Endelea 🌻
Sona pia, alishtuka ndani ya moyo wake baada ya kumuona Dada yake, hakutaka watu wote wauone mshtuko wake hivyo aliachia tabasamu
"Bila shaka ulizaliwa siku ya mavuno....karibu mezani upate chai" Bi. Fatma aliongea huku akimtengenezea kiti akae
"Ahsante nyie endeleeni niko hapa kuzungumza na Liam..... tafadhali naomba uniazime dakika 20 au 30 hivi" Sona aliongea
Liam hakuwa na shaka, kwa pamoja walielekea bustanini
"Nafurahi kuona tukio la kuzama Meli halijaathiri Kampuni lako kwa kiwango kikubwa kama nilivyo fikiria...." Sona aliongea
"Nashukuru, enhe niambie kwanini umeomba kuzungumza na Mimi" Liam aliuliza
Kabla Sona hajajibu kitu, ujumbe uliingia kwenye simu ya yake
🩸Nimefanikiwa kuipata pafyumu iliyotumika kumuangamizi Marmar pamoja na rekodi ya mtu mtu aliyeagiza kutengenezewa pafyumu hiyo katika Kampuni ndogo ya Touch me 🩸 Ujumbe ulisomeka
Liam hakuonesha kushtuka, aliirudisha simu yake mfukoni
"Nimefanikiwa kumpata muuaji aliyehusika na kifo cha Marmar...." Sona aliongea
Liam alishtuka kwa maneno haya, amekuwa akiisubiria habari hii kwa miaka miwili sasa
"Nitakupatia taarifa kamili baada ya kutoka kazini, nahitaji kupeleka ripoti kamili katika Ubalozi wa Israeli kuhusiana na Waharifu pamoja na maiti nilizo zipeleka Nchini humo....." Sona aliongea kisha akaondoka
Hakuwa na lengo la kuzungumza hivi, lakini kitendo cha kumuona Sultana kimebadilisha kila kitu katika ufahamu wake....
Liam hakurudi ndani badala yake alienda kuonana na Msimamizi wa club ya spoon silver kutokana na ujumbe aliomtumia
"Sona....ndio mtu pekee anayeonekana katika hii rekodi" Vivi aliongea huku akimuonesha Liam
"Sona ni Polisi, huenda alinunua pafyumu hii kwa ajili ya kazi maalumu...hainiingii akilini hata kidogo. Nakumbuka baada ya aliyetaka kuwa mke wangu kupoteza maisha, Sona aliugua mwezi mzima kiasi cha kutaka kufa. Wawili hawa walikuwa marafiki naomba urudie kuchunguza upya" Liam aliongea
"Mtu wa mwisho kukutana na Marmar alikuwa ni Sona..... kipenzi cha moyo wako hakwenda hekaluni kama ulivyo fahamishwa" Vivi aliongea
Liam alimkaba mwanamke huyu baada ya kuona ana mchanganya
"Wivu wa mapenzi ndio ulimuondoa Marmar....Sona ni mwema machoni kwenu lakini ni shetani mkubwa mbele yangu na kwa marehemu Marmar" Vivi aliongea akamtoa mikono
"Kaniambia tayari kashampata muuaji.... naomba ufanye kama sijawahi kukupa hii kazi, Sona ni Malaika na si shetani" Liam aliongea kisha akaondoka
Vivi alibakia kucheka kwa namna Mwanaume huyu anavyo muamini Sona.....
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Mida ya jioni Sona akiwa chumbani kwake akijipaka mafuta, alitiririkwa machozi kwa sababu ya kitu anachoenda kukifanya muda si mrefu.
Alisogea kwenye kioo akajiangalia..... alijikuta akitamani uzuri wa Sultana uhamie usoni kwake. Hakuridhika kabisa na muonekano wa uso wake.
Alivaa nguo kisha akaingia kwenye gari
Ndani Ya Jumba La Dhahabu 🌻
Watu wote walionekana kumsubiria Sona.....shauku ya kumjua Muuaji aliyepelekea kifo cha Marmar ilikuwa juu sana
Dakika 15 hazikupita Sona alifika akiwa kabeba boksi dogo.
"Poleni kwa kunisubiria nilikutana na misukosuko barabarani lakini nimepambana kadri ya uwezo wangu kufika hapa..." Sona aliongea huku akitabasamu
"Pole....siku zote huwa naamini katika uwezo wako, hata kama ungekutana na maadui wengi kiasi gani ni lazima ungefika hapa, naomba tusikie kuhusu Muaji aliyepatikana" Bi. Fatma aliongea
"Kabla Marmar hajapoteza maisha alikuwa akinieleza mara kwa mara kuna Mwanamke kutoka Kijijini Odes anaye shirikiana na Wahalifu kutoka sehemu mbalimbali kuvunja sheria....sikuona kama ni kitu kikubwa sana. Lakini siku moja aliniambia huyo mwanamke kaahidi kumuua kisa na maana Marmar alikuwa kikwazo kwenye biashara zake" Sona aliongea kisha akatulia kidogo
Watu wote waliendelea kumsikiliza
"Huyo Mwanamke ni Kahaba maarufu Kijijini Odes...., japo alikuwa mbali lakini simu yake moja aliyopiga ilitosha kumuangamiza Marmar" Sona aliongea
"Huyo Muaji yuko wapi.....sitaki kusikia maneno mengi nahitaji kumshuhudia kwa macho yangu" Liam aliongea
"Muingizeni mhalifu ndani....'' Sona alitoa amri
Vivi aliletwa akiwa kachapika mbaya mbovu
Liam alishikwa na mshangao kwa sababu amekuwa akifanya kazi na mtu huyu kwa muda mrefu
"Kila kitu nilicho kueleza ni uongo..... Mimi ndio niliomba kutengenezewa pafyumu ya sumu baada ya kupatiwa amri na Boss wangu" Vivi aliongea huku machozi yakimtiririka
"Boss wako yuko wapi?...huyo ndio tunamhitaji kuliko kitu chochote...." Ali (dreva wa Bi. Fatma) aliuliza baada ya kuona wengine wote wametekewa
Vivi alinyanyua kidole chake akakielekeza kwa mtu mmoja, watu wote walitazama kwa umakini kujua kimemlenga nani
Itaendelea 💥.