Endelea 🌻
"Mimi na Sultana tumekutana kwa muda mchache tu lakini nimejikuta nikimpenda.... nahitaji kumuoa kabla sijachelewa. Tafadhali sana pindi nitakapo tangaza nia yangu naomba uwe upande wangu.... ukifanya hivyo itakuwa rahisi kwa watu wengine kulipokea wazo langu kwa mtazamo chanya" Liam aliongea
Moyo wa Sona ulivunjika vipande vipande, hakutaka kuonesha maumivu yake hadharani hivyo alimkumbatia Liam
"Kila kitu kitakaa sawa....nitakusaidia katika hili, umemfikiria tu Bi. Fatma na Ali vipi kuhusu Dada yako Rayuna wiki ijayo atarejea Jijini Odes ni mtu wa kukosoa sana kila kitu lakini nitamthibiti pia" Sona aliongea, safari hii machozi yalimtiririka yakadondokea shingoni kwa Liam
"Kwanini unalia?" Liam aliuliza
"Nafurahi kuona moyo wako umempa nafasi mtu mwingine.... nilikuwa naumia kila iitwayo leo kuona unaongea kuhusu Marmar muda wote, sasa atapumzika kwa amani huko aliko" Sona aliongea
"Ahsante kwa maneno yako mazuri.... tuwahi kazini, kama hutojali naomba nikupe lifti siku ya leo" Liam alijipendekeza
"Naweza kusikia kwanini umempenda Sultana mapema namna hiyo kabla hata hujamjua kiundani zaidi...." Sona aliuliza
"Sijui ni nini kimenivutia kwake.... naomba usiniulize" Liam aliongea
Sona aliachia tabasamu, kwa pamoja waliingia kwenye gari wakasepa
Upande wa Sultana akiwa jikoni alipambana kujifunza kupika keki
"Kwanini unahitaji sana kujua kuhusu keki, usiniambie unataka kuwa Mpishi wa keki hapa Odes" Bi. Fatma aliongea
"Mpishi wa keki? acha kujidanganya kila kitu nafanya kwa ajili ya tumbo langu.... napenda sana kula keki kama Kijijini kwetu kungekuwa na Mwanaume anaweza haya mambo hakika angenioa bure" Sultana aliongea
Bi. Fatma alimuweka bao la kichwa kwa upuuzi aliozungumza
"Kuna watu wa kuolewa kisa keki lakini si wewe....thamani yako ni kubwa sana na hata sielewi Liam ana shida gani. Anapaswa akutangazie upendo kabla ya watu wengine kukuona"
Sultana aliachia tabasamu kwa maneno ya Bi. Fatma
"Najisikia raha kuona una changanyikiwa kupita kiasi sababu ya muonekano wangu"
"Wiki ijayo Dada yake Liam atakuwa hapa, japo ni mtu wa kukosoa kosoa sana vitu lakini naamini atachanganyikiwa juu yako" Bi. Fatma alidokeza
"Nilijua Liam ni Mtoto pekee kwenye hii familia.....nafurahi kujua ana Dada yake" Sultana aliongea
"Vipi kuhusu wewe.... muonekano wa macho yako unatosha kuniambia una ndugu yako unayemjali sana" Bi. Fatma aligusa pabaya
"Naomba usiulize sana kuhusu mdogo ndugu yangu..." Sultana aliongea
Bi. Fatma aliachia tabasamu kisha akaondoka kwa gia ya kuongea na simu, hakutaka kumkwaza
"Naomba uende Kijijini Odes, hakikisha unaniletea taarifa kamili kuhusu familia ya Sultana, hii kazi niliyo kupatia ni siri yetu...." Bi. Fatma aliongea
Ali alitikisa kichwa chake kuashiria ameelewa
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Siku iliyofuatia, Sona alimtoa out Sultana kwa lengo la kuzungumza
"Kwanini bado upo Jijini Odes.... nilitarajia baada ya kutoka salama tunduni mwa Simba ungesepa Kijijini kwetu cha ajabu ni kama umedhamiria kukaa kwenye Jiji moja na Mimi" Sona aliongea
"Siyo dhambi kama Mimi na wewe tukivuta hewa ya Jijini Odes.... sielewi kwanini unatamani Mimi kufa na si kuishi, naomba nisikie kutoka kwako kwanini unanichukia namna hii" Sultana aliuliza
"Sielewi kwanini na kuchukia, pengine ni kwa sababu una sura nzuri kuliko Mimi, pengine ni kwa sababu Mwanaume ninayempenda hajawahi kunitazama kwa matamanio au pengine ni kwa sababu ya tabia zako za Ukahaba" Sona aliongea
"Upuuzi mtupu! kuanzia sasa sitafanya chochote kwa ajili yako, kama si wewe kuniweka kwa siri kwenye Meli ya Star watu 280 wasingepoteza maisha.... naomba kuanzia sasa usifanye matendo magumu tena.... kuhusu Liam nampenda kwa sababu ni Mwanaume wa kwanza kunipenda bila kujali historia yangu chafu....hivyo nitaolewa naye" Sultana aliongea
Sona alivurugika kabisa akili, alinyanyua mkono wake amnase kibao Dada yake lakini hakufanikiwa baada ya kushikwa ilivyo
"Sona..... nimekusamehe yote uliyonitendea siku za nyuma, lakini kuanzia sasa na kuendelea sitasamehe kosa lolote utakalo nifanyia" Sultana aliongea kisha akamsogeza karibu kwa kuvuta mkono wake
"Pamoja na kwamba nilitembea na robo tatu ya Wanaume wote wa Kijijini kwetu, hakuna hata mwanamke mmoja aliwahi kunikabili.....si kwa sababu ni wajinga bali hawakuwa na uwezo tu wa kunikabili.....hata simba wa tunduni walishindwa kuniadhibu si kwa sababu Mimi ni mtakatifu bali muonekano wa macho yangu uliwatisha, kuanzia sasa usijaribu kupima uvumilivu wa hasira yangu" Sultana aliongea kisha akaondoka
Sona aliishia kutetemeka, tangu akiwa mdogo alikuwa ni mtu wa kumpandishia sauti Dada yake, alishindwa kuelewa kapata wapi ujasiri wa kumchimba mkwara
Sultana akiwa katika alipishana na Kijana mdogo akiuza keki, mate yalimjaa akashindwa kujizuia
Alitoa pesa mfukoni akanunua kipande kimoja....hakuona shida kutembea huku ana kula
Ile anataka kung'ata kwa mara ya tatu alijikuta akikodoa macho baada ya kukutana na kitu cha ajabu
Itaendelea 💥.