ENDELEA...........
Osman akiwa bafuni anaoga mlango ulifunguliwa, Hilda aliingia, yeye pia alihitaji kuoga.
"Siku yako imeandaje..." Hilda aliuliza huku akimsugua mgongo.
"Imeenda vizuri, kuna kitu nahitaji kukuambia..." Osman aliongea.
"Naelewa uko hapa na Mimi kumfurahisha Mama yako lakini moyo wako upo una mfikiria Anjeli. Siwezi kukulaumu katika hili kwa sababu naijua tabia ya moyo..." Hilda aliongea.
"Una maanisha nini kusema hivyo..."
"Mlete Anjeli hapa, nipo tayari awe mke wa pili....furaha yangu ni kuona moyo wako una furahia na si kingine" Hilda aliongea.
Osman alimgeukia mke wake kwa mshangao mkubwa.
"Una uhakika na maneno yako!".
Hilda alitikisa kichwa kuashiria ndiyo.
"Kitu gani kimekufanya useme hivyo"
"Naelewa sikuwa chaguo la moyo wako, unaishi na Mimi kwa sababu ya tu Mama yako alipendezwa na Mimi, tofauti na hapo sina uhakika kama nina nafasi kwenye moyo wako kama ilivyo kwa Anjeli...." Hilda aliongea akiwa kakunja ngumi, maneno haya yalikuwa hayatoki moyoni mwake.
Osman alijikuta akimshangaa, tangu azaliwe hajawahi kusikia Mwanamke anaye ruhusu mume wake kuoa Mwanamke mwingine bila shinikizo.
Kulivyo pambazuka asubuhi Hilda akiwa jikoni anaandaa chai Asha alimfuata akaweka kichupa cha sumu mezani.
"Siwezi kuua Mwanamke anaye mchanganya Osman kupita kiasi, nimefikiria usiku mzima ni kaona sipati faida yoyote kama nitafanya hivyo. Ni kweli nampenda Mumeo lakini sihitaji unisaidie katika hili...." Asha aliongea.
"Umewahi kufikiria kwanini Sabrina aliona nafaa kuwa mke wa Osman!" Hilda aliuliza.
"Sitaki kujua sababu lakini sina uhakika kama hata wewe umewahi kufikiria kwanini Sabrina ananiacha niendelee kuwa Mlinzi wa Osman pamoja na kuukasirisha moyo wake mara kwa mara" Asha aliongea kisha akaondoka.
Hilda alikitizama kichupa cha sumu akaachia tabasamu. Aliendelea kukaangiza.
Upande wa Anjeli akiwa chumbani kwake alijikuta akimkumbuka Osman.
Kuna namna alijisikia hatia kwa kuondoka na kumuacha pekee yake.
Muda wa yeye kuingia kazini ulifika, alioga vizuri kisha akavaa sare za kazi.
Akiwa katika kutembea alijikwaa, mara nyingi akianza siku yake kwa kujikwaa siku yake huwa inaenda vibaya.
Hakuwa tayari siku yake iishe vibaya tena katika eneo la kazi.
Alienda kwa Msimamizi wa Casino akaomba ruhusa.
"Sijisikii vizuri ingawa kwa kunitazama unaweza kusema nipo poa.... naomba unipe ruhusa ni kapumzike" Anjeli aliongea.
"Ni kweli sura yako haioneshi kuumwa....kwanini tusikae hapa wote tuwe tunaangalia Wateja wanaoingia na kutoka" Msimamizi alipendekeza.
Anjeli aliachia tabasamu, mara nyingi Msimamizi huyu hupenda kumuweka karibu.
Alivuta kiti chake akakaa, kila alipogeuza shingo yake alimkuta Msimamizi akimtazama.
"Kwanini unaniangalia hivyo...." Anjeli aliuliza.
"Kuna muda natamani ungekuwa Mtoto wangu ili ni kupangie Mwanaume wa kukuoa, uzuri wako ni wa kipekee sana." Msimamizi aliongea.
"Ningekuwa mzuri wa kiwango unacho ongea wewe nina uhakika ningeshaolewa na Mwanaume mwenye pesa nyingi..." Anjeli aliongea.
"Una uhakika hakuna Mwanaume hata mmoja mwenye pesa zake aliyewahi kukuhitaji kupita kiasi".
Anjeli alicheka kimtindo, alijikuta akimkumbuka Osman.
"Kuna kichaa mmoja tu amewahi kuzungumza kuhusu mahusiano, bahati mbaya ni Mume wa mtu.....sikuwa tayari kukatwa vidole sababu yake".
"Mume wa mtu?.... sijawahi kuweka hiyo tofauti, naamini Wanaume wote ni sawa bila kujali ana pete mkononi au la huenda hukumpenda na ndio maana una zungumza hivi"
Walijikuta wakipiga stori za hapa na pale, upande wa Osman akiwa na Walinzi wake walipanda ndege kuelekea Morogoro.
Masaa matatu yalitosha kuwafikisha katika Jiji hili.
"Kama unaipenda kazi yako basi naomba ujitahidi sana siku ya leo kuzuia huo mdomo wako usije kuzungumza ujinga wa aina yoyote ile" Victor alimkumbusha Asha.
Picha ya Anjeli ilipita chapu chapu mtaani.
Yule Mama aliyewahi kumpa Anjeli wazo la kwenda Casino kufanya kazi alikutana na Osman.
"Naweza kujua kwanini unamtafuta huyu mrembo?...."
"Ni mke wangu mtarajiwa.... kama umemuona naomba unipe maelekezo" Osman aliongea.
"Anapatikana katika Casino la Blueberry..... hakikisha kweli ni mkeo mtarajiwa tofauti na hapo acha kumpotezea muda wake!" Mwanamke huyu aliongea kisha akaondoka.
Anjeli akiwa ana kunywa wine alijikuta akishtuka baada ya kumuona Osman akiwa na Walinzi wake wakija usawa wake.
Hakuwa amefanya kitu kibaya lakini alijikuta akitetemeka tu bila sababu ya msingi.
"Sielewi kwanini huyu mpuuzi ananifuata....." Anjeli aliongea huku akigeuka nyuma aone kama kuna mtu mwingine lakini hakuepo
"Huna haja ya kuogopa huwezi kuondoka hapa bila ruhusa yangu...." Msimamizi wa Casino aliongea huku akishushia kinywaji chake.
Muonekano wa Osman ulitosha kumuambia siku ya leo atavuna pesa nyingi kupitia Anjeli.
Osman alivuta kiti kisha akakaa karibu na Anjeli.
Aliwapa ishara Walinzi wake waondoke
"Hilda kaniruhusu ni kurudishe nyumbani naomba usinikatalie" Osman aliongea kisha akashushia wine ya Anjeli.....................FULL STORY/MUENDELEZO 1000 TU.
NAMBA YA MALIPO 0743770612 JINA JOFREY
UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP NAMBA 0683009150..