Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SULTANA 14 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu) MTUNZI; LIZY MICA

1st Aug, 2025 Views 8


Endelea 🌻
Bi. Fatma alizirai baada ya kumshuhudia binti yake wa pekee amepoteza maisha akiwa katika huzuni mkubwa.

"Kitu gani kimetokea? kwanini umemleta hapa badala ya kumpeleka hospitali" Ali aliuliza akiwa kapaniki

"Ali, kila kitu kilitokea kama movie hivi....sijui ni kitu gani napaswa kuongea, lakini niliona inapendeza yeye kuja nyumbani na si kwenda hospitali" Sultana aliongea akiwa bado kabeba maiti mgongoni

"Liam yupo ana zungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi mpya anaotaka kuufungua, usimpigie simu......mtu yeyote hapaswi kujua mpaka pale Bi. Fatma atakaporejesha fahamu. Mvalishe mavazi mazuri Rayuna....risasi zilizopenya kichwani mwake haziwezi kuwa sababu ya yeye kuonekana mchafu" Ali aliongea ilihali uso wake umejaa machozi

Sultana alifanya kama alivyoambiwa.....alimpendezesha Rayuna. Safari hii hakuwa akilia tena....alishirikiana na Wafanyakazi kazi wengine kuandaa sherehe yake ya mwisho.

Sona anafika ndani ya jumba la dhahabu kwa gia ya kuleta majina ya Makampuni yanayosifika kwa kutengeneza nguo nzuri za Maharusi.

Anajitia kushangaa baada ya kuona picha ya Rayuna ikiwa imepambwa maua yanayoashiria msiba. Kama kawaida yake alipoteza fahamu. Alibebwa akaingizwa katika chumba cha Wageni wakiamini muda si mrefu atarejesha fahamu

Mida ya Jioni Liam anarejea nyumbani, anashtushwa na mavazi meupe yaliyokuwa wamevaliwa na watu wa familia yake

"Liam.....Rayuna yetu kazima kama mshumaa, watu wasiojulikana wamemuua..." Bi. Fatma aliomboleza

Kama si Sultana kumshika kipenzi cha roho yake basi angedondoka chini.

"Sitaacha hili jambo lipite.... Mimi kama Polisi nitaomboleza huku kazi ya uchunguzi ikiendelea, Sultana wakati tukio linatokea naamini ulikuepo... naomba ufuatane na Mimi ili tujue tunaanzia wapi" Sona aliongea huku machozi yakimtiririka

"Huna haja ya kuogopa ni kazi yake kupata ABC ili ajue anaanzia wapi hivyo ongozana naye"Bi. Fatma alimuambia Sultana

Sultana hakuwa na shida aliongozana na Mdogo wake.
"Umekuwa mtu wa mkosi sana....yaani kitendo tu cha Rayuna kutoka out na wewe kapoteza maisha, hakika unastahili adhabu na si msamaha" Sona aliongea baada ya kufika kituo cha Polisi

Sultana alimkunja mdogo wake, ni wazi alikuwa amekasirika kupita kiasi

"Nilikuambia safari hii ukifanya makosa sitakusamehe, umemuua Rayuna kisa na maana alifahamu siri zako zote za kipuuzi. Sona, ndoto yangu ilikuwa ni kuwa Rubani wa ndege lakini sikuweza kuitimiza kwa sababu ya ujinga wangu Kuanzia sasa nitakuwa Mlinzi wako, kila jambo baya utakalolitenda utalilipia " Sultana aliongea

"Nina uwezo wa kutengeneza ushahidi utakao kufunga bila mzani wa tundu la simba.... naomba uondoke Jijini Odes, huna haja ya kunichimba mikwara" Sona aliongea kisha akaitoa mikono ya Dada yake kibabe zaidi

Sultana alimtia kofi mdogo wake kiasi cha damu kutoka.
"Maisha yangu yote yatakuwa ndani ya Jumba La Dhahabu....labda ni wakati wa wewe kurudi Kijijini Odes na siyo Mimi. Naweza kuonekana mrembo machoni kwako lakini moyo wangu hauna tofauti na ule wa malaika muasi....nitaiharibu ndoto yako uliyoihangaika kwa muda mrefu" Sultana aliongea kisha akaondoka

Sona aliishia kujishika shavu lake, ni wazi kabisa hakuamini kama Dada yake kamnasa kibao

🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Isingekuwa rahisi kwa watu wa Jumba La Dhahabu kulaza maiti ya Rayuna.
Tanuru dogo kwa ajili ya kuchoma mwili wake lilitengenezwa
Sona pia alihudhuria katika mazishi ya Dada yake Liam.

Muda wote macho yake yalimtazama Sultana ni kama alikuwa ana mchunga asije akaropoka.
Kitendo tu cha kugeuzia shingo yake pembeni alimpoteza Sultana.
Hakujua ni wapi kaelekea.... alitaka aondoke akamtafute lakini Liam alimuomba watoke faragha kwa ajili ya mazungumzo

Sultana alielekea nyumbani kwa IGP Zero, Kiongozi wa juu kabisa wa Polisi wote Jijini Odes. Japo ilikuwa ni usiku lakini Mlinzi wa getini alimfungulia

"Ni kitu gani kimekuleta nyumbani kwangu usiku huu...." IGP Zero aliuliza huku akimeza mate kutokana na urembo wa Sultana

"Nimekuja hapa kufanya biashara na wewe sikutarajia kama utakuwa Kijana mdogo namna hiyo mwenye uzuri wa kipekee.." Sultana aliongea

"Usitake kuniambia unataka ni kusaidie kusafirisha vitu haramu nje...." IGP Zero aliongea ilihali kichwa kikivimba kutokana sifa aliyomwagiwa

"Kumekuwa na matukio ya ajabu sana yakiendelea chini kwa chini bila wewe kujua, kama hali itaendelea hivi nahofia kusema serikali itahitaji maelezo kutoka kwako, pengine ulikuwa hujui lakini Meli ya Star ilizama sababu ya Polisi.... kwahiyo lawama zote mlipaswa kubeba nyie na si bahari..... " Sultana aliongea

"Unaweza kunitajia jina la huyo Polisi kichaa...." IGP Zero aliuliza

"Sona..... kabla Polisi Tee hajapoteza maisha alinitajia jina la huyu kiumbe, sijui ni kitu gani utafanya kwake.....roho ya Polisi Tee inahitaji kupumzika kwa amani, kitu kingine nitalala hapa siku ya leo ili uweze kufanya maamuzi ya busara" Sultana hakuona shida kujitoa sadaka kwa ajili ya jambo kubwa

IGP Zero aliachia tabasamu, hata hivyo amewahi kusikia tetesi kuwa Sona ana kitamani cheo chake....hoja za Sultana ziliongeza uzito

Ndani ya jumba la dhahabu; watu wote walionekana kuwa na shauku ya kujua wapi Sultana alilala usiku mzima

"Ni kosa la jinai mtu kulala nje kabla hata msiba haujapoa vizuri....nimeangalia vyumba vyote lakini sijamuona" Sona alichochea

Kabla Bi. Fatma hajatia neno, ilisikika sauti ya mtu akikohoa....wote kwa pamoja walielekeza macho chini ya uvungu wa meza

Itaendelea 💥.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SULTANA 14 (Ndani Ya Jumba La Dhahabu) MTUNZI; LIZY MICA  >>> https://gonga94.com/semajambo/sultana-14-ndani-ya-jumba-la-dhahabu-mtunzi-lizy-mica
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest