Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

UDHAIFU WA MR CEO...Chapter 7--8

11th Sep, 2025 Views 102



7

"Wewe mimi siwez kulala na wewe, kwanza nipo period, siwez kufanya mapenzi tena na mwanaume mimi, kama ndio ulikuwa umenitafutia kazi ili unile basi sina shida na kazi yako, nikashangaa anaweka kidole chake kwenye lips zangu na kusema naomba usiongee sana, si unajua mimi siwezi kelele, ila sijasema kuwa nataka kusex nawewe, nimesema naomba kwenda kulala na wewe, au wewe umeelewa tofauti, nakuahidi sitakaa nikufanye kitu chochote kile bila ridhaa yako, nataman tu kulala bila dawa, na nililala kwa mara ya kwanza nikiwa karibu yako, naomba nisaidie kwa hilo...

Hapo angalau nikamuelewa, ingawa najua wanaume huwa hawatabiriki, ila nafsi yangu ikawa inaniambia kuwa natakiwa kumuamini tu, maana ni kweli najua anashida, na mimi ndio natakiwa kumsaidia kutokana na shida yake... Basi nikakubali, na wakati wote akawa ananiangalia na kila muda ananishika mkono, tumefika kwake akapitiliza bafuni, mimi nilikuwa tayari nimeshaoga, hivyo sikwenda kuoga na baada ya hapo kila mtu akapanda kitandani ila kila mtu akageukia upande wake, nilikuwa naogopa kuliwa kama nini, na wakati mtu mwenyewe ameshawah kunila, ila sijui hata nilikuwa naogopa nini kiasi chote kile....

Basi tukakaa kitandani lisaa lizima, hakuna mtu kati yetu ambae alipata hata chembe ya usingizi, nikashangaa Edward anaamka, kisha akaenda kuchukua vidonge vyake, nikamuuliza kwanini anachukua, akanambia ameshindwa kulala, nimkamzuia kisha nikamrudisha kitandani, maana nishajua mimi ndio dawa yake, nikalala kifuani kwake kisha nikaanza kumuimbia nakuja kumuangalia ameshalala kitambo, taratibu nikajitoa mwilini mwake nikashangaa kanishika, ikabidi nilale kifuan kwake, kweli tulilala mpaka asubuh, mpaka akapitiwa kabisa na alitakiwa kufika kazini saa moja kamili na wakati huo ilikuwa ni saa tatu asubuh, nikasema simuamshi, ila kumbe nikiamka mimi nay eye lazima aamke, kweli akaamka, kuangalia saa ni saa tatu...

umeona sasa wewe mtoto namna ambavyo nimepitiwa kwenda kazin na nilikuwa nina kikao saa mbili kamili, nikawa sina cha kufanya zaidi ya kucheka tu, na kumuambia sasa, tujiandae twende....

Akasema "hapana, leo ni siku yangu mimi kukaa na wewe, maana sijawah kulala kwa muda mrefu bila dawa nataman kuendelea kulala, akachukua simu yake akapiga simu kuwa hatofika kazini, akamkabidhi mtu majukum, kisha tukapika na baada ya kupika tukala na kusafisha nyumba, nilishangaa kwanini mtu kama Yule asiwe na wafanya kazi, kumbe aliwatimua, tukafanya kila mtu akaingia bafuni kuoga, na mara baada ya kuoga akataka nimuimbie, sikufanya hiyana, nikaanza kuimba hapo kanilalia kwenye mapaja nikaanza kuimba kweli alilala, akalala karibu masaa mawili...

Amekuja kuamka akawa ananiangalia kisha anatabasamu, ikabidi nimuulize mbona unatabasamu... " sauti yako inamaajabu gani, kwanini nalala kila nikisia sauti yako, akasema..

"ina uchawi, huoni nikikuimbia unalala tu, nikajibu akaanza kucheka, na mimi nikacheka..

Basi kwakuwa hakuwa amenigusa nikajua huyu hajanipenda, huenda ni kweli anataka kunisikia tu sauti yangu na anataka niwe karibu yake. kwakuwa namsaidia kukaa sawa na nasaidia asitumie dawa zake, kumbe mwamba kanielewa ila kusema ndio changamoto..

Kesho yake tukaenda kazini, akasema kuwa nitakuwa secretary wake, watu walishangaa maana watu wengi walikuwa wananifahamu maana nilitoka kufanya field muda mchache uliopita, sikukataa, akawa akitaka kwenda sehemu ambayo imamkusanyiko wa watu anaenda na mimi, kwa kuwa sehemu nyingi hazikuwa na kelele akawa akijiskikia vibaya ananishika tu mkono akaaa sawa, akajihakikishia kuwa yuko sawa, kumbe makelele yakizidi hata nikimshika mkono ni bure...

ITAENDELEA...Chapter 8

Basi kama mnavyojua mwanamke asiposifiwa wala kuambiwa nakupenda kuna namna anataman asikie, siku moja nimetoka kazini, nikasema nizunguke zunguke maana Edward alikuwa kwenye kikao, nikaparamiana na mwanaume mmoja, alikuwa ananukia balaa, alafu analips tamu, mpaka nikawa nataman kuzikiss, nay eye aliponiona ni kama aliduwaa na kunigeukia kisha akasema unaitw anani mrembo..

shimena, nikamjibu huku natabasamu na macho naangalia chini kwa aibu za kike..... owww unajina zuri kama wewe mwenyewe, shimena sijui ni kwanini ila nilipokuona kuna namna moyo wangu umedunda sana, nimejikuta nataman kukufahamu zaidi, akatoa bussness kadi yake kisha akasema kuna sehemu ya muhimu naenda ila naomba unitafute, naitwa Alfred kisha akaondoka zake...

Basi nikawa namuangalia huku natabasamu, mpaka nikahakikisha macho yangu hayamuoni tena, nikarudi zangu ofisini, nikawa nimekaa tu namfikiria huku natabasamu, kumbe Edward amerudi muda mrefu ananiangalia nikiwa natabasamu tu, akawa anashangaa nawaza nini hicho ambacho kina nipa furaha kiasi chote hicho, akaona asiendelee kunishangaa akanishika na kuniita" shimena...

Ndio nikashtuka, "ahhh boss Edward umekuja.. Nikashangaa ananiangalia kwa hasira kisha kwa sauti ya ukali kidogo akasema " nifate ofisini... Sikubisha nikaanza kumfata, ila nikashangaa hana cha kunipa nifanye, maana nilihisi labda anataka kunipa majukum, ila hakuna hata majukum yoyote yale ambayo alinipa na badala yake akawa kimya tu anafanya mambo yake... boss umeniambia nikufate ofisni, nikaanza kusema, akanifata kisha akanambia umeshapata mwanaume ee..

"mbona unaniangalia kwa hasira hivyo, kwani kuna shida gani kwa mimi kuwa na mwanaume na wakati mimi ni mwanamke, au unadhani nitakufa nikiwa single, mimi ni mwanamke bana hilo swali sio la kuniuliza, nikasema nikashangaa mtu amepanic, kisha akasema " nilijua tu, sasa hi hivi sasa hivi nimeshakaa sawa, sasa hata kama ukitaka kuwa na mtu unaruhusiwa na sitakaa nikusumbue kwenye maisha yako tena, nashkuru sana kwa kunisaidia ila hatimae nilishapona, unaweza kwenda ukaendelee na majukum yako..

Sikujua ni kwa sababu gani alikuwa ananipanikia kiasi chote kile, ila sikutaka kuzozana nae, nikakaa zangu kimya na kuendelea na mambo yangu na majukum kama kawaida....

Basi kama kawaida tukai nyuymban, alikuwa na hasira hata hakula, na hilo halikunisumbua sana, nikaenda kumpikia ila bado alikataa kula, kumbe mwamba kuna namna kuchanganyikiwa, hapo mimi namuwaza zangu Alfred tu, maana niliamin Edward ananitumia tu, na inatakiwa ifikie hatua na mimi niwe na maisha yangu na nipendwe...

Basi nikawa nambembeleza pale akalala, sasa kumbe kama akili yake haljatulia anakuwa analala usingizi wa maruerue mimi sijui, nilipohakikisha amelala nikachukua ile business card kisha nikamtumia sms Alfred maana bado muda haukuwa umeenda sana, ilikuwa ni kama saa tatu tu...

Tukaanza kuchart kwa raha zetu, hapo nacheka mpaka najisahau nacheka kwa sauti, ingawa nilikuwa chumba ambacho alikuwa Edward ila kwa namna nilivyokuwa busy hata sikuwa najua kama ameshaamka, basi nikashangaa naanza kukabwa, nilinyongwa mpaka nikashangaa huyu anashida gani, ila ghafla kuna kama kitu kikamjia kisha akaniachia na kukaa kimya akaanza kujikunyata kwa uwoga..

umefanya nini Edward kwa nini ulikuwa unataka kuniua, nikashangaa anaanza kulia usiniache shimena wangu, naomba uwe pemben kisha akasema naomba usiniache naomba yangu kila siku....

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

UDHAIFU WA MR CEO...Chapter 7--8  >>> https://gonga94.com/semajambo/udhaifu-wa-mr-ceo-chapter-7-8

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest