SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 46
Na Simulizi Za Kiswahili 0717255498
Maamuzi ambayo aliyakuchukua ni kujiua kwa kujichoma kisu katika eneo la shingo, maamuzi haya yalinisababishia mimi kusoma Al-badili kavukavu bila kujali mimi ni dini gani? Namwamini Mungu kiasi gani ila nilichotaka kumthibitishia Sammy kwamba hata mimi uchawi nauweza sema sijamaamua kuroga lakini, kwakuwa alitaka kupima kina cha maji kwa mguu basi nilimpa stahiki yake
SEHEMU YA 46
Weka Like yako hapa kabla ya kuanza kusoma......
Baada ya mazishi ya Betrice nilikaa na Mama yake nikamweleza kila kitu, kuanzia siku ya kwanza hata kabla ya kifo cha Brandina hadi tunamzika na mwisho kabisa maisha yamtoto wake.
Nilimweleza kwamba nataka kufanya kitu ambacho kitakuwa nje ya serikali na hakuna ambaye anaweza kuamini kama mimi ndio nimefanya unyama kama ule. Nilimwambia kwamba ni muda wa kumroga mtu wa kutumia Faraq kama sio Quran.
Mama Betrice kwakuwa alikuwa ni mchamungu sana alileta za kupinga ila nikamkumbusha kwamba kulipa kisasi ni sehemu sahihi katika maisha ya Binadamu.
“Mama unakubalije Betrice anatoweka duniani akiwa na umri mdogo vile ilhali mtu ambaye amemuua yupo na unajua wapi anapatikana?”
“Alvila sio kwamba sitaki kufanya unachoniambia lakini nafsi yangu inakataa. Mungu anasema katika Waroma 12: 19-20 kwamba ‘kulipa kisasi ni Shaula langu, mimi nitalipa. Adui yako akiwa na njaa mpe chakula, akiwa na kiu mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo kutamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake”
‘Awe! Awe! Sio mimi aise, mambo hayo aliweza Mama yang utu ila mimi hapana, nasema siwezi kabisaaaa. Kama unakataa hata usiilazimishe wewe chakufanya nipe mie idhini tu halafu mengine hayo yaache, nitayamaliza” nilimwambia
“Kwahiyo wewe utafanya kila kitu ila mimi nisihusike?”
“Ndio maana yake, najua wapi pakuanzia” nilimweleza.
Kutokana na maumivu kama sio machungu ya kuondokewa na mtoto wake alinikubalia, alinipa idhini ya kusoma Al-badiri, nami niliondoka pale huku kituo changu cha kwanza ikiwa nyumbani kwa kina Fatma Ussi.
Kama utakuwa umemsahau Fatma Ussi basi naomba nikukumbushe vizuri, huyu ndio yule mdada ambaye nilikuambiaga kwamba alikuwa anakuja shuleni ili kutupa umbea na matukio yaliyojili mtaani kwao na sio vinginevyo. Siku ukimuona kaja shule ujue mtaani kuna tukio limetokea, otherwise haji shule ng'oo.
Baada ya kufika kwao nilimwambia kwamba nahitaji kufanya kitu ambacho dunia itakuja kushangaa kama Tajiri namba moja ndani ya Sinza ndio amefanya
“Kuna ostadhi yoyote ambaye unamjua?” nilimuuliza
“Kuna nini unataka kufunga ndoa au?”
“Achana na masuala ya ndoa sio muhimu sana, hivi unajua kitu ambacho kimemuua
Brandina na Betrice?”
“Nilikuwa nasikia kwamba walikuwa wakisikia sauti zikiwataka wajiue”
“Then?”
“Sikufuatilia vizuri, ndio uniambie sasa” alisema.
Niliona kwakuwa nina shida basi natakiwa kumweleza japo kwa uchache, nilimfafanulia nini haswa ambacho kilikuwa kimewaua ndugu zangu
“Jamani, kwahiyo ndio unamtafuta Ostadhi ili kuwasomea dua au?”
“Hapana kwa ajili ya pigo takatifu, wao si wamerogea pemba sijui unguja mimi namwanika mtu pale nyumbani safi tena mchana kweupe”
“Hahaha! Nyie kweli Alvila umechafukwa”
“She doesn’t know me well (Hanifahamu vizuri) nina matukio ya kikatili kuliko hili” nilisema
“Hakuna sida kama ni hivyo twende” alisema huku akinitoa pale kwake.
Tulipanda katika gari na kunipelea maeneo ya kongowe ambako tulifika kwenye moja ya nyumba, nilimkuta Ostadhi mwenye madevu hivi ilinibidi nizungumze naye kwa kumwambia nini ilikuwa shida yangu.
“Una hakika kama huyo mtu ndio amehusika maana kawaida ya hii inakula kila aliyehusika” Ostadhi aliniambia
“Nafahamu kila kitu ndio maana nipo hapa kwako nataka msaada wako tafadhari”
“Mh! Sawa hakuna shida, utafanyia wapi na muda gani?”
“Muda upi ambao inakuwa kali sana kuliko mwingine?”
“Mchana yaani mkisoma muda huo mbona unayemsomea akili zitampata tu”
“Kinahitajika nini na nini?”
“Mbuzi watatu, kondoo, ubani na hudi pia majina matatu ya huyo mtu”
“Hilo halina shida Kesho nitakufuata kama sio mimi basi nitamwagiza hata huyu hapa rafiki yangu” nilisema na kuondoka mahala pale.
Niliporudi nyumbani nilikuwa ni mtu wa pirika pirika mno, kina baba waliniona kama nimechanganikiwa hivi lakini kile ambacho nilikuwa nakifanya nilitambua ni nini na nafanya kwa lengo gani.
Hadi kufikia jioni nilikuwa nimeshawapeka mbuzi pale nyumbani pamoja na kondoo kama alivyosema
“Mama leo unaonekana upo busy sana” aliniambia Mama Brandina huku nikiingia ndani, niliweka tabasamu na kugeuka kidogo kisha nikasema
“Ukiona kiza kimetanda basi kunapambazuka, adui achekewi maana atakumaliza”
“Una maana gani?”
“Ni muda wa kuwaua wot ewanaoua”
“Nani tena?”
“Sammy, Kesho hapa namsomea Al-badiri kavu na anakufa mbwa yule” “Umekuwa muislamu tena?”
“Kwa Al-badiri ipo kwa ajili ya waislamu tu? Kisasi hakina akina dini, nimeamua kutumia silaha ambayo hata yeye pia alitumia”
“Mh! Sawa hakuna shida” Mama Brandina aliniambia.
Usiku uliingia nililala huku ikiomba kupambazuke ili nimuoneshe umwamba mbwa ambaye alitaka kunimbwekea nyumbani kwangu. Kila dakika ambayo ilikuwa inaenda niliimani kuwa inaenda kubadilisha maisha yangu na kuwa mtu mwingine kabisa.
Hatimaye asubuhi ilipambazuka, niliona Fatma akifika nyumbani akiwa na Ostadhi ambaye nilimkaribisha kabisa ndani.
“Kila kitu kipo sawa” aliniuliza Ostadhi ambaye aliongozana na wenzake kama wawili hivi
“Ndio kila kitu kipo sawa kazi kwenu tu” nilisema
“Ondoa shaka tunajua nini la kufanya” Ostadhi alisema.
Kwakuwa aliniondoa shaka, niliamua kuwapa majina matatu ya Sammy kisha huyo nikaondoka zangu kuelekea katika Swimming Pool ili kuoga huku nikiwaacha wao ndani wakiendelea na maombi yao.
Wakati nikiwa katika Swimming Pool mimi na Fatma ambaye siku ile alioga na kufurahi kama unavyojua watoto wa uswahili wakifika ushuwani hujifanya kila kitu wanajua basi ndivyo ilivyokuwa kwake.
Aliogelea kila sehemu huku akipiga stori za hapa na pale, niliona Ma ostadhi wakichinja mbuzi na kuingiza ndani kisha walichinja na kondoo lakini sikutaka kuwajali sana maana niliwaachia kazi wao. “Yaani katika siku ambayo umenifurahisha leo moja wapo” alisema Fatma
“Hahaha! Kwanini?”
“Yaaani unasoma Al-badiri mchana kweupe kweli?”
“Ndio, dawa ya….” Kabla hata sijamalizia kuongea niliona mtu akitaka kufungua geti.
Nilipeleka macho vyema niligundua kwamba yule hakuwa mwingine bali ni Sammy, ambaye aling’ang’ana kuingia ndani
“Kaja kufanyaje huyu?” nilijiuliza huku nikitoka katika maji. Nilivaa nguo zangu na kueleka katika geti.
Nilipofika pale nilikutana na Sammy kweli lakini alikuwa akilia na kuniomba msamaha kwamba nimsamehe, machozi yalikuwa yakimtoka huku akiwa amepiga magoti. “Nisamehe! Nisamehe Alvila sikufanya kwa makusudi yangu ni shetani tu ndio, ndio alinipitia nakuomba nisamehe mimi” alisema
“Hahaha! Shetani hata nami mbona amenipitia” nilisema kisha nilifunga geti na kuingia ndani lakini kabla hata sijafika mbali nilimsikia Mama Brandina akisema
“Samehe saba mara sabini”
“Mimi ni Petro sina msamaha, nitafanya kazi ya kaisal kwahiyo hayakuhusu” nilisema na kuendelea kupiga hatua.
Nilipoingia ndani nilikoleza ubani vizuri katika moto, nikamtazama Ostadhi mkuu ambaye aliweka tabasamu
“Nje kuna mtu kaja enh?” aliniuliza
“Ndio, umejuaje?”
“Nilihisi hilo maana hata kabla ya kuja hapa alikuja nyumbani kuniomba msamaha”
“Mh! Aya soma bwana akufe mbele huko” nilisema na Ostadhi aliendeleza kisomo…
Weka Like yako ushamaliza kusoma....
Nunua kwa bei ya ofa yaani punguzo. Kila season huwa kwa 3000Tsh. Lakini leo nakupa season zote nne kwa 2500Tsh. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498..