Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

*VERY HANDSOME* *🌸Lover boy💓💓01_05*

22nd Aug, 2025 Views 44


*__________________________________*

*SEHEMU YA 01*

Guys amkeni bhana mnalala sasa hivi mna raha gani 🤔, Penina aliongea kwa sauti hapo usingizi ndio ulikuwa ushaanza kunipitia na hivi punde nilikua nimetoka kunywa dawa za kutuliza mafua priton .
mafua yamenibana kiasi kwamba nilishindwa kwenda hata chuo leo hapo nina siku mbili tangu niripoti....
Nini bhana Penina unapiga makelele wakati unajua kuwa naumwa.. nilimjibu
Kwanza wewe bikira Maria lala hii haikuhusu wewe si unajidai mama mchungaji mimi namwambia Aggy....
Penina na Aggy ni watoto wa mjomba yangu kwahiyo hawa ni binamu zangu.
Wote umri wetu ulikuwa unalingana hatujapishana sana tukaanza shule mwaka mmoja hadi tukamaliza wakati huo mimi nasoma kijijini.
Tukamaliza kidato cha nne tukaenda tano na sita hadi chuo ndipo mjomba akanichukua ili anisomeshe pamoja na watoto wake....

Aggy hivi umemuona yule mkaka aliyekuja kuripoti leo chuoni 🤔 ..?
Ndio nimemuona kafanya nini tena...?
Hajafanya kitu ila wewe unamuonaje mbona ni Hb sana yaani yule atakuja kufanya watu wagombane sio siri ngoja tuone mimi tayari nishachanganyikiwa siwezi kuishi bila yeye walah 😁...
Mh Penny ushaanza huwezi kuishi bila yeye, yeye mwenyewe anajua hilo 😁 nilidakia.
Mh atajua mwenyewe ila nitahakikisha hachomoki kwenye kumi na nane zangu...
Angalia tu isije kuwa kumi na moja zako isitimie hiyo kumi na nane 🤣🤣 tukajikuta tunacheka wote..
Mimi nikapitiwa na usingizi asubuhi ilifika leo nilikua najisikia nafuu angalau..
Nilijiandaa tukaelekea chuo, nilifika nikaenda kukaa sehemu ya nyuma sipendi kukaa mbele mimi ni mtu mwenye asili ya aibu 😌 .
Mara akaja huyo mkaka aliyemsema jana Penina.
Wadada walibaki wanamshangaa aliingia akakaa mbele ambapo watu wanaogopa kukaa..

Mkaka HB kweli msafi sana halafu ni bishoo nikajisemea moyoni hapa lazima watu wachanganyikiwe anyway watajijua wenyewe mimi hainihusu...
Lecture aliingia darasani kufundisha somo lenye mahesabu alifundisha kidogo tu kisha akatoa quiz.
Hii quiz mtaifanya kwa makundi ili nione uwezo wenu kesho mtanikusanyia sasa sijajua mtapangaje hayo makundi? Lecture aliuliza

Yule kaka alinyoosha mkono ✋ ili atoe wazo..
Okay simama hapo naona umenyoosha mkono pia ningependa ujitambulishe jina kisha utoe wazo lako..
Asante sana sir Naitwa Gerson hayo makundi tuyapate kwa kuhesabu namba kila mtu moja hadi nane kisha kila mtu aende kwenye namba yake asanteni.
Yah wazo zuri anza kuhesabu wewe mwenyewe namba...
Basi Gerson alihesabu namba moja wengine wakafuata hadi namba nane , akaanza mwingine hivyo hivyo hadi namba nane wadada wakawa wanatamani na wao igonge kwenye namba moja 🤣 nilijikuta nacheka huku nilimuangalia Penny...
Mungu sio athumani akaangukia namba moja

niliona amefurahi...
Nikiwa sina hili wala lile namba ikaishia kwangu moja hivyo tukajikuta tuko kundi moja na Gerson hilo kwangu halikuwa na umuhimu sana ....
Itaendelea dears❤️.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*VERY HANDSOME* *🌸Lover boy💓💓01_05*  >>> https://gonga94.com/semajambo/very-handsome-lover-boy-01_05

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest