Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Alifika mahala pale na kuutoa mchoro wake ambao unafanana na ule Alioweza kuonyeshwa na Bob.
Aliufinyanga finyanga na kuutupia kwenye Dustbin huku akivuta pumzi nzito kwelikweli.
Bieber alimtizama na kujua kabisa hilo limemuumiza Nanah.
Alichukua karatasi na kuchonga penseli kisha na yeye moja kwa moja alianza ku draft mchoro.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Baadae kidog Doy alikuja ofisini na hapakuwa na yoyote kabisa.
Aliona karatasi lililo viringishwa viringishwa likiwa ndani ya Dustbin na alilichukua kisha akalifungua.
"Huu mchoro.....heee!!! Mbona uko vizuri hivi kwanini ameutupa? Hapana nahakikisha hatakaa auokote tena na huu utakuwa mchoro wangu" alijiambia hivyo Doy na kwenda na ule mchoro kwenye meza yake.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Kwanini umekuja?" Aliuliza Nanah.
"Unaniuliza kama Boss Bieber au kama Bieber?" Alihoji Bieber aliyekuwa nyuma ya Nanah anayechagua vitambaa kwaajili ya michoro yake miwili iliyobakia.
Nanah alimtizama tu na kutabasamu.
"Hapo itakuwa naulizwa kama Bieber na kama ndo hivyo najibu kama ifuatavyo..... alizungumza Bieber na kubaki kimya.
Nanah alibaki akiwa amemtizama na Bieber alitabasamu kisha akamwambia
"Natamani nikuone kila saa ndomaana nipo nyuma yako kila mahali"
"Hahahahah" Nanah alicheka tu kwa kuachia tabasamu bila kutoa sauti.
"Ok Bieber".
Walianza kutembea na Bieber alimuuliza
"Unachagua nguo ya mshono upi?"
Nanah alitoa simu yake na kumuonyeshea.
"Mmmmhh kama ni huu, basi unapaswa kupata kitambaa cha silk chenye rangi ya gold alafu kwa upande wa stones sasa ziwe za tanzanite unaonaje?"
Nanah alifikiria kwa sekunde kadhaa na kumjibu.
"Yeeah ni sawa, good Boy".
"Nanah kwakuwa nimekuwa Good Boy, ukanichezee tena basi na leo usiku".
Nanah alitoa macho kwelikweli akishangaa na Bieber alimpandishia nyusi zake juu.
Mmmhh alikohoa kwa aibu na kugeukia vitambaa.
"Nanah" aliita Bieber kwa madeko akiwa nyuma yake na kuegemea bega lake moja.
Nanah aliondoka pale na Bieber alitabasamu kisha akamfuata.
Vitambaa vilisogezwa pale walipo na ilitokea sura iliyo vuta mdomo wake kuonyesha wazi amekasirishwa na maneno yaliyokuwa yakiongelewa na watu hao wawili.
Bob Risky alibaki akimtizama Nanah kwa hasira ambaye hakujua kabisa hilo.
Mbele walikukowa wakielekea Nanah na Bieber walikutana na Shalha aliyekunja mikono yake akiwatizama.
"Mmmhhh" Shalha aliguna na kuanza kumtizama Nanah juu mpaka chini.
"Yani kweli umeishiwa wewe, kwahiyo umeona mwanamke bora wa kuni replace naye ni huyu Bi Mkosi".
Nanah aligeuka na kumtizama Bieber kwa mshangao.
"Ooohhh haukufaham kwamba alikuwa mpenzi wangu kabla ya kaka yake kuwa mume wangu? So sad!!!".
Bieber alibaki akimtizama tu kwa macho ya kia ina na Shalha aliendelea.
"Ila siyo mbaya ni mzuri kidogo, kwahiyo unaweza kumchezea utakavyo ila najua moyo wako uko kwangu mimi kwasababu mimi ndo mwanamke wako wa kwanza. Mimi ndiye niliyekufundisha mapenzi ni nini na huwezi kunisahau kamwe katika maisha yako".
Shalha alizidi kubwabwaja na siyo Nanah wala Bieber aliyemjibu chochote kile.
"Ok uwe na siku njema Bi Mkosi, kama kuna mahali utakwama kuhusu Bieber njoo na uniulize mimi kwasababu nafahamu vingi sana kumuhusu".
Shalha alim busu Bieber kwa mbali na kuondoka akiwaacha.
Nanah na Bieber kila mtu alibaki akiwa amesimama vilevile yani ni kama walipigwa shoti.
Nanah ndo alijisikia vibaya wanaume wote ambao amewahi kuwapenda basi walishampenda mwanamke mwingine mmoja kabla yake.
Alishaanza kujihisi kumpenda Bieber japo hakuelewa kama anampenda au analipiza kisasi kwa Brown.
Bieber aligeuka na kuondoka pale pale akitoka njee ambako Shalha naye ameelekea hukohuko.
Nanah vimachozi tu ndo viliishia kumlenga na hilo lilimfurahisha Bob Risky japo alikuwa kwa mbali na hakusikia maongezi yoyote yale.
Alimfuata Nanah.
"Kuna nini?"
"Hamna kitu" alijibu Nanah kinyonge na machozi yakim dondoka aligeukia upande mwingine.
"Nanah!!! Kuna kitu bwana kwanini unalia?"
"Hamna" alisisitiza Nanah na kuondoka zake akitoka pale.
Bob Risky alitabasamu akimtizama kwa nyuma na aliamua kumfuata.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Kunywa hii itakutuliza"
Bob Risky alimpeleka hadi njee ya mgahawa ambao hupata wote chakula na hapo alim patia maji ya baridi.
Nanah aliyanywa.
"Haya niambie kuna nini?" Aliuliza tena Bob alitaka kujua kiliongelewa kitu gani na Shalha hadi kumfanya Bieber aondoke akiwa hana furaha usoni mwake huku Nanah akidondosha tu machozi japo kwa uchache.
"Hamna kitu Bob"
"Nanah, nilikuona ukiwa unalia huwezi kusema hamna kitu".
"Sikuwa nalia kuna mdudu tu aliingia machoni pangu"
Alijibu Nanah akiwa hamtizami kabisa Bob machoni kwani angemtizama angegundua kiasi gani Bob anakasirishwa na jibu lake la hamna.
'Sawa kama unahisi hatuna urafiki wa wewe kuniambia kitu gani kina kusibu"
Nanah aliinua macho yake na kumshika mkono Bob Risky.
"Nashukuru kwa kujali ila hakuna chochote niamini mimi".
Bob Risky aliweka tabasamu feki na kumshika mkono wake kwa juu.
"Nataka ujue ukiwa na tatizo lolote lile yupo mtu wa kukusikiliza na kukusaidia haupo mwenyewe hapa sawa?"
"Asante sana kiukweli nilihitaji maneno ya faraja kama hayo"
"Usijali Nanah utayapata mengi sana kutoka kwangu"
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Hivi mkeo umemuona?" Aliuliza Bieber alipomkuta Brown ofisini kwake na Shalha.
"Ahaaaa kumbe uko hapa tayari, hivi umemwambia mumeo ya kuwa leo umemwambia Nanah kabla ya kuwa na mumeo ulikuwa na mimi kwanza?"
"Nini? Amemwambia nini Nanah?" Aliuliza Brown hadi kuinuka kwenye kiti chake.
"Hahaha mkeo alikuwa akimuonea wivu Nanah, muda mwingine vyema umkumbushe yeye ni mkeo hapaswi kunionea wivu mimi ni shemeji yake" Bieber aliondoka na alipofika ofisini kwake hakuweza kumkuta Nanah.
"Ameenda wapi?" Alijiuliza na kutizama mahali anapokaa Bob na kiti kilikuwa kitupu.
"Boss" aliita Doy akiinuka.
"Nimeshaweza ku design gauni ninalo litaka" Doy alimuonyesha Bieber design yake na alimwambia.
Lizuri sana, approved litengeneze ila Doy unajua ume design vizuri sana jitajidi sana tena sana watu wasiweze kuliona.
"Usijali Boss kwasababu hilo ndo lengo langu nitaenda kulishonea nyumbani kabisa".
"Vizuri" alijibu Bieber.
"Eheeee alafu watu wengine wako wapi?"
"Ahaaa Kurwaa hayupo ametoka kidogo".
"Na Bob Risky?" Aliuliza Bieber ambaye alijua akimuulizia yeye ni sawa na amemuulizia Nanah kwasasa.
"Mr Handsome, umenimiss?" Aliuliza Bob akiwa amesimama mlangoni na ame uegemea mlango kwa madoido.
"Aaaa upo mwenyewe kumbe".
"Hapana nilikuwa na Nanah, hajisikii poa hivyo nimemuombea ruhusa ameenda nyumbani. Amekataa hata nimsindikize"
"Hajisikii poa? Anaumwa na nini?" Aliuliza Bieber akimsogelea Bob na kujikuta amemshika mkono.
Bob alitabasamu huku akimrembulia.
"Hajaniambia chochote but analia"
"Basi sawa natoka kidogo" alijibu Bieber na kuondoka zake
Bob alilamba lipsi zake huku akimtizama Bieber kwa nyuma huku akirembua kwa mbali.
Bieber alipanda tax na kuondoka pale.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Kilisikika kibao kilichotua shavuni mwa Shalha.
"Kilikuwasha nini. Nakuuliza kilikuwasha nini mpaka ukamwambia Nanah ya kuwa ulishawahi kuwa na mahusiano na sisi wote wawili?"
"Brown umenipiga"
"Of course yes au nikupige kingine?" Aliuliza Brown akinyoosha mkono wake
"Nimejitahidi kuficha huo uchafu wako ulioweza kuufanya miaka ya nyuma lakini naona sasa unajifanya mwamba na kujitangaza mwenyewe sindiyo?"
Shalha alibaki akimtizama tu.
"Aise kaa mbali na yule mwanamke kaa mbali naye Shalha. Nimevumilia upuuzi wako wote ila usinijaribu kwa Nanah kwasababu hata wewe unatambua we sisi chochote kwangu mbele ya Nanah"
Itaendelea In Shaa Allah.