Nikashangaa ananipeleka sehemu moja kama restaurant, ilikuwa imeendikwa chiken fish, kisha akaagiza kuku wa tatu na chips..
Baada ya kama nusu saa wakaletwa kisha akasema "sikuwa najua kama sophy unapenda chips sana, hata kuku hao apo na chips naomba ule na umalize..
Nikashangaa maana sikumuambia kama nilikuwa na njaa, na walam sikuwa nataka kula kuku mimi, sasa sijui ni nani ambae alimuambia kuwa nina shida na kuku na chips zake, akajua kabisa kuwa sikuwa nataka kula hivyo akaniambia tena kuwa “ kuku na chip hao hao unatakiwa umaliza, na utanambia kuwa unataka kunywa na kinywaji gani…
"Mimi sina njaa nashkuru, nikajibu...
"Usitake kunitania wewe mwanamke, kula laa sivyo nitabadilisha mada, yaan wanaume wengine wakikununulia unakula ula mimi mumeo hautaki, naomba ule kabla sijawah mtu mwingine muda sio mrefu akaanza kusema na kiukweli najua akili zake na sikutaka kuendelea kubishana nae ,sikutaka aje kunifanyia mambo ambayo alishanifanyia siku chache nyuma, hivyo kwa unyonge nikaanza kula.
Kweli nilimaliza kuku mzima, sikula chips wala kinywaji maana niliamin huenda ikasababisha nikashindwa kula, ila nilikuwa nimeshashiba, kwa binti kama mimi kumaliza kuku mzima haikuwah kuwa kitu rahisi kabisa..
Basi bana baada ya kumaliza nikamgeukia na kumuambia " mimi nimeshiba, kwa sauti ya unyonge sana ..
Akacheka kisha akanambia " najua unapenda sana chips kuku ndio maana unakubali kubali kizembe offer za wanaume wengine, mbona mimi huwa nakuhudumia vizur sana au ndio hauridhiki, au huduma zangu ndio hazina maana kabisa kwako...
" Umeshawah kunihudumia nini wewe, labda huduma pekee ambayo nimeshawah kuipata kwako n kero na kukosa furaha tu, na kuniharibia maisha yangu, kama hautajali naomba uachane na mimi, maana sina muda wa kupigishana kelele na wewe hata mara moja, nikajikuta nimejibu kwa kupanic sasa..
Akacheka kisha akanambia " mambo mengine tutaongea muda ukifika ila hakikisha unamaliza hicho chakula...
Nikaanza kula na wakati huo kelvin alikuwa ananiangalia kwa hasira sana, nikasema eheee kimenuka sasa..
Ila hata kama nipambane kiasi gani, ukweli ni kwamba siwez kumaliza kile chakula hata iweje, na yueye mwenyewe anajua kuwa uwezo wa kumaliza sina ila ananifanyia kusudi tu, nan i kama alikuwa anataka kunikomoa..
Nikashindwa maana nilikula mpaka nikaona sasa chakula kinaelekea kwenda kuziba pumzi, maana sehemu ya chakula imeshajaa...
Nikamuangalia kisha nikamuambia kuwa nataka kwenda nyumban..
Hata hakukataa akasimama na kunambia kuwa atanipeleka, nguvu ya kubisha pia sikuwa nayo tena..
Basi akanirudisha mpaka nyumban, kiukweli chuki na hasira zangu kwake ndio zikazidi mara dufu, maana niliona kama ni shetan mwenye umbile la kibinaadamu ila ana roho ya kishetani, ila kumbe mwamba kanielewa na anachokufanya ndio kama namna ya kufikisha upendo wake kwangu, ila ubabe na kuforce mambo ndio tabia yake, hajui kutongoza na mara zote huwa ananunua wanawake, na kama tunavyojua wanawake wa kununua huwa wanaangalia pesa tu, hawaangalii wewe ni romantic kiasi gani, maana hilo wao haliwahusu hata kidogo.
ITAENDELEA…
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments