Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Shalha alibaki akiwa anamtizama Bieber na kushindwa kusema jambo.
"Haya file la nini hili?"
"Nimeleta sketch za design za nguo kwaajili ya event ya mwezi huu".
"Sawa nitakagua kisha nitakujulisha".
"Nimeambiwa umempa nafasi Nanah na yeye aandae".
"Ndiyo"
"Ndiyo?" Aliuliza Shalha kwa mshangao.
"Ndiyo, kuna tatizo kwani?"
"Unaulizaje kama kuna tatizo? Inamaana we huoni tatizo?"
"Tatizo gani sasa?" Aliuliza Tena Bieber akimtizama kwa kutokutambua tatizo.
"Sawa endelea ku ekti kama haunielewi. Ila Bieber unawezaje kumruhusu huyo mwanamke awe mshindani wangu?"
"Shalha, embu weka pembeni hayo mashindano yako ya kimwanamke, hapa ni kwenye kampuni na tunahitaji lililo bora na siyo wewe na Nanah tu ndo mtajumuika na hili Bob , Kurwa na Dotto pia wote nimewapa kazi hiyo hiyo uliyonayo wewe na Nanah".
"Unasemaje wewe? Yani umeanza kulinganisha kipaji changu na hao wakina Doy? Huoni kwamba unanishushia heshima?"
"Mmmhh Shalha sasa ni vyema ukanionyesha kwa wakati huu kwamba wewe huna mshindani kati ya hao wote. Na nikwambie tu jambo hili litakuwa fair kwa kila mtu. Sitampendelea yoyote yule"
"Oohh kweli kwamba hutampendelea yoyote hata haka ka mdoli kako kapya".
"Ndiyo hata hako ka mdoli kangu kapya" alijibu Bieber.
Shalha aliondoka kwa hasira na kumuacha Bieber ofisini kwake.
Alisimama na kumtizama Doy na Kurwa waliokuwa busy na karatasi mkononi mwao waki design na ndivyo ilivyokuwa kwa Bob pia.
Alimkazia macho Nanah ambaye alikuwa busy akiandaa zake mchoro mwingine.
Alitoka kabisa njee na kuelekea ofisini kwake.
Nanah aliinua macho yake sasa na kutizama mlango alioweza kutokea.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Umeshampata huyo mwanamke?" Alihoji Bi Everline akizungumza na mtu fulani kwenye simu.
"Hapana , bado nazidi kumtafuta. Bi Everline unajua alikuwa akikutana naye kwa siri sana katika hoteli ambayo inaficha sana taarifa za wateja wake".
"Ni zaidi ya miaka 3 sasa bado jibu lako ni lilelile , kama unaona hii kazi ni ngumu kwako niambie mapema acha kuniambia maswala ya hoteli inaficha taarifa maana kila siku maneno yako ni hayohayo".
"Bi Everline, nataka nikwambie tu nipo karibu na ukweli hivyo vumilia kidogo".
"Sawa na vipi kuhusu mwanamke aliyewagombanisha vijana wangu?"
"Bi Everline hiyo umeniambia siku mbili tu zilizopita na tukio hilo lilitokea miaka ya nyuma lazima itanichukua muda mrefu kidogo kupata mahali pa kuanzia".
"Basi sawa , ila nakwambia tena siku ukimjua huyo mwanamke sitaki umfanye chochote kile mpaka mimi nitakapokuwa hapo".
"Usijali Bi Everline, wewe ndiye Bossi wangu kwahiyo nitafanya utakacho".
Bi Everline alikata simu yake na kijana yule alitabasamu akigeukia kitandani kwake huku akiwa kifua wazi.
"Anasemaje huyo Bi kikongwe?" Aliuliza Shalha ambaye alikuwa kitandani kwa mwanaume huyo wanayemuita William.
"Bado anataka kukufaham mchepuko wa mume wake"
"Hahahaha"
"Na pia mwanamke uliyewagombanisha vijana wake" alijibu William akim busu Shalha.
"We mwanamke ni hatari kama nyoka, hivi umewezaje kulala na wanaume wa familia moja? Yani baba na watoto wake?"
"Hata wangekuwa na babu yao ningelala nao pia" alijisifia ujinga Shalha.
"Na namna ulivyomfanya Brown akanyamaza ndo sija ielewa hadi leo"
"Hahahaha Brown alinikuta na baba yake na Bieber alishanitambulisha kwake kama mpenzi wake. Hivyo kwa kulinda heshima ya baba yake alimwambia baba yake aondoke na mimi niachane na Bieber. Nilikubali tu pale ili kupooza mambo ila alipokuwa akinywa mipombe yake nilimpa mhudumu kidonge chetu na alienda kumuekea alipokuja kuzinduka ni mimi nilikuwa naye kitandani. Alikasirika sana ujue ila nilimwambia sitaachana na Bieber kama vipi aniowe yeye akakubali".
"Hahahaha".
"Brown anampenda Sana mdogo wake Bieber asingeacha Bieber alale na mwanamke mchafu kama mimi hivyo akaona mimi tu ndo niwe wake".
"Lakini angeweza kumwambia Bieber na hasara ingekuwa kwako".
"Kamweeeee Brown hawezi mwambie mama yake wala mdogo wake uchafu wangu. Hataki waumie kwa namna yoyote ile niamini mimi".
"Mmmhh hivyo ni vizuri pia, kwasababu utafanikisha jambo lililoweza kukupeleka kwenye ile nyumba na usisahau mimi ndo mwanaume wako".
"Inafahamika hilo William"
William na Shalha walianza kula burudani na William alimuuliza
"Utaondoka saa ngapi?"
"Hakuna anayejali kuhusu mimi William, nimemaliza zaidi ya lisaa limoja na hakuna hata simu iliyoita".
"Hahaha nimefurahi kusikia hivyo" alijibu William na waliendelea na mambo yao sasa.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Vipi huendi nyumbani wewe?" Aliuliza Bieber akitoka ofisini kwake na kumkuta Nanah akiwa anafanya kazi tu.
"Namalizia hapa Bieber"
"Napenda unavyoniita" alizungumza hilo Bieber na Nanah aliinua macho yake akimtizama kisha akasema.
"Namaanisha Boss Bieber".
"Ni sawa Sekretari Nanah" alijibu Bieber na kuvuta kiti kisha akakaa karibu na Nanah.
Nanah alisogea nyuma kidogo kwani alimsogelea kwa ukaribu sana.
Bieber alibaki akiwa anamtizama tu hali iliyomnyima confidence Nanah ya kuendelea na kazi yake.
"Mi ukinitizama siwezi kufanya chochote, unaweza kwenda?"
"Hapana, kwasababu bila kukutizama siwezi kulala kabisa usiku".
Nanah alitabasamu kwani alijua kabisa anadanganywa.
"Umetabasamu kikejeli flani hivi, kwamba huniamini au?"
"Niliacha kuwaamini wanaume siku kaka yako, aliyonikataa mbele za watu". Alijibu Nanah.
"Huyo siyo mwanaume ujue, ni mpumbavu mmoja hivi mwenye jinsia ya kiume".
"Hahahha" Nanah alicheka na kuweka kalamu yake chini akitaka kupiga stori sasa zinoge.
"Na wewe ndo mwanaume sasa Bwana Justin Bieber".
"Hahahaa acha ukorofi wewe. Mi siyo Justin Bieber na Bieber Bernard Benjamini"
"Kwanini mna ma B B mengi hivyo?"
"Sielewi hata si unajua unapewa jina bila hata kushirikishwa na wazazi wako".
"Hahahaa unanifurahisha wewe, sasa ungewezaje kushirikishwa wakati ulikuwa mchanga hivyo".
"Wangeniitaga tu mtoto wasubiri nikuwe ndo tujadiliane kuhusu jina langu".
"Hahaha we unachekesha kweli"
Bieber alibaki akitizama tabasamu la Nanah na Nanah aliacha kucheka kisha akamuuliza
"Vipi?"
"Hivi unajua nakupenda kweli?"
"Sijui, sitaki kujua na siwezi kumuamini mwanaume yoyote yule duniani".
Bieber alimshika mkono Nanah.
"Namaanisha nachokisema".
"Kama una mpango wakumlipizia Kisasi Brown kwa kupitia mimi, utapoteza muda wako Bieber. Yani mimi sina hisia na mwanaume yoyote yule unless nitakuchezea tu na kukuacha"
"Napenda kuchezewa sana mwenzako, vipi ukanichezee leo?"
"Uko tayari?" Aliuliza Nanah.
"Yeah"
"Namaanisha Bieber".
"Namaanisha pia Nanah, vipi unaenda kunichezea wapi kwangu au kwako?" Alihoji Bieber
Na baadae wote wawili walionekana kitandani kwa Nanah wakibanjuana.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Yani mkeo mpaka saa 3 hii usiku hajaja na wewe unakula tu?"
Brown alimtizama mama yake na kumuuliza.
"Unataka hiki chakula nile au nikiache?"
"Eeeeh sorry!! Lakini nimeuliza tu kazini mnatoka saa 12 mpaka sasa hivi mkeo hajaja na hujauliza chochote kile ni kosa mwanangu?"
"Jamani za saizi" aliingia ndani Shalha.
"Ooohh binti yangu yani nilikuwa nakuulizia sasa hivi kwa mumeo".
"Mama nilibanwa na kazi kwelikweli si unajua events tumebakiza wiki tatu kasoro?"
"Mmmhh ila mbona sikukuona kazini maana ndo nilikuwa huko".
Shalha ali stuck kidogo kisha akajichekesha na kusema
Yes.....aammmhhh nilienda kwenye duka letu la vitambaa kwaajili ya kuona kitambaa gani kitakuwa poa".
"Nilikuwa huko pia lakini sikukuona"
"Ulifika?" Aliuliza Shalha
"Ndiyo"
"Mama una haja gani ya kumuuliza swali mtu ambaye anakujibu uwongo?" Aliuliza Brown
"Brown unamaanisha nini mume wangu?"
"Nimeshiba jamani" alijibu Brown na kuamka akiondoka zake mezani.
Shalha aligeuka na kumtizama kwa kejeli hadi alipoishilia chumbani kwao alimgeukia mama mkwe wake.
"Ulikuwa wapi Shalha?"
"Mama" aliita Shalha akijaribu kutafuta uwongo mwingine.
"Hakuna mwanamke ninayemchukia katika maisha yangu kama msaliti, siku nikigundua unamsaliti kijana wangu. Nitahakikisha hutaisahau katika maisha yako" alisema hilo Bi Everline na akiwa hana sura ya utan kabisa usoni mwake.
"Mama kwanini unanifikiria hivyo?" Alihoji Shalha akimshika mkono na kuanza kutafuta uwongo mwingine.
Itaendelea In Shaa Allah.