Nilivyomaliza kuchati nilifuta meseji maana akina Penina huwa wanapenda kuniazima simu yangu muda mwingine sikutaka wajue kama naongeaga nae.....
Usiku usingizi haukuja nilikua naona kunachelewa kukucha asubuhi ilivyofika niliamka mapema nikafanya shughuli zangu nikajiandaa nilivaa gauni langu refu zuri nikamuaga shangazi kuwa naenda kumtembelea rafiki yangu wa chuo shangazi aliniruhusu akaniambia nirudi mapema nyumbani nisichelewe....
Nilifurahi huyo nikaondoka nikaelekea stendi nikapanda hice zinazoenda banana... Nusu saa nikawa nimefika nilisimama sehemu tuliyokubaliana anikute....
Kweli nilikaa kidogo saa mbili na dakika tano akawa ameshafika sikugundua kama ni yeye maana alikuja na gari nyingine.....
Angel aliniita..... Enhe kumbe ni wewe nishakariri gari yako nyeupe leo umekuja na nyingine nyeusi....
Niliingia kwenye gari ๐ tukaondoka kuelekea nyumbani kwake tukapita majumba sita hadi kinyerezi.....
Tulifika kwenye nyumba ๐ moja nzuri ilikuwa na geti alipiga honi mlinzi alikuja kufungua geti akaingiza gari ndani....
Alipaki gari tukashuka tukaingia ndani ....
Karibu hapa ndio nyumbani kwangu ....
Asante ๐ niliitikia huku nikiangaza huku na huku nikaona picha ipo ukutani mtu kavaa nguo kama za jeshi....
Gerson wewe ni askari? nilimuuliza alijikuta anapatwa na kigugumizi kidogo akajibu no hiyo picha ni ya pacha wangu hata hivyo hayupo hapa....
Sawa niliitikia ila sikuridhika na majibu yake niliona kama ananidanganya....
Alienda kwenye friji akaniletea juisi ๐น asante ๐ nashukuru nilichukua nikaanza kunywa taratibu.....
Unakaa mwenyewe? Nilimuuliza
Ndio naishi mwenyewe vipi unaogopa kupigwa ๐..
Ndio mwisho aje mke wako anikute hapa mimi kupigana siwezi nilimwambia..
Ondoa shaka bado sijaoa hakuna wa kukupiga jimbo lipo wazi..... Vipi wewe shemeji yetu ajambo...?
Gerson sina hata huyo mpenzi mwenyewe...
Sawa sasa mimi mgeni akifika nyumbani kwangu anakuwa mwenyeji mama ingia jikoni..
Jiko lako kila kitu kipo upike tule...
Sawa nilimjibu nikainuka nikaelekea jikoni nilikuta kuna kila kitu nilitoa vitu navyotaka kupika nikapika wali na samaki ๐ wa nazi kulikuwa na matunda nikatengeneza na juisi ๐น.......
Nikiwa jikoni wakaja wageni watatu walikuwa marafiki zake....
Alikuja jikoni akaniambia kuna marafiki zangu wamekuja wapo sebuleni wanataka wakusalimie...
Gerson kwanini umesema nipo jamani ujue naona aibu ๐ ... Nilimjibu
Tafadhali nakuomba nisingependa waondoke bila kukuona.....
Haya sawa nakuja..... Nilimjibu huku nikinawa mikono yangu nikajifuta maji nikavua apron nikaenda sebuleni..
Gerson alivyoniona alifurahi akawaambia wenzake huyu anaitwa Angel, Angel hawa ni marafiki zangu...
Asante ๐ Angel tumefurahi kukuona shemeji yetu... Nikashangaa ohoo tena nimekuwa shemeji ya ghafla ghafla bila taarifa....
Ikabidi tu niitikie kishingo upande..
Na mimi nimefurahi kuwafahamu ๐ nikalazimisha na tabasamu la uongo na ukweli.
Hapa lazima tuhakikishe tunaoa mtoto mzuri kama jina lake wewe ni malaika umeshushwa moyoni nikajisemea hawa mashemeji kazi yao ni kupamba tu hata kama mko kumi....
Sawa mimi nipo jikoni ngoja niandae chakula ili mle.... Nilienda jikoni nikaanda chakula wakala kisha wakaondoka mimi nikaosha vyombo nikamfuata Gerson nikamwambia muda unaenda nataka niende nyumbani...
Akaniambia usiondoke kwanza nina mazungumzo na wewe ...
Itaendelea
VERY HANDSOME
๐ธLover boy๐๐10
Mazungumzo gani ๐ค tena hayo mbona unanitisha Gerson.... nilimwambia....
Alikuja hadi niliposimama akawa ananiangalia usoni mimi nikawa naona aibu ๐ nikawa naangalia chini....
Haya nimekuita nataka tuongee mimi na wewe face to face naona kama kuna kitu unataka kuniambia ila unashindwa be free Angel... Gerson aliongea huku akinisogelea na mimi nikawa narudi nyuma...
Mbona unarudi nyuma hujawahi kusogelewa na mwanaume zero distance...
Gerson naomba niondoke nataka kurudi nyumbani....
Nyumbani nitakurudisha tena hadi kwa mjomba wako nitamwambia ulikuwa na mimi...
Kwanini nikiwa na wasichana wengine unachukia? Unanipenda....
Gerson aliniuliza swali nikajikuta napatwa na kigugumizi cha ghafla.....
Gerson unaniuliza swali gumu nashindwa kukujibu....
Ukiona mtu anashindwa kujibu it means kwamba jibu ni Yes.....
Alinisogelea zaidi akanibananisha ukutani oh my gosh nilijikuta napandwa na hisia nikaanza kuhema kama nakimbizwa akawa anapumua karibu na lips ๐ zangu... nikataka kutoka akanizuia akaanza kuninyonya mate,....
For the first time nikawa nimekunywa juisi ๐น ya wakubwa ๐nikajikuta nampa ushirikiano.
Alininyonya kama dakika mbili ndipo akaniacha
Nakupenda Angel naomba unijibu na mimi kama unanipenda...
Weuh nani akatae nilikua nataka aanze kusema yeye kuwa ananipenda ....
Ndio nakupenda โค๏ธ....nilimjibu
Asante ๐ nashukuru kwa kunipenda nahaidi kukujali na kukuheshimu siku zote nilikupenda tangu mara ya kwanza niliyokuona na niliona unanifaa na sio wengine wapo kwa maslahi muda umeenda sasa twende nikupeleke nyumbani kwenu mjomba wako asije akakufukuza ๐.
Sawa... Nilichukua mkoba wangu nikavaa sandles zangu nikatoka nje kumsubiri...
Yeye akaenda kuvaa shati baada ya dakika tano alitoka akaniambia niingie kwenye gari ๐.
Alinipeleka hadi nyumbani akaniacha mtaa wa pili na nyumbani kwetu kabla sijashuka alifungua wallet yake akatoa pesa laki akanipatia...
Itakusadia hii kwa matumizi yako naomba nikuache tutaonana wiki ijayo kesho nasafiri kikazi...
Sawa..
Nilishuka kwenye gari ๐ nikaelekea nyumbani.
Angel ndio unarudi sasa hivi ๐ค toka asubuhi yaani una bahati baba na mama wamechelewa kurudi ..... Aggy aliongea.
Sikuenda mbali nilikua hapo banana kwa rafiki yangu...nilimjibu
Mh rafiki gani huyo hapo banana halafu mbona kama hiyo harufu ya pafyumu naijua mhh hii harufu ni ya Gerson ulikuwa na Gerson sema ukweli...
Sikuwa nae sijui anakaa wapi pili kwani pafyumu anayo yeye peke yake hapa duniani mbona mnapenda kumuhusudu mtu jamani...
Sawa wewe ficha tu duniani hakuna siri ujue..
Sasa dada Aggy nifiche nini mimi kama wewe unaona ni rahisi kutembea na Gerson mfuate..
Haya mama.....
Nilienda chumbani nikajitupa kitandani nikaanza kuwaza lile busu ๐ alilonipa Gerson
Nilitamani muda huo tungekuwa wote amenikumbatia....
Kweli alikaa kimya wiki moja bila kunitafuta nilijihisi mpweke sana nilikua nikimtumia text zinagoma kabisa hata nikipiga simu haitoki hadi nikapotezea..
Jioni moja tukiwa tumekaa simu yangu iliita alikuwa ni yeye nilifurahi, niliinuka nikaenda kuongea na simu nje wenzangu wasisikie.
Alooh hatimaye leo umenipigia simu ulikuwa wapi siku zote hizi jamani? Nilimuuliza
Nilikuambia nasafiri kikazi hata hivyo ndio natoka airport hapa ndio narudi.....
Waoh nimekumisi sana.....
Njoo nione..... Gerson aliongea
Mh sasa hivi ๐ค jioni hii nitarudi saa ngapi? nikamuuliza...
Itaendeleaaaaaa.
Maoni