Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI: NURU HALISI SEHEMU 19

16th Jul, 2025 Views 35



ENDELEA.......
Kwa hofu ya wingi wa Mbwa, Asha alijikwaa akadondoka chini
Mbwa walitaka kumrarua lakini Victor aliwazuia.

"Mjin.....ga wewe, kitu gani umefanya..." Victor alimuuliza Asha huku akimtia kibao.

Asha hakukubali kupigwa kilichofuata ilikuwa ni vita.

Mbwa walitengeneza duara Asha na Victor walianza kutupiana makonde.

Upande mwingine Anjeli alifikishwa hospital.
"Hatuwezi kumuokoa mtoto wa tumboni sumu iliyopo mwilini mwake ni kali sana hivyo utanisamehe katika hili...." Daktari bingwa aliyefundishwa mambo mengi na Sabrina alizungumza.

"Nilitegemea ukipita mikononi mwangu utakuwa na ujuzi mkubwa kuliko Madaktari wote wa Mwanza nilikosea kuwekeza matumaini ya namna hiyo,,, niandalie chumba cha siri nitamtolea Anjeli sumu yote...." Sabrina alizungumza akiwa anajiamini
Daktari hakuwa mbishi utaalamu wa Sabrina anauelewa vizuri.

Isingekuwa rahisi kwa Osman kukaa hospital bila kumkamata Asha.

Alishika simu akam-track Victor aliamini alipo yeye na Asha atakuepo.

Alifanikiwa kugundua sehemu alipo, alichukua pikipiki akaondoka haraka sana.

Dakika 20 zilikuwa ni nyingi alifika eneo la tukio, Victor na Asha walikuwa bado wanapigana..... alielewa kama hatoingilia kati basi watu hawa watachukua muda kumaliza kwa sababu nguvu zao zinalingana.
Osman alimkamata Asha kwa urahisi....

"Kama nitafia mikononi mwako kwangu litakuwa jambo la kheri" Asha alizungumza.

Osman alikuwa kakasirika hakutaka kusikia sauti yake, alimzimisha
Victor aliwashukuru Mbwa kisha yeye na Osman waliondoka.

"Kama Anjeli na mtoto wa tumboni watapoteza maisha Mimi pia sitamsamehe Asha, kwa mikono yangu nitamuua.... kwa sasa naomba umhifadhi kwenye chumba cha giza" Osman alimpatia agizo Victor kisha yeye akarudi hospitalini.

Sabrina aliendelea kupambana kufyonza sumu mwilini kwa Anjeli. Ndani ya moyo wake alijiahidi kumtendea ukatili mkubwa Asha pindi atakapo patikana.

Asha anarejesha fahamu akiwa kwenye chumba cha giza,,, mapigo ya moyo wake yalipaa juu alielewa Osman amekasirika sana na si kidogo.

Alinyanyua mikono yake ajinyonge lakini hakuweza kwa sababu mwili wake wote ulipigwa sindano ya ganzi.

Sabrina alifanikiwa kutoa sumu yote mwilini....kupitia ultrasound mtoto alionekana kuwa salama.

""Asha kapatikana?" Sabrina alimuuliza Osman huku akivua gloves.

"Anjeli na mtoto wapo salama?" Osman aliuliza swali badala ya kujibu swali.

"Kila kitu kipo sawa...."

"Mama, niliahidi kumuua Asha endapo Anjeli na mtoto wangepoteza maisha lakini kwa kuwa wapo hai wote sioni sababu ya kufanya hivyo ".

"kama nisingekuepo hapa, Anjeli na mtoto wangepoteza maisha ilikuwa ni kazi ngumu..... Daktari bingwa wa Mwanza kashindwa, katika hili naomba usiingilie kaa mbali kabisa".

"Niache ni muadhibu Asha, kama adhabu yangu haitafaa basi utamuadhibu wewe..." Osman alizungumza.

"Kifo pekee ndio adhabu itakayo mfaa Asha, endapo utaendelea kunichanganya akili nitakuua pia" Sabrina alizungumza kisha akaondoka alionekana kukasirika sana.

Osman hakuwa na namna, alimuacha Mama yake atende atakavyo.

Katika chumba alichowekwa Asha taa iliwashwa, aliingia Sabrina akiwa na Victor.

"Sikuwahi kufikiria kama huyu mpuuzi anaweza thubutu kupima kikomo cha hasira zangu,, siku ya leo lazima nimuue..." Sabrina aliongea akiwa kamkanyaga Asha aliyekuwa chini hajiwezi.

"nasubiria amri yako" Victor alimuambia Sabrina.

"wala usihangaike....nitamchuna ngozi yake kisha nitatengeneza viatu vya kumtoshea Anjeli pamoja na Osman,,," Sabrina alizungumza kisha akamvua nguo zote Asha.

Mwili wa Asha ulikuwa na makovu mengi ya risasi
"nini hiki...." Sabrina alimuuliza Victor
"hizo risasi zote zilipaswa kuwa mwilini mwa Osman lakini Asha alikuwa akijitoa sana kwa kifupi aligeuka kuwa ngao...." Victor aliongea.

Sabrina alikuwa dhaifu ghafla, ukatili aliopanga kumtendea Asha alisitisha....hakuona sababu ya kukaa kwenye hiki chumba aliondoka..............FULL STORY 1000.

WHATSAPP NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : DADA POA WA USIKU MMOJA MTUNZI: NURU HALISI SEHEMU 19  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-dada-poa-wa-usiku-mmoja-mtunzi-nuru-halisi-sehemu-19
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKAπŸ™ˆ3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest