SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 42
RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Niliyasikia maongezi yao tena yote na niliamua kuyarekodi kabisa ikiwa kama sehemu ya Ushahidi wangu, sikutaka kufanya mambo bila kuwa na Ushahidi wa kile ambacho nataka kukifanya.
Kuanzia pale ndio nikajua kwamba kilichokuwa kikimsumbua Brandina sio ugonjwa ambao Daktari aliniambia yaani Auditory Hallucinations ingawa ulitaka kufanana nao bali ni uchawi kutoka kwa Sammy.
“Ama zangu ama zao, watajua NANI
KANIAMBUKIZA ROHO MBAYA” nilijisemea ndani ya moyo wangu.
SEHEMU YA 42
Anza na Like kwanza.......Nilirudi kwa Betrice huku nikiwa na sura ambayo imechangamka kiasi hadi alishikwa na mfadhaiko kwanini nimebadilika ghafla kutoka kuwa na huzuni hadi mtu ambaye tabasamu limeanza kuonekana kwenye uso wangu.
Alinitazama kwa muda huku akitaka kujua ukweli, ni nini haswa kilikuwa kinaendelea hadi nikawa vile.
“Kuna nini maana umetoka kuongea na simu tu umekuwa kama mtu ambaye umechanganikiwa hivi?” aliniliuza Betrice
“Kila kitu hutokea kwa sababu, Mama aliwahi kuniambia hivi “In the magical universe there are no coincidences and there are no accidents. Nothing happens unless someone wills it to happen” labda kama utakuwa hujaelewa alimaanisha kwamba
“Katika ulimwengu wa miujiza ni kwamba hakuna kukosa ushirikiano au linganifu katika vitu fulani yaani kila kinachotokea basi kina sababu yake na hakuna ajali katika dunia hii bali kila kinachotokea ni kwamba huenda mtu ambaye linamtokea amesababisha kama sio kutaka” nilimwambia Betrice.
Niliona Betrice kama akifikicha macho hivi, akazamisha kidole sikiooni. Moja kwa moja nilitambua wazi kwamba hajanilewa kile ambacho nilikuwa namaanisha nikasema.
“Ukiona mtu limempata jambo fulani basi tambua kwamba yeye ndio amesababisha, hivi nitakuwa nakosea endapo nikiuua mjomba na
Sammy?”
“Kwanini?” Betrice aliuliza.
Sikuona kama nilipaswa kumjibu kwa maneno badala yake, nili-play sauti ya mazungumzo yao ilia pate kusikiliza. Alisikia kile ambacho kilikuwa kikiongelewa.
“Mungu wangu! Inamaana hawa ndio wamemuua?”
“Kama ambavyo wewe unashangaa ndivyo ilivyokuwa kwangu. Je, katika hili nitakuwa nakosea kuua?
“Mh! Kwa hasira ambazo mimi niko nazo nahisi wewe unachelewa kuchukua maamuzi au nenda kasema kwa askari”
“I know them, hawaamini katika uchawi so even those sound (kwahiyo hata hizi) wanaweza kupinga”
“Ila kweli hapa ndipo serikali muda mwingine inakwama”
“Usijali nitajua nini la kufanya kaa nyuma yangu” nilimwambia Betrice.
Tuliongea mengi hadi polisi walipokuja na kutukabidhi mwili wa Brandina huku wakisema kwamba ni kweli ripoti ya Daktari inaonesha kwamba mgonjwa alikuwa na msongo wa mawazo ndio maana alijinyonga hivyo tunapaswa kwenda kumpumzisha.
Hatukutaka kuwasikilizisha wala kuwaambia lolote lile badala yake niliondoka na mwili wa ndugu yangu hadi nyumbani ambako nilikutana na watu mbalimbali ambao walikuja ili kutupa pole.
Mzee Jawan na Mama walitupokea huku nao wakidondosha kilio, nilijaribu kuangaza kulia na kushoto labda ningemuona Shammy ama Loy mahala pale lakini sikubahatika kumuona.
“Vipi mmepanga mnazika saa ngapi?” aliniuliza Betrice
“Hapana ila tutakaa na Mama pamoja na
Mama kisha tutaona tunafanyaje”
“Si wapo hao hapo kwanini usizungumze nao?”
“Sawa hakuna shida” nilisema.
Nilimuita Baba pamoja na Mama kisha nikakaa nao pembeni kidogo ili tupate kuzungumza juu ya mazishi.
“Muda wa kumpumzisha ndugu yetu ni saa ngapi?” niliwauliza
“Mjomba yenu ndio ana idhini ya kusema saa ngapi na wapi maana sisi tupo tu hapa kama ambavyo ninyi mnajua”
“Kwahiyo hadi waje wao si ndio?”
“Naona itapendeza zaidi” alisema Mama Brandina.
Usoni kwangu niliweka tabasamu ila ndani ya moyo wangu kulikuwa na hasira, sikupendezeshwa na kitendo cha wao kujitenga na msiba ule huku wakimsukumia Loy kwamba ndio anapaswa kufanya kile kitu.
“Sawa lakini hakuna shida, kama akija tutapanga na asipokuja tutapanga wenyewe” nilisema kama nikiwa na hasira hivi
“Si ulimpa taarifa ama?’
“Ndio, anajua kila kila kitu na aliniambia kwamba atakuja hospital lakini sijamuona”
‘Ok, basi tumsubiri maana sisi hatuna sauti lolote endapo yeye akiwepo” Mama alisema.
Niliondoka mahala pale kisha nikarudi kwa Betrice kuzungumza naye, nilimwambia kwamba usiku tunapaswa kuwa makini mno. Hatutakiwi kulala hata kidogo tena tuwe katika chumba cha maiti ili kuilinda wasije kufanya ya kufanya.
Uzuri wa Betrice alikuwa ni mwelewe sana, alikuwa akiniheshimu sijui kisa nilikuwa namsaidia sana ama lah lakini naimani kwamba upendo huzaa upendo. Laiti kama Betrice nisingekuwa nampenda basi hata asingekuwa anapambana nami kwa namna ile.
Dakika zilienda na jioni ilikuwa imetia timu, nilimuona mjomba akiwa nyumbani na Sammy. Walisimamisha gari katika eneo la maegesho kisha walishuka lakini niliona Sammy akilia kupita maelezo, ilinibidi nimnong’oneze Betrice
“Umeona wanafiki wanavyokuwa, wanalia sana msibani wakati wao ndio wala nyama”
“Kila kitu kitaenda sawa, mwache alie leo ila Kesho atalia yeye” Betrice aliniambia.
Loy alipiga hatua hadi sehemu ambayo nilikuwa nimesimama huku Sammy akielekea kuongea na Mama.
“Alvila ilikwaje mbona hujanipa taarifa?” aliuliza mjomba huku akinichunguza kwa mbali ili kujua kama yale maongezi yao ya asubuhi niliyasikia ama lah
“Ndio hivyo, msiba upo kama kawaida sidhani kama tunapaswa kulaumiana. Kila mmoja alikuwa anatambua kwamba Brandina alikuwa anasumbuliwa na nini?” nilimwambia
Mjomba
“Mh! Mungu ampumzishe ila nimeumia kwakweli”
“Hakuna sababu ya kuumia ikiwa tunajua kwamba hata ingekuwa vipi angekufa, namna mzuri ya kumfanya Brandina awe sehemu salama ni kumuombea tu” nilisema kama kumtoa mjomba katika unafiki wake ambao alitaka kuniletea.
Maongezi yetu yalifika tamati, tuliitana kama familia na kupanga muda sahihi wa mazishi ambapo tulisema saa tisa alasiri ndio tunatakiwa kumpumzisha Brandina katika makaburi ya Sinza sehemu ambayo hata Mama yetu pia tulimpumzisha.
Nakumbuka usiku wasaa tisa, nilikuwa nimekaa pembeni ya mwili wa Brandina ambaye alikuwa kitandani. Upande wangu wa kulia kulikuwa na Betrice ambaye alishikwa na usingizi hivyo aliamua kujilaza.
Niliendelea kutazama mwili wa ndugu yangu lakini, nilihisi kama mlango ukifunguliwa hivi. Haraka nilimwamsha Betrice kwa kumsukuma naye aliamka huku nikimziba mdomo.
“Nahisi ndio anakuja kuwanga” nilimwabia kwa kumnong’oneza
“Nani?”
“Sammy, jifanye umelala nami nimelala” nilisema.
Kama ambavyo tulivyopanga, basi tulifanya hivyo kwa kujifumbisha macho. Dakika moja mbele Sammy aliingia ndani, kisha akazima taa na kuwasha tena lengo kupima kama tulikuwa macho ama lah.
Alipoona kwamba tumelala, alisogelea maiti na kuchukua nywele moja lakini, nilisema.
“Kwahiyo ndio kazi ambayo imekuleta hapa sio?” niliona akitetemeka huku akitupa nywele chini na kutaka kuondoka lakini Betrice aliekea katika mlango na kufunga kwa funguo kisha aliitupa kwa nje
Unalalamika inachelewa kutoka wakati nimekushushia bei, kutoka kila season kwa 3000Tsh mpaka bei ya 2500 kwa season zote tatu... Bado unalalamika... Achana na bei ya zamani ya 9000Tsh.... Njoo na 2500 usome simulizi yako.... WhatsApp namba 0717255498..