Dar es salaam bandarini wanashuka watu kwenye boti wanaelekea kituo cha mabasi ya mwendo kasi abiria wanasubiri basi kuelekea mwembe chai
Abiria wanashuka muembe chai wengine wanaelekea katika mabasi kwa ajili ya safari ya Kampala Uganda
Kuna wanaonunua vyakula maji kwa ajili ya hakiba ya safari
Mizigo inatiwa sehemu maalum Wanafunzi wanaingia ndani ya basi kila moja anakaa kutokana namba yake ya kiti safari inaanza kuelekea Uganda
Tunapita mkoa hadi mkoa baadhi ya vituo Tunasimama kwa ajili ya kuchimba dawa na kupata chochote kwa ajili ya kula
Tukimaliza safari inaendelea... muda wa siku mbili ndio tunawasili mpakani tunashuka kwenye basi tunaingia uhamiaji mizigo inakaguliwa
Nasisi tunagongewa muhuri katika hati ya kusafiria kuna Mtanzania pia tunakaguliwa na Mganda
Tunachenjisha pesa palepale mpakani zoezi linamaliza tunaanza safari ya kuelekea Kampala Uganda
Chuo kikuu cha Kampala
Tunafika jioni tunashuka na mizigo yetu tunaingia ndani katika mabweni wanaume yao na wanawake yao yametenganishwa na barabara
Kila mtu anapandisha mizigo yake juu katika vyumba Tunaenda kufatia godoro
Kutoa uchovu naingia chooni kujitia maji navaa nguo yangu natoka nje saa kumi na mbili tayari wakati wa kugaiwa chakula unapanga foleni kama tupo loliondo kwa babu kikombe
Waganda wana foleni yao na Sisi watanzania tuna foleni yetu
Inafika zamu yangu natiliwa chakula kila kitu umoumo kama bata wali sembe maharage utajijua π€£
Narudi zangu bwenini kwetu chumbani tunakula na wenzangu mapishi tafauti na kwetu chakula hakina samaki
Siku nyengine tunapikiwa matoke ndizi zinachemshwa zinapondwa π
Siku za skukuu ndio mnapikiwa supu ya nyama na kuku
Asubuhi mnapikiwa chai au uji kitafunwa mtajijua wenyewe
Nje kunauzwa mihogo apo ndio kijiweni tunakutana watanzania ndio hoteli yetu ya nyota tanoπ
Bweni letu la wanaume horofa ya juu ukisimama unaona wanapofua na kuanika nguo wanawake
Natupa jicho kama masihara nataka kuligeuza linagoma moyo unanishawishi muangalie vizuri
Toto la kiganda amevaa taula yakufutia maji imeanza kifuani imeishia kwenye mapaja
Mrefu kiasi ana nywele za Kiafrika nyingi nyeusi refu uso wa mviringo
Shingo refu kama twiga kasiringana kiuno na hipsi miguu minene ana rangi nyeusi ya kungara
Kila nikitaka kugeuza shingo moyo unakataa
Mtoto kavaa taula anafua na kuanika nguo mapigo ya moyo yanapiga kwa kasi
Usiku wakati wakujipumzisha taswira yake inanijia kila nikifumba jicho
Kumekucha anaamka usingizini la kwanza kukumbuka taswira yake sitamani kuamka kitandani lakini imenilazimu kuamka
Tunanaanza pirika za kufanya usajili kulipa ada pamoja na kukutana na walimu mimi nachukua stashahada ya IR (international relations) uhusiano wa kimataifa
Tunaanza masomo rasmin mchakamchaka
Chuo tulichofikia cha manesi na Daktari walikuwa ni kipindi cha kufanya mitihani
Mnajua penzi likeshaingia kwenye moyo linahangaisha nikaanza kuhaha natamani kumuona mganda kila wakati
Asubuhi kabla ya mtihani wanakaa paredi jicho linamsaka kila kona linatulia ninapomuona mtoto katulia kuanzia kichwa hadi unyayo
Chuoni kuna bustani watu wanakaa kusoma mkufunzi anatusomesha upo mwili akili haipo jicho lote kwa toto la kiganda mpaka mdomo nimeachama denda linanitokaπ€£
Nashtuka wenzangu wananiita oya vipi mwamba najibabaisha mkufunzi ananitizama kwa mashaka
Tunamaliza kusomeshwa uzalendo unanishinda namfata bonge la dada π
Samahani naomba tuzungumze mtoto ananiangalia jicho regerege la kike hasa mimi hoi msela
Analeta pozi namshika mkono tafadhali anautoa mkono mbio unamhisi kama mtu alopata shoti ya umeme
Ananitolea macho anajitahidi kukaza lakini unaona kabisa hali siyake
Anataka kunyanyuka nakaa kwenye kiti naibana mikono yake kwenye meza asinyanyuke
Uganda Queen anaangalia kila upande kama watu wanatuona au hawatuoni mimi ata sijali nijili moja maulidi ya bwana mtumeπ€£
Sauti yangu naiyona imebadilika hafla inanguruma kama simba yupo mawindoni macho yetu yanakutana Uganda Queen anatulia ananisikiliza kidume natema nyongo
Tafadhali nisikilize mtu hakatai wito anakataa analoitiwa tangu nikuone sijui kimeniingia nini katika moyo wangu Ugandan Queen
Natamani nikuone kila wakati inanijia taswira yako unaitwa nani ananitumbulia macho hajibu kitu
Mara anakuja mwanafunzi mwenziwe anamuita Sara twende tukasome napata kufahamu jina lake anaitwa Sara
Sara ananyanyuka anaongozana na mwenziwe namimi namsindikiza kwa macho najipa moyo kama kavutika namimi nitaona ishara
Sara wanafika mbali kidogo karibu wanataka kupinda anageuza uso ananitizama anatabasamu
Sara meno yake yamepangika vizuri meupe akicheka anabonyea mashavu. Ananiacha hoi mtanzania mimiπ
Sara anataka kujikwaa mwamba nanyanyuka haraka naita Sara watu wanageuka wananitizama
Sipepesi macho Sara anasaidiwa na rafiki yake ananyanyuka anajiweka sawa anageuka tena ananitizama anatabasamu
Nahisi amani ya moyo namimi namrejeshea tabasamu
Tunapokutana sehemu huwa tunaanzisha marafiki wapya, chuoni kuna mshkaji tunasoma kada moja tunazoena anakuwa ndio rafiki yangu
Nje ya chuo kuna muuza matunda pia anakuwa rafiki yangu nikienda kununua matunda tunapiga stori mbili tatu siku zinaenda
Kila nikimfukuzia sara ananiringia lakini mwamba sikati tamaa
Nimekaa bwenini Sara anapita chini barabarani bahati nzuri nimekaa kwenye dirisha naona mtu anaangalia juu nilipo
Namimi jicho lote kwake kwenye nafsi yangu ipo siku nitakutia mikononi Sara utakuwa wangu mama watoto
Rafiki yangu ibra anakuja karibu yangu oya Vipi nakuona hujijui kwa yule demu unamjua mtoto wa kizito baba yake ndio mwenye chuo hichi vituo vyote anamiliki yeye
Najikuta nacheka sana rafiki yangu watoto wa kizito hawana moyo hawapendi
Ibra anasema kwa msisitizo mimi nakutahadharisha anae kwambia anakupenda tafuta vinuka mkojo wenzio kina mwajuma machupiπ€£
Sawa nimekusikia ila nitahakikisha mpaka anakuwa mama watoto hata kama mtoto wa raisi
Mimi nimempenda kwa nia safi kuamini nguzo marufuku kukata tamaa
Ibra umekuwa sharukhan na filamu ya koila kila la kheri ukikumbana na Amrishpuri mimi simo nakukana kabla jogoo halijawika
Sawa mkuu niachie mimi nimelianza namaliza mwenyewe mchezo mzima
Ibra anaguna hmm jifanye shujaa legendari uambulie Asante kama majeshi enzi izo
Manzi kama wale tunakula kwa macho basi tunawamezea maji funda la mate tunawaachia wanaomiliki nchi
Wewe unajifanya ukawa mkaidi ohoo kita kukuta kitu
Sawa tulale nimechoka risala gaazeti kubwa fupisha nakesho nayo siku
Watu wote washalala mimi sijapata hata lepe la usingizi nawaza maneno alonambia mshkaji mazito
Namimi nishajiingiza kwenye mtumbwi wa vibwengo
Najipa moyo hakuna kurudi nyuma CCM mbele kwa mbeleπ
Naamka nachungulia dirishani naona upande wa jengo la wanawake chumba anacholala Sara na wenziwe taa haijazimwa
Sara anatoka mpaka varanda kavaa nguo ya kulalia kibukta na topu juu jicho limenitoka pima natamani nimfate lakini naanzaje kwa mfano
Sara anageuka ananiona tunatazamana anashtuka anabetua midomo anaingia chumbani mbio
Narudi kitandani nahisi hisia mchanganyiko nawaza uzuri wa sara nawaza maneno ya muhuni π kanambia ukweli mtupu kanipiga mabapa ya mapanga kisawasawa
Asubuhi mapema naenda kuchukua chai tunakutana na Sara tunagongana Sara anakasirika angomba ukienda huangalii mbele
Mimi sina la kusema nakuwa kimya naangalia tu uumbaji wa mungu mtoto anamidomo mizuri unatamani umpige busu
Sara anachukua chai anaondoka nimetulia namtizama anavyotembea mpaka anapotea machoni
Nachukua chai napasha uchango kwa maji ya moto tayari kupiga kitabu
Tunafanya kazi za vikundi majadiliano tunawasilisha mada mtu moja moja mbele imefika zamu yangu unajua uwoga wakusimama mbele ya hadhira ya watu
Nasimama naanza kuwasilisha mada tulopewa katika kikundi chetu Sara anatokezea napata ujasiri sijawahi kuwa nao
Nawasilisha mada jicho lote lipo kwa Sara nahisi kama hapana mtu tupo mimi na yeye tu
Mpaka namaliza namuona Sara anapiga makofi natabasamu nasikia kofi za wengine ndio nahisi uwepo wao
Mapenzi yana nguvu sana unaweza kufanya vitu ambavyo hajawahi kufanya maishani inategemea uko upande upi wa mapenzi hasi au chanya
Ukiwa katika mapenzi chanya unakuwa na furaha kila wakati
Katika kazi za maendelo unakuwa mstari wa mbele kwenye masomo utafanya vizuri
Una utulivu na amani unaweza kushiba bila ya kula unanawiri unaridhika na vitu vidogo
Unajitoa sana kwa watu unakuwa mwenye kutatua changamoto za wengine
Unajali unathamini umpendae pamoja na watu waliokuzunguka
Unanguvu ya ndani na nje inayokusukuma kuwa na ubinaadamu kwa sababu ya kupata unachokipenda
Mapenzi yakiwa hasi unayempenda hakupendi au umependa sehemu sio sahihi
Unakosa kujiamini unajiona mkosefu unaanza kujitoa kasoro unakuwa na huzuni
Inaathiri ufanisi wa kazi unyong'onyevu wa mwili na akili
Hasira unajichukia wengine huenda mbali huona hawana sababu ya kuishi na kuondoa uhai wao jambo ambalo sio sahihi
Kukataliwa sio mwisho wa maisha kuna vitu tunavipenda lakini havina kheri nasi
Tujifunze kuto kuendekeza nafsi isitupelekeshe
Kusubiri muhimu pindi unapopata jawabu lahapana
Using'ang'anie usipopendwa unapoteza wakati
Hamisha ufanisi kwenye kazi wekeza nguvu zako kwa anaekupenda ili umsahau unaempenda
Kuna mtu tayari yupo kwa ajili yako Anasubiri utupe mshipi anase mazima.
Penda unapopendwa ridhiya utafurahia maisha
Sara wanamaliza mitihani wanataka kuondoka situlii nawaza akiondoka itakuaje sijazungumza nae
Napata wazo namtumia rafiki yake, nampa barua utafikiria tupo shule ya msingi 9100 π
Habari yako Sara
Natumai umzima wa afya
Sara naandika barua hii matumaini yangu utaisoma na kuzingatia
Ugandan Queen naomba tuonane nina jambo muhimu nataka nikwambie
Tafadhali usikatae wito kataa utachoambiwa
pia zingatia kama kitakuwa hakina dhara na chenye kuleta faida usikatae
Mimi Omar
0778955701
Sara anamaliza kusoma barua anatabasamu anatafuta sehemu iliyojificha ametulia anaingiza namba anapiga simu
Nimekaa najisomea chumbani nasikia mlio wa simu natizama namba ngeni naipokea mbio
Upande wa pili nasikia sauti ya kike Assalam Alaykum warahmatullah wabarakatuh
Naitikia Waalaykum Ssalam warahmatullah wabarakatuh
Sara anajichekesha nimeitikia wito Omar
Najipa moyo naamini kama mtoto kakubali kuzungumza nami ishara tosha kuwa kashaanza kunielewa kilichobaki kugongomelea misumari vizuri
Nazungumza kwa hisia Sara naomba tukutane juu ya mlima tafadhali saa kumi jioni
Sara anaitikia sawa Omar anakata simu
Nahisi furaha mpaka natetemeka mara nikae mara nisimame naisevu namba ya Sara Ugandan Queen
Je! Sara atakwenda juu ya Milima?
Hii simulizi mpya nitakuwa natuma kwenye ukurasa wangu tu
muendelezo followππ
Simulizi Za Mpemba OG
0778955701
...............