Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 47

19th Jul, 2025 Views 149

SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 47

Na Sam Darfur 0717255498

RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Nilipoingia ndani nilikoleza ubani vizuri katika moto, nikamtazama Ostadhi mkuu ambaye aliweka tabasamu
“Nje kuna mtu kaja enh?” aliniuliza
“Ndio, umejuaje?”
“Nilihisi hilo maana hata kabla ya kuja hapa alikuja nyumbani kuniomba msamaha”
“Mh! Aya soma bwana akufe mbele huko” nilisema na Ostadhi aliendeleza kisomo…

SEHEMU YA 47
Unapoanza na kuweka Like kabla ya kusoma, unafanya jambo moja la muhumu sana. Ebu Like Tajiri....

Wanasema ukitaka kumuua nyani basi usimwangalie usoni bi maana kumwangalia kwako usoni kutakufanya uone chozi lake, pindi chozi linapokutana na macho yako basi huenda ukapoteza adhima ya kufanya maamuzi uliyopanga kufanya.

Ndio ilikuwa hivyo siku ile, kwakuwa nilidhamiria kuondoka na uhai wa Sammy sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuwasisitiza masheikh kama sio ma Ostadhi kufanya ya kwao.

Nakumbuka Mama alikuja na kuniambia kwamba Sammy alikuwa akilia na kusaga meno, nilitoka zangu nje kumtazama. Ni kweli alikuwa akilia huku akiniomba kwamba nimsamehe lakini moyo wangu ulikuwa umevaa ngozi ya kijeshi, ngozi ambayo sikutaka kusikia lolote lile.
“Kila mmoja anavuna kile ambacho amekipanda, ungekuwa na akili pale ambapo tulimaliza mgogoro basi ungefanya kuheshimu lakini kwa jeuri ukasafiri kabisa hadi
Zanzibar” nilisema
“Halafu Alvila mbona unaongea sana huyu muache awe chizi sijui nani? atajua mwenyewe” alisema Fatma
“Fikirae kwamba huyu angekuwa ni ninyi?” “Mama bwana! Mbona yeye hakufikiria kwa kile ambacho alikuwa anataka kukifanya?” nilimuuliza

Wakati tunaendelea kuongea niliona masheikh wakitoka ndani huku mikononi wakiwa na rangi za kombe, niliwageukia na kuwauliza.
“Jamani kila kitu mmekamilisha si ndio?”
“Ndio kila kitu kipo tayari kazi yako imekamilika”
“Mbona yupo hai sasa?”
“Anh! Hana muda mrefu anaenda kufa huyo” alisema Ostadh
Uso wangu ulikuwa na tabasamu nzuri mno lakini kwa Sammy alikuwa amechanganikiwa, alijaribu kuwakimbilia ma ostadhi na kuomba msamaha lakini hakuna ambaye alimpa sikio zaidi ya kuondoka mahala pale.
“Nenda kafe huko” nilisema kama kumzodoa mwanamke yule ambaye alikosa haya.
Nilifunga zangu geti kisha huyo nikarudi ndani ambako nilienda kuangalia kama kila kitu kilikuwa kimepangwa vizuri. Kwa bahati nzuri kulikuwa kumekamilika.
“Nafuraha sasa maisha yangu yanaenda kuwa ya amani zaidi” nilisema kumwambia Fatma ambaye alikuwa pembeni yangu “Umemkomoa yaani unamfanya kama vile humjui hivi”
“Wenye tamaa wote tulishawazika, anastahiki kupata hichi kwa 100% naimani” nilisema

Wakati tunaendelea kuongea niliona mlango ukifunguliwa na Mama aliingia ndani huku akiwa amshika kichwa chake, alionekana kama mtu ambaye amechanganikiwa hivi lakini sikujua wala kutambua ni kitu gani ambacho kilimfanya achanganikiwe.
“Kuna nini Mama?” nilimuuliza
“Amepasuka kichwa mbele yangu, kichwa kimelia pah!” Mama alisema huku akifanya kwa vitendo jinsi ambavyo kichwa kilipasuka.

Shauku ya kutaka kwenda kuona ilikuwa mbele yetu yaani mimi na Fatma, haraka tulitoka nje, tulifika hadi getini ambapo tulikutana ana mwili wa Sammy ambao ulikuwa umepasuka kichwa. Sehemu kubwa ya ubongo wake ilikuwa nje.
“Pigeni simu polisi” nilisema huku nikitazama mwili
“Mh! Na kesi je?”
“Khe! Umeona wapi mambo ya kichawi yanakuwa na kesi, we naye?” nilimjibu Fatma ambaye aliniuliza.

Mshahara wa dhambi huwa ni mauti siku zote, siku ile Sammy alipoteza maisha na ndio ulikuwa mwanzo wa maisha yangu mengine, maisha ambayo niliyachagua ya kuishi. Maisha ya furaha, maisha niliyoyapenda kupita maelezo.

Mwezi mmoja mbele nilianza kufuatilia mambo yangu ya masomo katika chuo ambacho nimechaguliwa, nilienda kila sehemu kuhakikisha kwamba nakamilisha usajili ili kuwa mwanafunzi halali.

Hichi kilikuwa ni kipindi kingine cha furaha katika maisha yangu, kilikuwa ni kipindi kipya ambacho naweza sema nilikuwa Alvila mwema, mpole na mpenda kusaidia wengine. Nikiwa na miaka 20 tu, niliingia chuoni huku nikitokea nyumbani huku nikiwa na dereva maalumu wa kike ambaye alikuwa akiniendesha.

Ilikuwa kawaida yangu ndio hii, sikutaka kutokea eneo lingine zaidi ya pale nyumbani hivyo nililazimika mambo mawili kuyaweka pembeni ili niweze kumaliza masomo yangu. Mambo hayo ni marafiki pamoja na mapenzi.

Sikuwa napenda kukaa na marafiki wa hovyo sababu nilitambua kwamba wengi wao wangekuwa wanakuja kwangu kwa ajili ya pesa, kuhusu mapenzi ndio kabisa sikutaka kusikia maana nilijiambia kwamba kama nitataka kuingia katika mapenzi basi niwe na mwanaume ambaye anaeleweka ili aweze kunioa.

Hatimaye muhula kama sio semester ya kwanza ilimalizika, tukapewa likizo ndogo ambayo ilikuwa inatutaka tubakie nyumbani. Niliporudi nyumbani nilianza kujifunza kuhusu kuendesha kampuni hivyo ilinilazimu muda wangu mwingi kwenda katika kampuni yetu.

Nilianza kufanya kazi kule, na CEO wa kipindi hicho hakuacha kunifundisha namna nzuri ya kuongoza kampuni. Kiukweli namshkuru sana yule jamaa maana hakuwa na tamaa za kimapenzi kama wengine.

Sijui alikuwa ananiogopa kwakuwa nilikuwa ni kiongozi wake au ni vile adabu tu. Ila itoshe kusema kwamba alikuwa anajitambua na Smart sana. Nilifanya kazi kwa kipindi chote cha likizo ndogo hadi tulipofungua chuo.

Kufungua kwa chuo kulienda sambamba na kuongezeka kwa shughuli za kimasomo ambapo ratiba zilianza kubana haswa, kama unavyojua chuoni kunakuwa na assignment za ajabu ajabu ilmradi mtu usifanye ili u-sup kama sio ku disco urudi zako nyumbani.

Niliona natakiwa kujipa u-busy wa hali ya juu mno, nilianza kukaa zangu library muda wote, nikitoka Library basi ratiba yangu ingekuwa katika eneo la chakula baada ya hapo ningeenda zangu nyumbani. Sikuwa na mambo mengi kama ilivyokuwa pis zingine za chuo.

Waliotaka urafiki nami iwe kimapenzi au kikawaida walipata shida kuniingia maana hata kutoa namba yangu ya simu ilikuwa ni kazi mno. Nakumbuka kuna mtu alikuwa anaitwa BERARD.

Alikuwa hana mvuto kabisa, kimuonekano haukuwa wa vijana wa kisasa. Kwanza hakuwa mrefu wa sifa wala mfupi wa kuchukiza bali ni mtu wa katikati hivi. Maji ya kundi ndio asili ya ngozi yake, nywele zilizochakaa. Unaweza sema kwamba labda hakuwa chuo kwa jinsi ambavyo alikuwa anavaa ama kuonekana.

Huyu alikuwa ni mwanachama mwenzangu katika group letu la Discusion kama sio majadiliano pale chuoni, tofauti na wengine wote Berard alikuwa na akili sana. Yaani ilikuwa mnaweza kushindwa na kitu, kwake akifumba macho na kufumbua basi jibu litapatokana mara moja.

Nilikuwa namchukia nisiwe muongo kutokana na jina lake kufanana na jina la Baba yangu yaani Benard lakini nilikuja kumpenda mara baada ya kujua ukweli wake, kumbe alikuwa ni maskini wa kutupwa tena alikuwa anatoka mbali mno ili kuja chuo akiwa na baiskeli yake mkangafu hivi.

Hapa nikajikuta naingia katika mtihani maana nilitaka kuzizuia hisia kutokupenda hivyo nilijifanya kuwa rafiki yake na ndio alikuwa rafiki yangu wa kwanza tangu nifike zangu chuo ila wanasema yajayo yanafurahia. Weka Like Boss.

Ni kama movie inaanza upya enhe🤔 Ns, tukutane WhatsApp ambapo natoa season zote kwa bei ya promotion. Lipia 2500Tsh tu. Kumbuka, bei ya awali ilikuwa kila season kwa 3000Tsh. Leo, unapata season nne kwa bei ya 2500Tsh. WhatsApp 0717255498.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 47  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-ya-maisha-nilimuua-mama-yangu-mzazi-ili-niolewe-na-baba-ep-47
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

TREVOR CHALOBAH 🫡

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 28💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

🌹I MISS YOU 🌹

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 22💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest