Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓03

24th Aug, 2025 Views 25



Nilishusha pumzi huku haja ndogo ikinibana kwa presha nilinyanyuka nikaomba ruhusa ya kutoka nje ili niende uwani...
Huku nyuma Gerson alienda pale mbele alielekeza mwanzo hadi mwisho watu wote wakajikuta wanaelewa hadi lecture mwenyewe alipiga makofi....
Nilirudi darasani nikakuta ni muda wa mapumziko kila mtu alikuwa ananisifia wa kwenye grupu letu moyoni wangejua hata sijafanya mimi hiyo kazi 😁 ..

Nilimuona Gerson yupo amekaa na rafiki yake wanakula, nikaamua niende nimfuate nikaenda kukaa pale alipo wadada waligeuka kunitazama akiwemo Penina..
Ulisema nije.... Anhaa umekuja madam Angel 😇.
Jana nilijua tu hutaweza kufanya hizi hesabu ndio maana nilienda kufanya na mimi nyumbani binti gani mrembo halafu kichwani hamna kitu
Unakaa nyuma ya darasa unategemea lecture akifundisha na wewe uelewe hivi inaingia akilini kweli 🤔.

Sasa kuanzia leo kaa mbele ya darasa ili uelewe vizuri ..
Sawa niliitikia nikaondoka huku nikiwa nimekasirika sana niliona kanidharau.
Nilijua ananiitia kitu cha maana kumbe ananiita ili anichambe mfuyuuu nilisonya..
Nilienda darasani nikaenda sehemu nayopenda kukaa nikakaa nikawa najisomea kitabu cha hadithi....
Penny na Aggy walikuja mahali nilipokaa.
Naona ukaribu wenu unashamiri wewe na Gerson.... Aggy aliongea

Ukaribu gani 🤔 kwenda kumuuliza maswali ndio ukaribu kwanza hivi mshawahi hata kupiga stori na yule kaka 😁 ni ana dharau balaa hawezi kuwa na mahusiano na mtu mjinga mjinga kwahiyo Penina naomba ujipange tena ujipange haswa ni hilo tu nikutakie ushindi mwema kwenye hilo.....
Mh sawa ngoja tuone.... Penina aliongea

Masomo yaliisha jioni watu wakatawanyika mimi nikaamua nibaki zangu, nilikaa darasani kulikuwa na baadhi ya wanafunzi wengine wachache wamebaki nao walikuwa wanajisomea...
Niliinuka nikaenda maktaba ili niazime kitabu kinachohusiana na mambo ya udongo...
Hapa nisiwachanganye tulikuwa tunasomea mambo ya kilimo...

Mjomba yangu yeye alikuwa ni afisa kilimo na mifugo hivyo alipenda na watoto wake na sisi tusomee hayo mambo...

Nilifika maktaba nikaingia nikawa nazunguka kwenye shelf natafuta kitabu nachotaka nikasikia madam Angel....
Niligeuka kutazama nani huyo anayeniita..
Alikuwa ni Gerson amekaa anasoma kitabu huku anaandika.....
Ge.... Gerson kumbe upo huku? Nilimuuliza huku nikiwa na kigugumizi moyoni nikachukia why nimemkuta huku huyu 😌 ..

Yah nipo najisomea mida ya jioni kama hii napenda kuja maktaba kupata maarifa..
Vizuri nilikuja kutafuta kitabu cha soil science kuna vitu nataka nijue...
Oh vizuri ngoja nije nikutafutie kitabu kizuri cha kwenda kujisomea...
Sawa niliitikia

Aliinuka akaja niliposimama akawa anatafuta kitabu mh hiyo harufu aliyokuwa ananukia na hiyo pafyumu aliyojipulizia nikatamani hata anikumbatie basi akawa ananigusa gusa.....
Hicho hapo nenda kajisomee ni kizuri kinakufaa alinipa kitabu...

Itaendeleaaaaaa

NAMBA YA MALIPO 0742133100.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓03  >>> https://gonga94.com/semajambo/very-handsome-lover-boy-03

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest