Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

Simulizi.. ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚. Mtunzi.. Sehemu ya 11.

19th Jul, 2025 Views 10

Simulizi.. ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚.
Mtunzi..
Sehemu ya 11.

Mimi na Brown tulienda hadi kwenye hotel na nikaagiza pembo sasa mtoto wa watu, nikaanza kunywa nilikunywa mpka nikawa chakali kabisa sasa nikaanza kuongea, huku nikimtukana sana allen muda huo Brown ananiambia tuondoke yani hapo mimi sielewi chochote nataka tu niendelea kulewa basi.

"Brown, hii ya mwisho sawa niache tu nimalizie hii jamani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚"

"hapana Anipha, amka twende nyumbani sawa umelewa sana"

"Sawa nitaenda nyumbani lakini, usinipeleke kule aliko Allen sitaki kabisa kumuona mwana haramu huyo 😑😑😑"

"sawa amka sasa twende"

Ile naamka tu kwenye kiti nilianguka nyie mpaka nguvu za kusimama zikaniisha, Brown akanibeba hadi kwenye gari lake Baada ya hapo sikujua kitu chochote tena, mpaka asubuhi nakuja kuamka nashangaa tu, maana hata sjui ni wapi jamani.

"Sasa hapa ni wapi jamani na mbona nguo sio hizi nilizokuwa nimevaa jamani eeeh, aah mbona kichwa kinauma hivi jamani"

Muda huo huo Brown alifungua mlango na kuingia ndani akiwa na bakuli yenye supu na chapati mkononi.

"hivi hali anipha, unajisikije"

"kichwa tu Ndio kinaniuma na mbona nipo kwako kwa nini??"

"jana ulikataa kwenda kwa Mainda kwa sababu hukutaka kuonana na Allen"

"daaaah sasa Ndio nimefanya nini mimi jamani sawa, wacha nioge niende nyumbani"

"jamani Anipha, kula kwanza Ndio ujiandae sawa me nitakuwa hapo nje nakusbiri sawa"

"sawa Brown asante"

Nilikula kile chakula haraka haraka baada ya hapo nikaingia bafuni kuoga nikarudi chumbani hapo nawaza navaa nini sasa jamani mimi daah, Mara Brown akagonga mlango.

"Anipha, fungua kabati kuna nguo humo sawa"

"sawa"

Nikafungua kabati la nguo humo chumbani nilikuta nguo nyingi sana kwenye lile kabati nikachangua nguo moja nikavaa chap chap nikatoka sasa ili niendee nyumbani.

"Brown, twende sasa"

"sawa mama twende"

"lakini Brown mbona unangua nyingi hivi za kike ni za nani??"

"πŸ˜‚πŸ˜‚, Anipha hizo nguo Ndio zile nilizonunua dukani kwenu siku ile, zilikuwa zako yani nilizinunua kwa ajili yako wewe hapo"

"Aaah sawa, asante"

Majibu ya brown yalinifanya nijiskia vibaya sana maan sina hata mpango wa kukubali kuwa mpenzi wake daah sjui hata nafanyaje sasa jamani mimi. Tulifika hadi nyumbani kila mtu akiwa kimya kabisa.

"asante sana Brown"

"usijali Anipha, badae ngoja mimi niende kazini"

"sawa kazi njema B"

Brown aliondoa gari maan hakuingia hata ndani aliishia getini na mimi nikaingia ndani, ile naingia tu ndani nakutana na Allen mlangoni.

"Samahani naomba kupita"

"unatoka wapi asubuhi hii, maana yake ni kwamba hukulala nyumbani"

"khaaa, wewe ni nani mpka uniulize hivyo yani πŸ˜‚πŸ˜‚"

Nilimjibu hivyo Allen kisha nikaondoka kwenda chumbani kwangu nikapishana na Tanasha mimi hapo niko busy mpka chumbani kwangu.

Itaendelea...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Simulizi.. ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚. Mtunzi.. Sehemu ya 11.  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-anipha-mtunzi-sehemu-ya-11
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest