Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 08

1st Aug, 2025 Views 20



ENDELEA.......
"Shindwa pepooo!" Anjeli aliongea huku akimsukuma Osman.

"Kwanini unanifanyia hivi!...kwani sina vigezo vyovyote" Osman aliongea huku akitetemeka, hisia zake zilikuwa juu sana...kama siyo mazingira ya ofisini huenda angebaka kabisa.

"Naweza kuwa Dada poa lakini kama Mteja aliye mbele yangu anakuwa hana vigezo huwa namsukuma kule kwendaaaa!" Anjeli aliongea.

Osman anajichekesha kimtindo huku akiwa anahisi aibu kwa kukataliwa.

"Kaa hapo nimalizie kazi yangu kisha twende Supermarket kuna mzigo nataka umpelekee Mama".

Anjeli alijitupa kwenye kochi kisha akakaa.

"Kwahiyo wewe ndio CEO wa hili Kampuni?" Anjeli aliuliza.

"Ndiyo"

"Magodoro yenu mnayo tengeneza ni ya kishua sana si rahisi kwa mtu wa hali ya chini kama Mimi hapa kununua, vipi mnapango wa kutengeneza godoro za bei ya chini kabisa" Anjeli aliuliza.

"Ndiyo.."

"Nina uhakika mtatengeneza godoro zinazodumu miaka 7 na kuendelea au unasemaje".

"Ndiyo..."

"Ndiyo ndio nini batamzinga wewe, Mwanaume unatakiwa uwe na uwezo wa kuzungumza sentensi ndefu walau wenye maneno mawili na si ndiyo tu" Anjeli aliongea.

Asha anaingia akiwa kabeba matunda, ana shangazwa na pozi alilokaa Anjeli.

"Hii ni ofisi jitahidi kukaa vizuri" Asha alikumbusha.

Anjeli alikaa kwa heshima, matunda yaliwekwa mezani.

"Godoro 20 zimeweza kuzalishwa, kabla hawajazalisha idadi kubwa ni vyema kama ungeenda kukagua" Asha alishauri.

"Nitafanya hivyo baada ya kurejea kutoka Supermarket, muambie Victor awazuie kuongeza idadi nyingine kwanza...." Osman aliongea.

"Ni gari lipi utalitumia kwenda supermarket...." Asha aliuliza.

"Nitapanda bajaji, huna haja ya kunifuata" Osman alitoa jibu lililofanya Asha ajisikie vibaya, alimtazama Anjeli kisha akaondoka.

Baada ya Osman kumaliza kazi yake, aliondoka na Anjeli.

"Nini kimetokea leo unaachwa!" Victor alimuuliza Asha kwa mshangao.

"Una kumbuka ile siku tumempeleka Boss Dodoma?" Asha aliuliza.

Victor alitikisa kichwa kuashiria ndiyo

"Ule usiku aliopotea alitembea na Anjeli....huyo binti ni Dada poa, sielewi kwanini kawa Mfanyakazi nyumbani kwa Sabrina" Asha aliongea.

"Muda mwingine ujifunze kuwa una amini mawazo yangu, kama usingeshauri Boss aende Dodoma sidhani kama angeishia mikononi mwa Dada poa. Sitaki kuwa muongo kwako lakini huyo Binti ni kisu.... wewe na Hilda hamuoni ndani" Victor aliongea.

Asha aliachia ngumi ikapasua mdomo wa Victor.

"Ipo siku maneno yako yatakuweka kwenye jeneza...." Asha aliongea kisha akaondoka.

Victor aliishia kujipangusa damu, kuna namna ana mhurumia Asha kwa sababu Osman ana mtazama kama Mlinzi na si vinginevyo.

Osman akiwa na Anjeli supermarket, alionekana kuwa na furaha zaidi kuliko hata anavyokuwa na Hilda.

Kuna mtu alionekana kuwapiga picha japo ni kwa siri sana.

Asha akiwa ametulia alitumiwa picha hizo, hakutaka aumie pekee yake alimtumia Hilda pia.

Hilda akiwa anakata kucha zake alishtuka sana baada ya kutumiwa picha hizi na Asha.

Alishika simu akampigia,
"Nini maana ya kunitumia hizi picha!... Mume wangu ni mtu anayejiheshimu hawezi kufanya ujinga unaofikiria wewe".

"Mwanaume ni sawa na sukari kwenye chai....nimekutumia hizo picha kama tahadhari tu, pengine ulikuwa hujui lakini Anjeli ni Dada poa aliyetembea na Osman kabla hajaitwa Mumeo." Asha aliongea kisha akakata simu.

Hilda alihisi moyo wake ukikandamizwa na kaa la moto...................FULL STORY/MUENDELEZO MPAKA MWISHO 1000 TU. KARIBU KULIPIA KWA NAMBA 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 08  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-dada-poa-wa-usiku-mmoja-mtunzi-nuru-halisi-sehemu-08
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest