Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Shalha alielekea moja kwa moja hadi ndani ofisini kwa Brown ambaye alishavurugwa kivyake.
"Brown, siwezi kuvumilia dharau hizi anazo nionyesha mdogo wako".
Brown aligeuka na kumtizama.
"Mama alisema mimi ndo ni design kwaajili ya hii events inayokuja, ila sasa mdogo wako amempa kazi hiyo Nanah na anasema yeye ndo mkuu wa kitengo pale"
Brown alibaki akiwa anamtizama tu.
"Brown , naongea na wewe".
"Shalha Mpigie simu mama mwambie Bieber amekunyang'anya alichosema nikupe. Hilo halinihusu mimi".
"Lakini wewe ndo una manage kila department hapa. Unaweza kusema kitu gani kifanyike".
"Siwezi" alijibu Brown.
"Huwezi? Kivipi?" Aliuliza Shalha.
"Kwasababu siwezi and Shalha, embu niondole kelele hapa tafadhali ni asubuhi sana na sitaki kashkash".
Brown alimfuata Shalha akamshika mkono na kumtoa ofisini kwake.
Shiiiittttt!!! Alisema hilo akiwa amekasirika kwelikweli.
"Sitaruhusu Bieber ayaharibu maisha ya Nanah hata kidogo".
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Bieber akiwa ndani ya ofisi yake macho yake yote alijikuta yakiwa kwa Nanah aliyekuwa busy akijaribu ku draft mchoro kwenye karatasi.
Doy alimfinya dada yake Kurwa atizame ofisini kwa Bieber.
Kurwa alitizama na kuona Macho ya Bieber pamoja na tabasamu lake likielekea kwa Nanah
Alimgeukia Doy na kuguna mmmhh huku akitoa macho kwelikweli.
Nanah akiwa anapepesa macho yake alikutana uso kwa uso na Bieber aliyejaza tabasamu usoni.
Alimtizama kwa sekunde kadhaa na alipoona aibu aliyatoa macho yake kwa Bieber na kujifanya anaendelea kuchora ila alipoyarudisha tena aliyakuta yakimtizama vile vile.
"Nanah, njoo tubadilishane pa kukaa" alizungumza hilo Bob Risky na kuinuka kwenye meza yake iliyokuwa upande mwingine karibu na mlango wa kuingilia ofisini kwa Bieber.
Nanah aliona ni vizuri sana kwani macho ya Bieber bado yalikuwa yakimtizama.
Bob Risky alikaa pale alipokuwa amekaa Nanah mwanzo na sasa alitaka Bieber amtizame yeye na siyo Nanah kwani alipatwa na wivu.
Nanah alienda kukaa sehemu ambayo Bieber hakuweza kumuona zaidi ya mgongoni tu.
Bieber alitoka ofisini kwake na kwenda akakaa kiti cha mbele ambacho hakikuwa na mtu na sasa alimtizama Nanah moja kwa moja.
Nanah aliinua macho akimtizama
Bieber alikunja nne yake akaweka mikono yake mfukoni na hakusema lolote isipokuwa kumtizama tu.
Bob Risky ndo alizidi kukasirishwa na kitendo kile cha Bieber kumtizama Nanah.
Nanah naye alikosa kabisa ujasiri na kujikuta hachori chochote tena kwenye karatasi lake zaidi ya kuisimamisha penseli.
Shalha naye alikuwa mlangoni akishuhudia tukio lile.
Nanah aliinuka na Bieber alimshika mkono.
"Naondoka mimi kama unaona aibu nikikutizame" alisema hilo Na kuinuka akarudi ofisini kwake.
"Sitaruhusu, Nanah amchukue Bieber kutoka kwangu kamweeeee!!"
Alikula kiapo hicho na kutizama namna Bob alivyoshikwa na hasira na yeye na aliona huyu ndo wakuanze naye.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Bob hivi unajijua wewe ni mzuri?" Aliuliza Shalha wakati ambao Bob alikuwa akipata juisi yake kwenye kivuli cha mti.
"Najua".
"Hapana hujui, yani wewe ni mzuri kuliko mwanamke yoyote kwenye ile ofisi yenu. Alafu unajua kuna siku nilikuona ukikatika balaa".
"Hahahah Madam Shalha bhana".
"Na sikutanii, yani unajua kukatika sana trust me ofisi nzima hii hamna mwenye kiuno kilaini kama chako, hata Nanah hakuwezi"
"Sitaki kusikia jina la huyo mchawi, yani siku ile ningeliacha life na pumu yake".
"Ana pumu?" Aliuliza Shalha kwa mshangao.
"Ndiyo" alijibu Bob.
"Ila tuachane nayo hivi unamuonaje Bieber?"
"Unamaanisha nini?"
"Naona namna unavyompenda, alafu unajua Bieber ni kijana wa kimarekani eee? Kwahiyo hakushangai kabisa".
"Unamaana gani?"
"Mmmhhh namaanisha Marekani mambo ya jinsia moja ni sawa, na Bieber alikuwa huko kama unampenda unapaswa kuonyesha hisia zako na siyo kumuachia huyo Nanah".
"Mbona sikuelewi" alijibu Bob akikaa vizuri na kuacha kunywa juisi yake.
"Bieber ni shemeji yangu na Amini mimi nikikwambia ya kuwa una nafasi ya kuwa na Bieber kimapenzi".
Bob Risky alitabasamu na kuweka juisi yake chini kisha akamshika kwa mikono miwili Shalha.
"Eheeeee!!"
"Unapaswa kupigania penzi lako na siyo kumuachia huyo mshamba asiyeweza hata kuvaa nguo vizuri na kama uko seriously na shemeji yangu na unaniahidi kuto kumuumiza basi nitakupa mbinu za kumpata". Alisema hilo Shalha na kuona kabisa alichokitaka tayari kimesha fanikiwa.
"Nakuahidi sitafanya kosa hata kidogo"
"Kitu cha kwanza pata hiyo michoro anayo design".
"Kwanini?"
"Kwasababu Bieber hapendi mtu mzembe, mfanye aonekane mzembe kwa kila anachokifanya nakuhakikishia Bieber ataanza kukuona wewe wa maana sana".
"Hiyo ni kazi rahisi sana kwangu, niamini mimi" alijibu Bob Risky akitabasamu.
"Nakuamini na naamini hichi kimtu kilichokuja juzi hapa hakiwezi kuwa juu ya sisi sote". Shalha alimshika mkono na kumuonyesha ishara ya kuwa wako pamoja.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Bieber aliingia ofisini na kugonga meza ya Nanah.
"Njoo ofisini kwangu".
Aliingia ndani na Nanah alimtizama kisha akainuka na kumfuata.
"Doy nakwambia kiutani utani hivi hivi utashangaa tunaanza kumuita Madam huyu Bi Mkosi kama ilivyokuwa kwa Shalha na tuko hapahapa shoga angu siyo mimi wala wewe mwenye nyota ya kueleweka".
"Mmmhh sema wewe shoga angu. Mi kuna vitu sivielewi ujue. Au sisi nyota zetu zimefukiwa makaburini?".
"Nimeshakwambia mara nyingi sana Doy, tukajitizame kwa waganga unasema ushirikina haya ona wanao enda kujitizama mambo yanavyo wanyookea".
"Mmmhhh sema kweli, ila waganga wenyewe ndo hawa unaona mabango mabarabarani? Wale matapeli bhana we tafuta waganga wa kueleweka". Alisisitiza Doy.
"Mbona hujaja na sketch zako?" Aliuliza Bieber.
"Hukuniambia hivyo"
"Haya kaleta nione, ulichofanya mpaka sasa"
Nanah aliondoka na kurudi akiwa na karatasi kadhaa mkononi mwake.
Alimuonyesha.
"Kaa nitachukua muda kuzipitia kidogo".
Nanah aliketi na kumtizama Bieber akiwa anasubiria majibu ya kile alicho kifanya.
"Umeenda kupata lunch wewe?"
"Hapana ila nitaenda" alijibu Nanah.
Bieber alitoka kimfuko na kuweka mezani.
"Endelea kula wakati napitia pitia hichi ulichokileta".
"Nitaenda kula boss".
"Boss?" Aliuliza Bieber akimtizama Nanah.
"Ndiyo wewe ni Boss wangu".
"Mmmhhh sawa Sekretari Nanah" alijibu Bieber na kuongezea.
"Ila ukumbuke tu hutatoka hapa kama hutakula nilichokupatia".
Bob alirudi na kumuona Nanah akiwa ofisini kwa Bieber alivuta mdomo wake kwelikweli huku akipandisha na kushusha hasira zake.
"Nitakuonyesha, huwezi kumchukua Bieber kutoka kwangu".
Itaendelea In Shaa Allah.