Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SULTANA 10 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu) MTUNZI; LIZY MICA

1st Aug, 2025 Views 35



Endelea 🌻
"Sultana ni mzima....." Ali aliongea
Watu wote walisogea kwa haraka kujionea,

Ni kweli Sultana alikuwa mzima tena alionekana kufanya dua.
Moyo wa Sona ulipasuka kwa maumivu....alijikuta akidondosha machozi.

Harakati za kumtoa Sultana ndani ya tundu la Simba zilifanyika.
"Naomba uniambie maana ya kumshtumu binti wa watu kuwa ni Muuaji" Bi. Fatma alimtupia swali Sona

Kabla Sona ajatoa jibu simu yake iliita, aliusikiliza upande wa pili kisha akakata simu
"Vivi kapatikana amekufa....nina uhakika watu aliotaka kuwa kamata Marmar miaka 2 iliyopita ndio wamemuua, nisamehe Sultana kwa kukupa shutuma za uongo.... ilikuwa ni rahisi kwangu kumuamini Vivi kwa sababu alinionesha ushahidi unao kufunga" Sona alijitetea

"Tangu mwanzo moyo wangu uligoma kuamini mrembo kama huyu anaweza kuwa sababu ya watu kupoteza maisha" Bi. Fatma aliongea akionekana kumhurumia Sultana

"Polisi pia ni binadamu.... naomba tumsamehe, nitafurahi kama siku ya leo hatutaikumbuka" Sultana aliongea

"Kabla hatujaingia sebuleni, naomba uniambie ni kitu gani unataka ni kutendee nitatimiza" Bi. Fatma aliongea

Sona alimtazama Dada yake asikie ni kitu gani ataomba

"Naomba ni kae hapa kwa siku kadhaa mpaka nitakapojua kutengeneza keki...." Sultana aliongea na kufanya watu wote wacheke kutokana na kitu alichoomba isipokuwa Sona,

"Tutaonana kwa wakati mwingine, natakiwa ni kaandike ripoti kuhusu kifo cha Vivi....kama nitapata muda nitakuja kumfundisha Sultana namna ya kutengeneza keki" Sona aliongea kwa unafiki wa hali ya juu kisha akaondoka

Bi. Fatma aliingia jikoni mwenyewe, akaanza kuandaa vyakula kwa ajili ya Sultana
"Ni vyakula vingi sana hivi...punguza kujipendekeza" Ali alishauri

"Kama sisi wote hapa tungeingia ndani ya tundu la Simba nina uhakika tusingetoka salama....hivyo Sultana anastahili na si kujipendekeza" Bi. Fatma aliongea

Ali alikosa neno la kuongea, badala yake alisaidia kukata kata vitunguu.

Sultana akiwa kwenye chumba cha Wageni alilia bila kukoma....akili yake ilikataa kuamini kama mdogo wake ana mchukia namna hiyo kiasi cha kutaka kumuua.
Liam akiwa kasimama mlangoni aliumia kwa namna Sultana alivyokuwa analia.

Uzalendo ulimshinda, alijikuta akiingia chumbani bila hodi.... hakuhitaji kufikiria mara mbili mbili alimkumbatia.
Sultana ndio kuangua kilio zaidi ya mara ya kwanza kana kwamba yupo kwenye mashindano

"Kila kitu kitakuwa sawa, naweza kuelewa ni kwa namna gani unajisikia vibaya kupewa shutuma ya vitu ambavyo huvijui" Liam aliongea

"Ni kawaida binadamu kukutana na dhuluma katika safari yake hivyo silii kwa sababu ya kupewa shutuma za uongo...nalia kwa kuwa nimewakumbuka wazazi wangu" Sultana aliongea, hakuwa tayari kuongea hadharani jambo gani linamsumbua

Chakula kiliwekwa mezani kwa ajili ya Sultana....japo alikuwa katika maumivu lakini hakuwa na jeuri ya kukikaushia. Alijikuta akila vyote bila kupumzika,
Watu wote walimfurahia kwa namna anavyojali afya yake hata katika kipindi kigumu

🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Mida ya jioni, Liam aliamua kumtoa out.....alimpeleka katika jengo lililokuwa linaonesha Cinema nzuri hasa kwa wapendanao.
Muda wote macho yake yalikuwa yakimkagua Sultana na si kuangalia Cinema.
Mapigo ya moyo wake yalizidisha kudunda kila Sultana akiachia tabasamu sababu ya utamu wa movie.

"Ahsante kwa siku ya leo nimefurahi..... mapenzi ya kwenye movie yanavutia kuliko ya uhalisia...." Sultana aliongea wakiwa wanapata vinywaji

Liam hakuwa akimsikiliza, akili yake yote iliishia kwenye midomo ya Sultana na hata maumbile yake yalianza kufurukuta.

Sultana hakutaka kumtesa Liam, kwa mara ya kwanza alichukua chumba kwa pesa yake.
Kwa pamoja walishirikiana kukidhi matamanio ya miili yao.

"Nakupenda..... niruhusu ni kuoe" Liam aliongea
Sultana aliachia kicheko baada ya kusikia neno ndoa

"Kwanini unacheka....." Liam aliuliza

"Sina uhakika kama nina stahili.....najua huwezi kuamini lakini Mimi hapa nilikuwa ni mke wa Wanaume wote Kijijini kwetu, hivyo si busara wewe kunifikiria Mimi kama mke" Sultana aliongea

Liam alimnyamazisha kwa kumbusu zaidi na zaidi....alimpiga marufuku kumhadithia matukio yake ya nyuma kwa sababu aliamini kila mtu ana dhambi zake mbaya

Upande wa Sona alionekana kufikiria kupita kiasi akiwa kashikiria picha ya Marmar
"Siwezi kuwa na Liam kwa sababu tu Mimi na wewe tulikuwa marafiki..... sina hata ujasiri wa kumuambia nampenda nikihofia kuonekana kichaa,.... nitahakikisha haoi kwani kila mwanamke atakaye jaribu kuingia Ndani Ya Jumba La Dhahabu nitamuua kama ilivyokuwa kwako" Sona aliongea na picha ya marehemu rafiki yake huku machozi yakimtiririka

Kulivyo pambazuka asubuhi, alishangazwa na ujio wa Liam nyumbani kwake

"Nimeona nikuwahi mapema kabla hujaenda kazini, nisamehe sana kuna kitu kinanitesa, sijui nitaonekanaje kwa Bi. Fatma na Ali lakini naamini wewe utanielewa....." Liam aliongea akiwa kamshika mikono

"Kitu gani...." Sona aliuliza huku akihisi joto, akili yake ilimtuma Mwanaume huyu anataka kumtangazia upendo

Liam alimtazama machoni huku akifikiria aanzie wapi kuzungumza

Itaendelea 💥.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SULTANA 10 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu) MTUNZI; LIZY MICA  >>> https://gonga94.com/semajambo/sultana-10-ndani-ya-jumba-la-dhahabu-mtunzi-lizy-mica
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest