye familia ya kawaida, lakini nimefunzwa na mama kuhusu heshima, kujitambua, na kutokuwahi kumtazama mwanaume kwa sababu ya mali au kitu chake ninachojali ni mapenzi yangu ya kweli kwake.
Mama Fariss alimtazama tena kwa makini, kisha akatikisa kichwa.
"Naona ulichonacho kina thamani, si sura tu bali hata tabia.
Mazungumzo yao yaliendelea kwa ustaarabu na hekima. Mama Fariss aliuliza maswali kuhusu familia ya Salma, maisha yake, malengo yake, na pia alipenda jinsi Salma alivyojibu kwa ujasiri na kwa heshima.
Baada ya muda, mama Fariss alimwambia Fariss kwa sauti ya taratibu.
"Fariss huyu binti anahitaji kupangiliwa maisha mapema. Kama umeamua yeye ndiyeawe mwenza wako usichelewe. Usimuweke roho yake juu, usimuache njia panda. Haya mambo ya kuchumbia miaka mitano, hayana maana.
Salma alijawa na mchanganyiko wa hofu na furaha. Fariss alitabasamu.
"Ndio mama, mpango huo upo."
"Vizuri sana baraka zangu nawapatia. Salma mwanangu karibu nyumbani hii ndio itakuwa familia yako mpya,"
" Sawa mama asante.
Walipomaliza maongezi walipata chakula cha mchana pamoja . Baada ya hapo Salma na Fariss waliondoka wakiwa na furaha.
" Uuuuh Fariss sikutegemea kama mama yako angenipokea kama vile.
" Nilikwambia mama yangu hana mambo mengi ni lazima angekukubali tu.
" Nimependa kwa kweli.
" Unatakiwa kujiandaa sasa si umesikia anataka nikuowe mapema.
" Mimi sina cha kujiandaa ni wewe mwenye hilo jukumu la kuja kumaliza kila kitu nyumbani kwetu.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.