Time Flies.... Imepita miaka 11 na hapa ni Estádio Mineirão jijini Belo Horizonte.
Thomas Müller alianza kwa kufunga dakika ya 11
Miroslav Klose akaongeza dakika ya 23 – bao lililomfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia.
Toni Kroos akapachika mabao mawili (dakika ya 24 na 26)
Sami Khedira akaweka ubao ukasoma 5-0 ndani ya dakika 29.
André Schürrle alimaliza kazi kwa mabao mawili ya kisanaa, na kuifanya Ujerumani kufikisha saba.
Oscar akafunga la kufutia machozi kwa Brazil dakika ya 90.
Baada ya mechi David Luiz alisema “Nilitaka kuwapa furaha watu wangu. Samahani… samahani sana.”
Belo Horizonte, Sao Paulo, Rio de Janeiro ilikuwa kama Berlin au Munich. Mwenyeji alikuwa kama mgeni na mgeni alikuwa kama mwenyeji.
Mkweli Alcantara.