Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

WAKILI HUCHOKI JAMANI❀ EP 13...14

10th Sep, 2025 Views 37



Nilikuwa mkimya mpaka akashangaa, mbona leo umepoa sana, sijakuzoea hivyo ety, nilifunika macho na mikono tukakaa kwenye viti, kwa jinsi nilivyokuwa na furaha, niliogopa ata kuongea, nilihitaji kwanza kutuliza ile furaha, nisije nikaongea vitu vya ajabu bila kujua,niliamua kumlalia tu mapajani, aliniweka vizuri akawa ananiongelea sikio, lile joto la mdomo, nikaona kabisa linanivuruga nikainuka, nilikuwa hoi, alivyonitizama tu mwenyewe akajiongeza, akaniuliza tu, "hatuwezi fanya mbinu tuondoke wote? Ilibidi tu nicheke, nikajibu leo haiwezekani ninahitaji kutulia kwanza nyumbani kidogo, alinitizama sana, mpaka ujasiri wa kutizamana nae ukaniisha, na sio kawaida yangu huwa namkazia sana..

Alisema dah leo nimepata kitu kingine cha ziada, nilishangaa ila nikashindwa ata kuuliza, ilibidi tuagane tu, ili waondoke, tuliwasindikiza kisha tukarudi sasa, mimi nilikuwa na kesi ya kutotoa taarifa nilijua nitasemwa mpaka basi lakini cha ajabu sikugombezwa ata kidogo, adi nikauliza leo mama yuko vizuri adi ajanigombeza nilijua apa wageni wakiondoka kutakucha...

Mdogo wangu wa kiume akadakia nakujibu, "anaanzia wapi kukugombeza akati wewe ndo umewafunika wote walioolewa humu ndani hakuna aliewahi kulipiwa mahali kubwa kama yako, yani mahali yako, ukijumlisha mahali zao wote bado hakuna awaifikii mahali yako, wote walicheka kasoro yule mdogo wangu mwenye roho yakukunja, ikabidi tunyamaze tu, Judith mdogo wangu alifurahi mno, alionesha furaha yake wazi wazi, mama akaanza kuhangaika mala ooh tutavamiwa naomba tugawane hizi pesa ziende ata benk usiku huu huu, yani hakuwa na amani kabisa, uzuri ilikuwa saa mbili mbili tu, ilibidi tuwahi tu tukaziweke kwenye acount, apo ndo amani yake ikapatikana , akaanza sasa kunisifia nilijua tu binti yangu ipo siku ataniheshimisha ilibidi tu tuanze kuminyana make πŸ™Œ...

Baba akamwambia aache unafki si ni yeye kila siku alikuwa ananipa pressure niolewe mara ananiletea wanaume wanuka maziwa,ugomvi ukaibuka tukaona apa tuwaachie tu wenye ugomvi wao tukalale, asubuhi tuliamkia kikao, make tayari walipanga mpaka tarehe za ndoa na sendoff, tulikubaliana kabisa sendoff tutafanya ya pamoja ndoa ndo tarehe zilitofautishwa kwa sababu ni sehemu tofauti tofauti,na familia pia ni tofauti, tuliweka mikakati yetu sawa, na kuamua kuanza kusambaza card, baada ya kikao nilirudi na mwanangu kwangu..

Tulivyofika tu, tukakuta gari ya Albert iko nje, nikajiuliza huyu alijuaje kama nakuja, kumbe ameshapata wakumpa ubuyu, yule mdogo wangu wakiume,nilifika nikafungua akaja tukasalimiana, leo nilimsalimia kwa heshima mno sio kama zamani...
Itaendelea....πŸ”₯

EP 14.

Adi mwenyewe akashangaa, tuliingia ndani, nikaingia kupika, akaja jikoni apo B kafikia kwenye zawadi za baba ake ata hana habari tena na sisi, B alikuja taratibu kabisa akanikumbatia kwa nyuma, nilishtuka nikajikaza ila tayari mwamba alikuwa kashaniweza vibaya mno, yaani saivi akinigusa tu vitu vinaitika vyenyewe, hakuwa kagundua ata angejua ningeliwa vibaya mimi🫣, alinikumbatia kwa muda kisha akauliza kama anaweza kunisaidia kuandaa viungo, nilikubali kwa kichwa niliogopa kuongea atanigundua...

Alinigeuza nimtizame, nilishindwa kumtizama kabisa kwa aibu nilikuwa nashusha tu macho, alipumua kwa shida kama mtu aliezidiwa, nikanyanyua uso nimzoom kama ninachohisi ni kweli? Nilivyoinua tu macho kumtizama, tukakutana macho kwa macho, niligeuka haraka kujitia bize kumbe nishabambwa naibia kumtizama, ila nayeye niligundua kabisa kashavurugwa apa kama sio B ningeliwa uku uku jikoni kirahisi kabisa...

Niliamua kumpa kazi aache kunimezea mate, alianza kuandaa viungo tukasaidiana kupika, nikatenga tukala, nilikuwa na ratiba ya kwenda kwa bibi nikamuone, make nina muda na ndie mtu alienisaidia sana kwenye uzazi, hakuwahi kunikoromea hadharani, alinionya taratibu, na kunirekebisha, ili nisirudie kosa, niliwaza apa natakiwa kuomba ruhusa, sasa ata sijui naanzaje, nilikuwa natapatapa mpaka Albert akahisi kabisa kuna tatizo, naogopa kusema...

Akaamua kuniuliza nina jambo gani? Nilishusha pumzi nikasema nilikuwa naomba ruhusa niende na B kwa bibi nikamtembelee, nina muda sijaenda na ndiko nilikojifungulia B, na hata hajajua kama umekuja nilitaka nikamwambie mwenyewe, " Joy yani hilo tu mama ndo linakufanya unahangaika muda wote huo unaogopa kuongea? Mbona ni jambo zuri tu na siwezi kukukatalia, ila naomba tu twende wote...

Nilikubali na kushukuru, nikashangaa ananitizama kwa matamanio huku anasema nimependa ulivyo mtulivu na heshima kwangu sio siri unazidi kunivuruga hio akaimalizia sikioni, B alitutizama akasema, mnirudishe kwa bibi yangu, nyie mnacheza tu wenywe, mimi mnaniacha nacheza peke yangu,ilibidi tu tucheke, tukaanza kucheza nae akafurahi mwenyewe...

Badae nikataka kumuogesha akakataa, nakuomba akaogeshwa na baba ake, kuna mambo ya kiume anahitaji kuongea na baba ake, nyie nilijikuta tu mbavu zinauma kwa kucheka, ata baba ake hakutarajia, alimchukua mwanaume mwenzake wakaongee hayo mambo ya kiume pembeni, niliwaandalia nguo, nikatoka kuweka uwanja wangu sawa, nikarudi nakuta washavalishana wanafuraha wenyewe, nikawaambia nitakuja kuwajibu ipo siku tu, Albert akajibu, saiv ina bidi tulete kabinti ili muungane, B akajibu ewaa baba mimi nimeshakuwa saivi, niliwatizama nakuwauliza mnazani ni rahisi eee?...

B akajibu yaani mama bwana kwa kudeka, aya kuna ugumu gani apo akati baba yupo, si uliniambia mpaka baba awepo ndo atanitafutia mdogo wangu? Tobaaa nilijikuta naona aibu nikatoka sebreni, wakaanza kucheka, B alipitiwa usingizi, baba mtu akaja ehee safari ni lini mamaa? Na tunaendaje? Kama inawezekana naomba tuandae bajet pamoja kwa ajili ya bibi, ili tuhemee, na tutumie tu gari yangu kwenda ama unaonaje?...

Nilijibu tu nisawa haina shida, tuliandaa bajet, na jioni tukaenda kuhemea kwa ajili ya safari,usiku Albert aliomba kulala na mimi, nilijikuta natetemeka kwa uoga utazani simjui, niliomba kwanza anipe mda, alielewa akalala na mtoto wake,kulikucha tukaamkia safari,tulifika nilikuwa nishampa taarifa bibi, na pesa ya maandalizi na kuongeza kagodoro make nilimjengea bibi nyumba japo niyakawaida lakini kwa kijijini ilikuwa nzuli mno, na vioo nilimuwekea, ilikuwa ya vyumba vinne self viwili na sebre, jiko,store na bafu..

Ila nilikuwa nimenunua vitanda tu bila magodoro, nikaona niagize ile jana viende na gari ili mgeni asikose, nilinunua kisiri siri tu, kujenga nilisaidiana na shangazi yangu mdogo, maandalizi yalikuwa vizuri tumefika kila kitu kiko sawa, tumechinjiwa, na B anampenda bibi yangu kuliko ata wake πŸ˜ƒ, akiwa huku anatuzwa mno, alifurahi akamtania kamletea mme...

Tulishusha mizigo na zawadi za bibi, tukaombewa kwanza ndio mambo mengine yakafata, tukiwa bize na ugeni Albert akawa anapigiwa simu anakata nikamuuliza kuna emergence kama ipo aende tu amuage bibi, make najua kazi zake hazina muda maalum hasa hao wateja, alisema kwa leo haondoki atashughulikia kesho, sikuwa na pingamizi, tulikula kuku zetu pale kwanza tukaanzia supu ya kienyeji supu supu kweli...

Itaendelea...πŸ”₯
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

WAKILI HUCHOKI JAMANI❀ EP 13...14  >>> https://gonga94.com/semajambo/wakili-huchoki-jamani-ep-13-14

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest