Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SWEETHEARTπŸ’‹πŸ˜˜ 01&2&3 (Ma oxygen yoooooπŸ™Œ)

16th Jul, 2025 Views 5



BY DIANA STORIES

WTSP 0768328909


Joy mama aliniita kwa sauti kubwa baada ya kurudi kwenye mihangaiko yake ya kila siku, ilikuwa mida ya saa nne kasorobo usiku.
Shikamoo mama nilimsalimia nikakaa chini nimsikilize leo kaja na lipi maana sio kwa kuniita huko

Marahaba vipi mmeshindaje hapa nyumbani?... mama aliniuliza
Tumeshinda salama pole na kazi mama nilimwambia
Asante umemaliza mtihani sasa hivi upo tu nyumbani huna kazi nataka uende kwa baba yako labda ukiwa karibu na yeye ataona aibu atakusomesha.
mh niliishia kuguna tu ....

Sasa mimi naongea unaguna nini? mama aliniuliza
Mama mtu toka nipo mdogo hata kutuma hela ya soksi hakuna, hata kusema mwanangu likizo hii njoo dar hakuna ndio niende sasa hivi kweli mama mbona mimi nimeridhika na maisha yetu haya πŸ₯Ή..

Joyce natamani ufike mbali mama yako sina uwezo endapo ukifaulu hela nitatoa wapi ? lakini ukiwa huko ataona tu aibu na nishampigia simu kesho kutwa utaenda nauli hii hapa najua ukifanikiwa wewe na mimi pamoja na wadogo zako tumefanikiwa....
Lakini mama ndio ghafla ghafla hivi πŸ€”. nilimuuliza
Hakuna muda wa kupoteza mwanangu angalia mbele
Nilishusha pumzi nilikubali kishingo upande kwa kweli

Kesho nilijiandaa na safari mama alinipa simu ndogo yenye laini na namba ya simu ya baba na yake..
kesho kutwa asubuhi niliondoka kwa upande mwingine nilifurahi kusafiri kwenda dar es salaam jiji lenye maghorofa na mataa....
Niliingia usiku sana mida ya saa sita kasorobo nilipiga ile namba akapokea baba nilimsalimia nikamwambia nimeshafika....
Akaniambia nisitoke nimsubiri hapo hapo anakuja, kweli baada ya dakika mbili alikuwa tayari ameshafika
nilikuwa nishaanza kumsahau maana nilimuona muda mrefu tangu nipo darasa la pili kipindi hicho amekuja kujenga barabara...

Tulisalimiana tukashuka kwenye basi nikaenda kuchukua mizigo tukaingia kwenye gari aina ya Prado.
mh yaani mzee ana pesa, gari kali halafu nilikuwa naishi maisha ya tabu nilijiuliza pasipo na majibu.
njiani kila mtu alikuwa kimya hadi baba alipovunja ukimya...
Joyce umekua sana nilikuacha mdogo sana vipi mama anaendeleaje? baba aliniuliza
Ajambo anakusalimia sana nilimjibu
Salamu zimefika karibu huku ndio nyumbani kwangu Dar naishi na familia yangu natumaini utawafurahia kuna ndugu zako kaka na dada zako pia mama yako mkubwa hivyo sidhani kama utajisikia mpweke...

Asante sana baba nashukuru nilijibu
Tulifika kwenye nyumba ina geti baba alipiga honi geti likafunguliwa akaingiza gari tukashuka...
alikuja mdada kutupokea alinikaribisha ndani...

Scola muandalie maji aoge,ale apumzike muda umeenda now tutaongea kesho..
Sawa baba yule dada alijibu akaenda kunionyesha chumbani kwake niliweka begi nikaenda kuoga nikaomba nilale maana nilichoka sana sikutaka hata kula....
Asubuhi na mapema niliamka nikaoga nilitoka sebuleni nikamkuta baba amekaa na mwanamke niliwasalimia nikakaa kwenye sofa...
Joyce..... Baba aliniita
Abeh......
Itaendelea

SEHEMU YA 02~03

Huyu ni mama yako utaishi naye hapa Happy na Joel wako wapi mbona siwaoni niwatambulishe ndugu yao ..
Joel kaenda kufanya mazoezi ya kukimbia Happy nahisi kalala bado mama alijibu....
Scola Muite Happy...... sawa baba

Baada ya muda Happy alikuja alisalimia akakaa
Happy huyu ni mdogo wako anaitwa Joyce tutakuwa nae hapa pia kuanzia leo utalala nae...
sawa baba aliitikia na kuondoka mama nae aliinuka akaondoka nikawa nimebaki na baba tu ...
Unaweza ukaenda kunywa chai sasa humu ndani kila mtu ana ratiba zake baba aliinuka na kuondoka chumbani kwake.

Niliinuka ili niende jikoni nimuulize Scola kuhusu chai nikakutana na kijana anaingia ndani kavaa nguo za mazoezi nikajua huyu ndio atakuwa kaka Joel bila kukosea...
Sorry ni mfanyakazi mpya wewe aliniuliza
kabla sijajibu Happy alitokea na kujibu huku akicheka mfanyakazi wapi ni ndugu yako huyo anaitwa Joyce πŸ˜‚πŸ˜‚......
ee makubwa karibu Joy umetokea wapi mbona sikufahamu.

Usimuulize maswali mengi bhana atakuogopa bure chai ipo tayari twendeni tukanywe ...
Tulielekea mezani kunywa chai tukiwa tunakunywa chai mama nae alikuja kunywa chai muda wote alikuwa ananiangalia kwa jicho kali hadi nikaanza kuogopa...

Joyce vipi mbona hunywi chai au unaogopa? mama aliniuliza kwa kebehi πŸ˜€ we mtu aniangalie vile halafu nisiogope mchezo πŸ˜‚...
Itakuwa anaogopa anashangaa vyakula vyote hivi hajawahi kuviona Joel alidakia..
Mhh una uhakika kaka wakati huko Rukwa nasikia wanalima sana hawana shida ya chakula Happy alijibu....
Halafu mama huko Rukwa si ndio kuna wachawi huko hajaleta kweli huyu Joel aliongea

Kaka sio vizuri hebu tuleni chakula Joyce kula nikutembeze mitaa natumaini utaifurahia mzoee tu kaka yangu ndivyo alivyo...
Kiukweli nilianza kukerwa na yale maneno nilijikuta hamu yote ya kula imeisha ghafla nilitamani niinuke ila nikaona hapa nitazua mengine mwisho nionekane jeuri hata siku mbili sina..
Mama alimaliza kunywa chai akainuka akaondoka zake na mimi ndipo nikapata ahueni kidogo nikaanza kula na vile nilikuwa na njaa na vyakula vilikuwa vya maana kweli...
nilipomaliza niliinuka ili nitoe vyombo Scola alikuja haraka na kuanza kutoa yeye..

Ngoja tutoe wote nikusaidie dada Scola sio vizuri tumekula uje usafishe peke yako.... nilimwambia
Hata usijali hii ndio kazi yangu nalipwa mishahara
Sijazoea kukaa bila kazi 😁nitakuwa nakusaidia tulijikuta tunacheka wote.
Tulikusanya vyombo tunapeleka jikoni nilimsaidia kuosha nikaenda nje kupunga upepo nilichukua simu nikampigia mama ili nimwambie kuwa nilifika salama
Simu iliita hadi akapokea nilivyosikia sauti yake nilifarijika kidogo.....
Itaendelea ......

FULL1000
WHATSAPP 0768328909
STORY HII IPO FULL KABISA KARIBU.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SWEETHEARTπŸ’‹πŸ˜˜ 01&2&3 (Ma oxygen yoooooπŸ™Œ)  >>> https://gonga94.com/semajambo/sweetheart-01-2-3-ma-oxygen-yooooo
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 14...15

majario rewards 100 Comments 0
 

MDOLI MPENDA UTAMU...1

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKAπŸ™ˆ3~4

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 11.

majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest