Endelea 🌻
"Sitaki kuamini ulilala uvunguni mwa meza" Bi. Fatma aliongea akionekana kumhurumia Sultana
"Ni sehemu pekee niliyoona inafaa kutuliza maumivu yangu.....ni mara yangu ya kwanza kumshuhudia mtu akikata roho sikuwa na ujasiri wa kulala chumbani" Sultana aliomboleza
"Liam, ni vyema ukimpeleka chumbani kwake..." Ali alishauri baada ya kuona maombolezo yanataka kuanzishwa upya
Wakati Sultana na Liam wanapisha sebuleni, simu ya Sona iliita.
Moyo wake ulilipuka baada ya kugundua Mpigaji ni IGP Zero aliondoka bila kuaga.
"Sona....." IGP Zero aliita baada ya kumuona mhalifu
"Yes IGP..." Sona aliitika kwa utii
"Ulimuua Marmar, ukamuua Polisi Tee....ukamua Vivi Mmiliki wa club ya spoon silver, umemuua Rayuna na kubwa kuliko yote uliua watu 280 kwa kuzidisha uzito kwenye Meli. Nilitaka ni kukate vipande vidogo vidogo kisha ni kuchome mfano wa mshikaki lakini yote haya hayana maana kwa sababu kuna mtu mmoja ametuliza hasira yangu kwa kunipa uchi wake hivyo kuanzia sasa wewe si Polisi...." IGP Zero aliongea kisha akamrushia barua
Sona aliidaka akiwa haamini masikio yake....katika maisha yake yote hakuwahi kutarajia kama Dada yake anaweza kuwa sumu kwake pamoja na visa alivyomfanyia.
Ilimchukua muda mwingi sana kutimiza ndoto yake lakini imekuja kuyeyuka ghafla tu baada ya Sultana kuingia Jijini Odes.
Alijitutumua mpaka alipofika ndani ya jumba la dhahabu, watu wote walimtazama kwa macho ya mshangao kutokana na huzuni iliyokuwa imetawala sura yake
"Nimeacha kazi...sina haja ya kuwa Polisi tena kwa sababu nilishindwa kumlinda Marmar na sasa Rayuna kapoteza maisha" Sona aliomboleza huku akiweka barua mezani
"Bila shaka kifo cha Rayuna kilikuwa ni onyo kwake....kwa ajili ya uhai wake pamoja na watu wake wa karibu ni lazima aache kazi, si kuacha kazi tu ni onyo kwa mtu yoyote kuchunguza kwanini Marmar alikufa. Liam nina uhakika hata Meli ya Star ilizama kama onyo kuhusu kufuatilia kifo cha aliyebakiza siku moja awe mkeo" Bi. Fatma aliongea
"Najua kuwa Polisi ilikuwa ni ndoto yako ya muda mrefu, lakini hata ndoto hubadilika kutokana na mazingira..... Mimi na familia yangu tutakuwa tayari kukuunga mkono kwa kitu kipya utakacho kifikiria" Liam aliongea
"Nitafungua hospitali....japo sijui chochote kuhusu mgonjwa na dawa lakini nitajifunza...." Sona aliongea huku akiachia tabasamu
Watu wote waliahidi kumuunga mkono.... walimpongeza kwa ujasiri wake wa kuisahau ndoto yake ya muda mrefu
"Mimi na Sultana tutaandaa chakula kwa ajili yenu endeleeni kupumzika" Sona alitoa wazo
Yeye na Dada yake walielekea jikoni, ile wanaingia tu Sona alimshikia kisu Sultana
"Wee Malaya naomba uniambie ni kitu gani umempa IGP Zero mpaka nimesimamishwa kazi!" Sona alifoka
"Tofauti na k*ma sikuwa na kitu chochote cha kumpa, nafurahi kusikia unataka kufungua hospitali lakini kama utaendelea kufanya matukio yako ya ajabu juhudi zako zitapotea bure" Sultana aliongea kisha akakisukuma kisu kikaanguka chini
"Naomba urudi Kijijini Odes, tofauti na hapo sitakuwa na huruma na wewe tena. Mama yetu alipatikana amefia kwenye kisima cha maji sababu ya ulevi wake...kila mtu aliamini hivyo lakini hiyo siku Mama hakuwa ameelewa, nilimsukuma ndani ya kisima kwa mikono yangu miwili" Sona aliongea
"Kwanini ulifanya hivyo...." Sultana aliuliza akiwa kwenye mshtuko mkubwa
"Sura yangu haina mvuto kama nitazembea kutafuta pesa hakuna Mwanaume atakaye ni tazama, lakini Sultana hahitaji kutafuta pesa kwa sababu muonekano wake ni wa kipekee, Mama yetu aliongea hivi" Sona aliongea huku akakiokota kisu kilichokuwa chini akaanza kukata mboga
Sultana alidumu kushangaa, alijiuliza mdogo wake alipata wapi ujasiri wa kumsukumia Mama yao kisimani akiwa na miaka 10.
Nguvu za kupika zilimuisha, hivyo kila kitu kilikamilishwa na Sona.
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Haikuwa rahisi lakini kwa kuwa binadamu wote tumeumbiwa kusahau kila mtu alirejesha tabasamu lake usoni bila kujali kuondoka kwa Rayuna
Sona alikuwa bize kuliko kawaida tofauti na mwanzo....hitaji lake la kufungua hospitali alilipa kipaumbele zaidi.
Ukiachana na mradi wa ujenzi wa hospitali aliamua kujenga kiwanda cha kusindika maziwa.
Lakini ndani ya jengo hili alijenga gereza dogo kwa ajili ya kuwa hukumu watu wote wataopita katika njia zake
"Wiki mbili zinatosha kiwanda hiki kukamilika..... naomba muajiri watu wengi, kazi inapaswa kufanywa usiku na mchana bila kupumzika. Nitawalipa pesa nyingi bila kujali nitabaki na akiba sifuri au la" Sona aliongea
Contractor aliyekuwa anahusika na ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa alitikisa kichwa chake kuashiria ameelewa
Baada Ya Wiki Mbili 🌻
Kiwanda cha kusindika maziwa kilikamilika....watu wengi walimpongeza Sona kwa namna alivyopiga hatua kwa haraka.
Familia ya Bi. Fatma ilipewa kadi ya mualiko katika ufunguzi wa kiwanda hicho......Liam alikuwa Mgeni rasmi kutokana na umaarufu wake.
🩸 Hakikisha gereza lina mpata mhalifu sugu siku ya leo 🩸 Sona alimtumia ujumbe Kijana wake wa kazi
Sultana alikiwa ana kunywa maji, alihisi mvurugiko wa tumbo ghafla....hakuwa tayari kuaibika mbele za watu hivyo alielekea chooni haraka
Liam alijikuta akisita kuongea baada ya kumshuhudia mrembo wake akielekea uwani. Kama si Sona kumkanyaga huenda angepoteza uelekeo wa kuzungumza.
Sultana aliingia chooni akiwa mwenye haraka, anajisikia ahueni baada ya kupunguza uzito.
Ile anatoka asafishe mikono yake alipuliziwa pafyumu iliyomfanya apoteze fahamu
Baada ya uzinduzi wa kiwanda cha kusindika maziwa kukamilika watu wote walianza kutawanyika
Liam aliangaza macho yake huku na kule lakini hakumuona Sultana.
Ghafla tangazo linatolewa kuhusu kuokotwa kwa pochi
Watu wote waligeuza shingo zao kuangalia pochi inayotangazwa
Itaendelea 💥.