Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 11--12

1st Aug, 2025 Views 21



ENDELEA......
Matarajio ya Anjeli yalikuwa ni sahihi, Osman alimpitishia ujumbe chini ya mlango.

"Naomba tutoke kuna kitu muhimu sana nimeandaa kwa ajili yako, nipo nje ya nyumba nimekusubiria" Ujumbe ulisomeka.

Anjeli alivaa nguo yake anayoipenda kuliko zote, alijua pindi atakapo ondoa mguu wake mahali hapa hatarudi tena.

Osman anaachia tabasamu baada ya kumuona, kwa pamoja waliingia kwenye gari.

"Unaonekana unapenda sana vitu vizuri, sikuwa nimelijua hili. Huenda ningeshauiba moyo wako siku nyingi" Osman aliongea.

"Inaonekana wewe ni mvivu sana kutongoza, sikushangai.... Wanaume wengi wenye pesa huwa hawajui kuongea. Hupenda kuitegea pesa ndio izungumze...." Anjeli aliongea.

Osman aliishia kuachia tabasamu kwa maneno aliyoelezwa.

Waliingia kwenye hoteli moja ya Kifahari, Anjeli aliachia tabasamu la uongo baada ya kupatiwa zawadi ya simu kubwa pamoja na funguo ya nyumba aliyompangishia

"Inaonekana hujafurahishwa na zawadi zangu" Osman aliongea, ni Mtaalamu wa kutofautisha tabasamu feki na halisi.

"Ningefurahi zaidi kama ungenipatia na kibunda cha pesa...." Anjeli aliongea.

Osman alimhesabia pesa nyingi ambazo hajawahi kuzishika na hatakaa azishike.

Hakuona sababu ya kukibania kiuno chake....alijituma ipasavyo. Lengo lake lilikuwa ni kumchosha Osman ili atakapo lala, alale fo fo fo.

"Kweli nina malengo na wewe..." Osman aliongea akiwa kachoka sababu ya mzagamuo aliopatiwa

Anjeli hakuwa tayari kusikia kuhusu malengo ya Osman juu yake kw sababu hakuwa na nia ya kukaa Mwanza tena.

"Nimechoka sana, kama utaniambia sasa hivi sitakuelewa. Kwanini usisubirie kupambazuke" Anjeli aliongea akijitia kachoka.

Osman hakutaka kumkwaza, walizima taa wakalala. Usiku wao ulikuwa wa kipekee sana kwa sababu walilala kwa uhuru utadhani ni Mume na mke.

Upande wa Hilda akiwa chumbani kwake aliandaa sumu kali kwa ajili ya Anjeli.
Si mtu wa kusamehe mara mbili, msamaha alioutoa mara moja ulitosha kuonesha ubinadamu wake.

Hali ya moyo wa Asha akiwa chumbani kwake ilikuwa ni mbaya, alilia mfulilizo bila kukoma.
Maneno aliyoambiwa na Osman wakiwa ofisini yaliumiza moyo wake kuliko kitu chochote.

Si mtu wa kutumia pombe kali Kupita kiasi lakini siku ya leo aliamua kunywa akiamini atatuliza akili yake.

Kulivyo pambazuka asubuhi, Osman anashtuka baada ya kujikuta amelala pekee yake.

Zawadi ya simu pamoja na funguo kwa ajili ya nyumba aliyompangishia zilikuwa mezani.
Pesa pekee ndio zilisepa na Anjeli.

Osman alielewa maana ya yote haya, moyo wake ulimuuma sana kwa sababu alijua huyu kichaa ameondoka.

Alikusanya nguvu zake zote akapanda gari....
Muda wa kwenda kazini ulikuwa umewadia hakutaka kwenda nyumbani alielekea ofisini.

Asha na Victor walikuwa wamemsubiria, baada ya kumuona walimkaribia.
Asha alitaka kuuliza kama yuko poa lakini baada ya kuona Victor kavunga kama haoni kitu yeye pia hakuuliza.

Osman alikuwa bize sana siku ya leo, alijitahidi kusahau kuhusu Anjeli lakini moyo wake ulimsaliti.

"Naomba uende stendi kuu, hakikisha unafatilia kwa kina kuhusu Anjeli. Nataka kujua amekata tiketi kwenda mkoa upi....sina uhakika kama atakuwa ameenda Dodoma" Osman alimuagiza Victor na si Asha.

Victor aliondoka akiahidi kufanya kazi kwa ufanisi.
Asha hakutaka kuuliza kwanini hajapatiwa hiyo kazi yeye..

"Nampenda Anjeli, naomba uniambie ni mbinu gani niitumie kumuoa bila kumuumiza Hilda" Osman alimuuliza swali Asha.

Asha hakujali macho ya watu, alimkumbatia CEO Osman baada ya kuona anateseka kupita kiasi sababu ya Dada poa..................

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 12

ENDELEA......
"Naomba uniambie kitu kinacho sumbua akili yako" Asha aliuliza ilihali anajua.

"Jaribu kuishi kama Mlinzi wangu na si Mama yangu!" Osman aliongea kwa ufupi kisha akaondoka.

Asha alijisikia vibaya kwa jibu alilopatiwa.
Hakutarajia kama ipo siku Osman atabadilika sababu ya Dada poa.

"Anjeli kaelekea Morogoro...." Victor anarudisha jibu baada ya kufuatilia kazi aliyopatiwa.

"Ahsante kwa kazi yako nzuri" Osman aliongea kwa ufupi.

Victor aliondoka bila kuuliza chochote, hii ilizidi kumuongezea sifa kwa Osman kama Mlinzi anayejua mipaka yake ya kazi.

Wakati anaelekea kwenye gari alikutana na Asha.
Mara nyingi ni watu wa kuvutana sana, kabla Asha hajaachia ngumi mkono wake ulidakwa.

"Kitu gani kinaendelea....naomba kujua kwanini ulienda stendi kufuatilia kuhusu Anjeli! usiniambie Osman anataka kumfuata huyo punguani" Asha aliongea.

"Kazi yetu sisi ni kuzuia risasi isipenye kwenye mwili wa Osman, kuhusu hisia za moyo wake si kazi yetu kujua!" Victor aliongea.

"Naelewa una zungumza mengi na Sabrina kuhusu Osman.... natamani kujua pia kila kitu kuhusu CEO kwanini unanificha!" Asha alifoka.

Victor alimkunja, alimsogeza kwa ukaribu kabisa

"Osman anampenda Anjeli lakini ana mheshimu Hilda"

"Una maanisha nini kusema hivi"

"Huna nafasi katika moyo wa Osman....sehemu yako ipo katika ubongo wake, kubali matokeo tofauti na hapo kibarua chako kitaota nyasi. Kosa lako ni kuishi kama Sabrina kwa Mwanaume ambaye hukumuweka tumboni....".

"Kwahiyo upo tayari boss atembee na yule Dada poa!".

"Nachojali Mimi ni usalama wa Osman na si kufuatilia kuhusu umbile lake lina mzagamua nani na nani...." Victor aliongea kisha akaondoka. Asha aliishia kurekebisha koti lake.

Upande wa Anjeli, baada ya kufika Morogoro alianza kutafuta kazi huku na kule.
Muonekano wake ulikuwa kikwazo cha Mama mijengo kumuamini.
Alijikuta akitumia siku nzima bila mafanikio.

"Mdogo wangu tafuta tu biashara yoyote ndogo ufanye... muonekano wako ni tishio kubwa kwa wake za watu. Usalama wa ndoa zao huenda ukaingia hatarini kama watakuweka ndani kama Mfanyakazi...." Mwanamke mmoja alimuambia Anjeli.

"Naomba unisaidie ni kitu gani nifanye niweze kutoboa maisha....nina kiasi kidogo cha pesa nipe akili tafadhali".

"Biashara ni ngumu sana siku hizi, kwa muonekano tu hauna leseni ya biashara....hiyo pesa uliyonayo itapukutika tu bila taarifa. Kuna Casino moja jipya limefunguliwa hapo ng'ambo mpaka sasa halina Wafanyakazi....kwanini usiende kuomba hapo kazi. Uzuri wako ni kigezo tosha huna haja ya kuchanganyikiwa.....pesa uliyonayo itumie kutafuta chumba cha kishua, kisha inayobaki weka akiba".

"Sina uhakika kama nitaiweza hiyo kazi" Anjeli alijitia mlokole.

"Mji.....nga wewe, macho yako yanaongea ukweli kuwa hii kazi iko ndani ya uwezo wako, Mimi pia nilikuwa kama wewe mwisho wa siku nilipata Mwanaume anayenipatia mshahara wake wote.....jitahidi kuwa mgumu na si kujirahisha kwa kila Mwanaume utakuja kunishukuru".

Anjeli hakuwa na namna, alijipiga kifua akaenda kwenye Casino linalojulikana kwa jina la Blueberry.

Msimamizi wa Casino hili alimpima kwenye mizani yake kwa umakini mkubwa.

"Umekidhi vigezo vyangu kwa asilimia 95.... karibu sana"

Anjeli aliachia tabasamu pana baada ya kusikia amepata kazi.
Ndani ya nusu saa tu aliweza kubadilika...alipatiwa sare kisha akaelekezwa vitu anavyotakiwa kufanya.

Uzuri wake ulimlinda na hata akapatiwa gheto la bure.

Ni wazi Msimamizi alihitaji kumuweka karibu asije kuondoka, aliamini kupitia Anjeli kuna namna atakuwa anapata faida pia.

Mida ya Usiku Osman anarejea nyumbani, muonekano wake ulitosha kumueleza kila mtu kuwa hayupo sawa.

"Nifuate chumbani kwangu nina ujumbe kutoka kwa Shangazi yako" Sabrina aliongea kisha akaelekea chumbani.

Osman alimfuata tayari alijua ni jambo gani anaenda kuambiwa.

"Weee mpuuzi sitaki kuamini unataka kuchanganyikiwa sababu ya Anjeli....kwanini unanifanyia hivi!" Sabrina alifoka

"Naamini ulimuajiri Anjeli hapa sababu ya uzuri wake....huo huo uzuri uliokuchanganya wewe ndio umenichanganya Mimi pia naomba uniache nifuate nini moyo wangu unataka" Osman aliongea.

"Ni kweli yule Binti ni mrembo lakini ulipaswa kufanya uhuni wako kimya kimya! kosa lako ni kuifahamisha hii nyumba yote kuwa wewe ni muhuni...Endapo utaendelea kuonesha maumivu yako mbele yetu nitafanya maamuzi yatakayo kuumiza maisha yako yote" Sabrina aliongea kisha akamtimua Osman.

Upande wa Hilda akiwa amekaa bustanini Asha alimuijia.

"Nina uhakika muda si mrefu utaambatana na Osman kwenda kumtafuta Anjeli, kuna kazi nataka unifanyie.....endapo utaifanya kwa usahihi nitakupa ruhusa ya kutembea na Mume wangu kwa usiku mmoja." Hilda aliongea na kumfanya Asha ashtuke.

"Una maanisha nini kusema unipe nafasi ya kutembea na Osman"

"Acha kujitoa ufahamu, najua unatamani kuwa na Mume wangu lakini hajawahi kukuelewa kama alivyomuelewa Anjeli. Kama akikuzagamua kwa usiku mmoja naamini utaridhika." Hilda aliongea kisha akamgeukia Asha.

"Hii sumu niliandaa kwa ajili ya Anjeli.... nilitarajia atarejea hapa lakini mambo yameenda tofauti. Hakikisha una mnywesha hii sumu pindi utakapo mtia machoni, juhudi zako ndizo zitakupa uwanja wa kumfaidi Osman kwa usiku mmoja" Hilda aliongea kisha akaondoka.

Asha alibakia kushikiria kichupa chenye sumu.................FULL STORY 1000. KARIBU KULIPIA KWA NAMBA 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP KWA NAMBA HII 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI; NURU HALISI SEHEMU 11--12  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-dada-poa-wa-usiku-mmoja-mtunzi-nuru-halisi-sehemu-11-12
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest