,
na kwamba ndimi zetu, baada ya kumuona yeye, huendelea kumuombea dua yeye na aliyemlea(mama na baba yake).
Yaani wao wanapojistiri ni kama vile wao ni mahuurul Ayn wa duniani walioumbwa ili waweze kuwarekebisha na kuwafunza watu ubinaadamu ni nini.
Kila mwanamke anapojisitiri na kujiheshimu, huongezeka uzuri na nuru (mwanga wa ndani) na hukua thamani yake na kuheshimika yeye na walio mpa malezi.
Ee Mola, waongoze wanawake na mabinti wa waumini,
wavalie vazi la haya, heshima na sitara (staha),
uwatie nguvu katika utiifu wako na ibada njema kwako pale wajapokutana na maneno ya kuwabeza na kuwakatisha tamaa mfano kuambiwa unajizeesha,
Ewe Mola wa walimwengu wote kubali, aamiin.